Bachelet alaani mashambulizi ya Bolsonaro kwa mahakama za Brazil

Bachelet alaani mashambulizi ya Bolsonaro kwa mahakama za Brazil

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mkuu wa haki za binaadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet amemkosoa vikali Rais Jair Bolsonaro akisema ameongeza mashambulizi yake kwa idara ya mahakama nchini Brazil na mfumo wa upigaji kura kabla ya uchaguzi wa Oktoba.

Bachelet ameonya kuwa hali hiyo inasababisha kitisho kwa demokrasia. Mkuu huyo wa haki za binaadamu ambaye anakamilisha muhula wake wiki ijayo, amewaambia waandishi wa habari katika kikao chake cha mwisho ofisini mwake kuwa ni jambo la kutia hofu kuwa Bolsonaro anawataka wafuasi wake kunadamana dhidi ya taasisi za mahakama.

Bachelet, ambaye mwenyewe aliwahi kuwa rais wa Chile mara mbili, amesema wakuu wa nchi wanapaswa kuheshimu taasisi nyingine kama vile mahakama na bunge.

Matamashi yake yamejiri wakati kukiwa na hofu kuwa kiongozi huyo wa Brazil wa siasa kali za mrengo wa kulia ambaye yuko nyuma katika tafiti za maoni, huenda akakakataa kuheshimu matokeo ya uchaguzi wa Oktoba ikizingatiwa jitihada zake za mara kwa mara za kutilia mashaka mfumo wa upigaji kura nchini Brazil.

Brazil hutumia mfumo wa kielektroniki, lakini Bolsonaro anataka paweko na karatasi inayotolewa kwa kila kura inayopigwa.
 
Back
Top Bottom