Bachelor: Mbinu za kuosha vyombo.

Bachelor: Mbinu za kuosha vyombo.

kizaizai

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2010
Posts
5,651
Reaction score
6,966
Mimi kupika siyo tatizo, kwani nifundi kupita wanaweke wengi tu, tatizo nikuosha vyombo. Mbinu gani nitumie ili vyombo vilivyotumika kupikia na kulia chakula visikae zaidi ya masaa 5 bila kuoshwa.
 
Mimi kupika siyo tatizo, kwani nifundi kupita wanaweke wengi tu, tatizo nikuosha vyombo. Mbinu gani nitumie ili vyombo vilivyotumika kupikia na kulia chakula visikae zaidi ya masaa 5 bila kuoshwa.

Jitahidi kuosha vyomba wakati unapika....kwa mfano unapopika mchuzi ukisha maliza kutayarisha mahitaji kabla kupika osha vile ulivyotumia....wakati mchuzi uko hatua ya mwisho,tuseme unasubiri kuzima moto tumia nafasi hiyo kuosha vilivyopo....Mfano umepika wali hakuna sababu kuacha chakula katika sufuria,chakula kipakue katika chombo kingine tia maji sufuria naibandike jikoni hata ukimaliza kula chini ukoko umeachia unachanganya na vile ulivyotumia wakati wa kula unaosha lakini ukisubiri mpaka umalize kula ndio uoshae utaona uvivu li siku.
Mimi binafsi sipakui chakula mpaka nihakikishe nimeosha vyombo nilivyo tumia wakati wa kupika.
 
Back
Top Bottom