Hiyo taaluma sio mpya kama ulivyoiweka wewe. Vijana wengi tu wamehitimu tayari na taaluma hiyo ya architecture in interior design na kwa sasa wanaifanyia kazi.
Tofauti kubwa ya Architecture, landascape na interior design ni kwamba (generally zote ni Architecture):
Architecture - hii ipo general na kazi yao kubwa ni ku-design the general premise ya building. Floor plan ipo hapa sana.
Land scape - hii ni kwa ajili ya ubunifu wa nje (landscaping). Hawa ndio wanahusika na urembo wote unaouona nje ya jengo, kama vile swimming pools, upambaji maua, njia za miguu, parkings na mapambo mengineyo. Kwa mfano, kuna mama mmoja (jina nahifadhi) ndio alipewa tenda ya kufanya design hii pale kwenye ukumbi wa bunge.
Interior design - hawa uwa wana husika na ubunifu wa ndani tu (ingawa wana knowledge vile vile ya floor plan), kama kuweka partitions kwenye jengo na mapambo mengine.