Mimi hapo umenikumbusha mbali sana. Nadhani ni zaidi ya miaka 17 nyuma. Nakumbuka kwa mara ya kwanza kusikia kibao hicho kilichokuwa katika album ya Kala-yi-boeing ni mwaka 1992 na vibao hivyovilikuja kuvuma sana mwaka 1993 na kuendeleaa ambapo mpaka leo nikisikia kwenye redo ni kama vitu vimetoika studio.
Mtunzi wake ni Adolph Dominguez, nakumbuka watuma salamu mbalimbali wa kipindi hicho kwenye redio fulani kama Mtu shapu Spencer Love Kalamkumnsa, sijui yuko wapi huyu.
Kwa mtu wa karibu anajua nazngumzia redio gani.