Bad news to PM Majaliwa and VP Mpango; The Tanzania-Dubai Treaty is covertly open-ended for facilitating ‘Arab settler colonialism’ in Tanzania

Tibaijuka ana shida sana
Katapeli viwanja Kigamboni na Bagamoyo..bado hatosheki

Sheria ya ardhi inaweka ukomo wa viwanja vingapi kumilikiwa na mtu mmoja?
Waliotapeliwa wamekwenda mahakamani?
JF is not a castle of speculations!
Think big by the help of evidence without shouting!
 
Nice piece...

Only to realize that instructions already made and to your surprise damage on DP side in terms of "financial resources" is done.

So we don't expect much, come what may... looks like embarrassing to the state decision makers and no turning point, unless the consequences become so vivid.

Unfortunately, CCM have this luxury of rulling and dictating whatever they want with little to no impact on power control to this beautiful nation.

Remember, who paid the piper, choses the tune.
 
I fully support your article. We don't see many of these articles today, especially on the crosscutting issues in Tanzania. However,I kindly, request it's publication in well known newspapers in East African region.
Congrats.
 
‘’Their being products of settler colonialism makes it difficult for them to see why the Tanzania-Dubai Treaty is nauseating!’’

Hapa Umedhihirisha Ushenzi na Ubaguzi. Huenda ikawa una hoja, ila hoja zako zinaanza kuonyesha upande uliojikita katika udini, ama chuki dhidi ya Zanzibar.

Ninaomba ufute mara moja kauli yako hiyo.
Wote hao ambao ni marais wa nchi zetu ni raia halisi wa Jamhuri Ya Muungano.
Kumkosoa mtu kisa asili yake ni ushamba na ulimbukeni. Jitahidi kuficha chuki zako.
 
Ndefu lakini nimeisoma na nimeielewa vyema.. Sana hasa hicho kipengele cha jamaa kuja kuwekeza Lupita FDI.. for the fact that hatuna undugu nao in terms of historical background n.k Bora kidogo wachina tunawajua sio Hawa wezi WA Wanyama wetu kwenye mbuga zetu za Wanyama na madini..

Wazee WA mtumikieni kafir ili Mambo yako yaende mpoo??
 
Rubbish 🗑️🗑️
 


Fahamu haya:

1. Tanzania ni dola ammbayo kwa historia yake imetokana na nchi mbili huru: Tanganyika na Zanzibar

2. Tanganyika ilikuwa chini ya ukoloni wa waporaji (extractive colonialism), ambao hatimaye waliondoka baada ya mchakato wa ukolonuzi (decolonisation) kukamilika.

3. Hii mmaana yake ni kwamba, utaifa wa Tanganyika umejengwa juu ya mapokeo ya wakazi wenyeji wenye asili ya kibantu (Bantu natives), na wageni waliobaki nchini Tanganyika wanalazimika kujijumuisha kwenye jamii za wenyeji ili kutembea kwenye nyayo za wenyeji hao.

4. Zanzibar ilikuwa chini ya ukoloni wa walowezi (settler colonialism), ambao hatimaye walibaki nchini Zanzibar baada ya mchakato wa ukolonuzi (decolonisation) kukamilika.

5. Hii maana yake ni kwamba, utaifa wa Zanzibar umejengwa juu ya mseto wa mapokeo ya wakazi wenyeji wenye asili ya kibantu (Bantu natives) pamoja na mapokeo ya walowezi, ambapo wageni waliobaki nchini Zanzibar hawalazimiki kujijumuisha kwenye jamii za wenyeji ili kutemmbea kwenye nyayo za wenyeji hao.

6. Hivyo, baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliozaa Tanzania, kulizaliwa dola mpya yenye utaifa chotara, hasa kutokana na historia ya upande wa Zanzibar. Kilichotokea ni kwamba waasisi wa dola mpya waliunda "utamaduni mpya," ambao unajumuisha mema kutoka upande wa wazawa na wageni, kwa misingi ya maadili asilia yanayozingatia hulka ya ubinadamu. Utamaduni huu mpya na jumuishi unaitwa "overlapping consensus."

7. Hata hivyo, watu waliozaliwa miaka ya 1960 bado hawajasahau mapokeo yao ya kisekta, yaani ama mapokeo ya kibantu au mapokeo ya kiarabu. Kati yao ni Samia Suluhu Hassan na Hussein Mwinyi ambao wamelelewa katika mapokeo ya kiarabu.

8. Fikra za binadamu zinaongozwa na "worldviews" alizookota wakati wa malezi yake. Maara "worldview" ni kama lenzi yenye kioo kinachotuwezesha kuona kilicho katika mazingira yetu. Kama kioo kina rangi nyekundu tunaona kila kitu kina rangi nyekundu. Hivyo, mtu akikwambia kwamba kitu mnachokiangalia kina rangi ya njano mtabishana hadi kesho.

9. Ni hoja yangu kwamba, huenda kwa sehemu kubwa, fikra za Samia Suluhu Hassan na Hussein Mwinyi bado zinaongozwa na "Arab settler colonial worldview," wakati fikra za wanasiasa wabantu zinaongozwa na "Native bantu worldview." Katika nyakati za leo "colonial worldview" haina nafasi tena, japo mabaki yake bado yanatusumbua. Mkataba was DPW ni ushahidi tosha.

Niko tayari kukosolewa kwa hoja na sio vinginevyo.
 

Hoja namba 3 ni Fallacy. Ni kweli kuwa zilikuwepo jamii za kibantu na jamii zisizo za kibantu nchini Tanganyika. Lakini hakuna ushahidi wa kimantiki wa moja kwa moja kuwa jamii zenye asili ya kilowezi zilizama katika kufuata unyayo wa makabila mengine ambao ni wenyeji.
Hii hudhihirishwa wazi na uwepo wa jamii nyingi nchini zenye kufuata mila na tamaduni tofauti tofauti mbali na jamii nyingine. Uwepo wa umoja na mshikamano haimaanishi kuwa jamii za wamasai zifate jamii za wasukuma. Au jamii za waswahili zifuate jamii za wabantu. Jamii hizi hujumuika kijiografia. Si kitamaduni wala kiitikadi asilia.

Hoja namba 5 pia si kweli. Hakuna ushahidi wa moja kwa moja kuwa Zanzibar ina watu asili wa kibantu. Wabantu nao walihama toka magharibi mwa Afrika kuja Mashariki mwetu.
Nikupe mfano, Historia inaonyesha huenda Zanzibar ikawa imepokea walowezi hata miaka elfu mbili nyuma. Wabantu nao walihamia kama walivyohamia waarabu na wasomali. Zanzibar ilikuwa na wenyeji wake. Wabantu kwa pale Zanzibar si wakaazi halisi bali nayo ni jamii iliyolowea na kuchangamanyika humo.

Hoja namba 6 nayo si kweli. Hakuna utamaduni wa pamoja kati ya Zanzibar na Tanganyika. Zanzibar kwa wingi wao ni waislamu. Hubebwa na utamaduni mwingi wa Uislamu na uchache mno wa dini za kitamaduni. Tofauti na Tanganyika ambapo utamaduni wake umejengwa kwa wingi katika misingi ya utamaduni wa kikabila na utaratibu wa wakoloni. Kama uliisoma sheria vizuri utagundua Gavana wa Tanganyika alizikubali tamaduni zote zile ambazo hazikuwa A Repugnant to justice and morality according to the British Views. Hivyo basi hakuna utamaduni mpya ulioundwa na waasisi wenye kubeba mema baina ya pande zote mbili.

Hoja namba saba nayo pia ni Fallacy. Kuzaliwa katika mapokeo ya kimabadikiko hakukufanyi kutokuwa na mtazamo tofauti.
Hoja kuu ni uwekezaji wa Bandari. Uwekezaji hufanywa na muwekezaji yeyote awe Mwarabu, Mswahili ama Mbantu. Pia kiasili kama ulikuwa unamaanisha uhusiano wa Mheshimiwa Rais na waarabu. Basi jua waarabu hao ni Waomani. Ambao ni waibadhi katika nyanja ya kidini. Si waarabu wa Dubai ambao kwa wingi wao ni wasunni. Mkataba haukutolewa kwa Waomani ambao ndio asili ya undugu wao. Si Wadubai. Waarabu wa Emirati wana utamaduni tofauti kabisa na Waomani. Hivyo hoja yako kuwa dhaifu mno.

Hoja namba nane naweza kuziita chuki binafsi dhidi ya Wazanzibari. Walikuwepo Hai Wazanzibari wenye asili ya kiarabu ila walikuwa na fikra na itikadi za kijamaa. Ambazo kimsingi zilitofautiana pakubwa na fikra za waarabu wa wakati huo. Ndio waliopeleka mapinduzi pale Zanzibar kwa mshikamano wao. Hivyo basi Mheshimiwa Rais hahusiki nazo kabisa tuhuma ulizompa kuwa na mafungamano na Arab Setller worldview.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Hello,

Asante kuandika kwa kirefu. Nitakujibu kwa mtindo wa point counter point.

Umeandika: Hoja namba 3 ni Fallacy. Ni kweli kuwa zilikuwepo jamii za kibantu na jamii zisizo za kibantu nchini Tanganyika. Lakini hakuna ushahidi wa kimantiki wa moja kwa moja kuwa jamii zenye asili ya kilowezi zilizama katika kufuata unyayo wa makabila mengine ambao ni wenyeji.

Hii hudhihirishwa wazi na uwepo wa jamii nyingi nchini zenye kufuata mila na tamaduni tofauti tofauti mbali na jamii nyingine. Uwepo wa umoja na mshikamano haimaanishi kuwa jamii za wamasai zifate jamii za wasukuma. Au jamii za waswahili zifuate jamii za wabantu. Jamii hizi hujumuika kijiografia. Si kitamaduni wala kiitikadi asilia.

Najibu: Hoja yangu ni kwamba, chini ya dola ambayo "utammbuliko wa kitaifa" (national identity") ni suala la kisheria (de-jure matter) badala ya kuwa suala la kimazoea (de-facto matter).

Hivyo, hata wasiofuata nyanyo za wazawa bado wanalazimika kufuata tunu za kitaifa zilizo kwenye Katiba na sheria za nchi, ambazo kwa sehemu kubwa ni tunu za wazawa. Nimeongelea dhana ya "overlapping consensus" kana dhana muhiu katika kutawala Taifa ambalo linayo makabila na mbari nyingi. Google na utaelewa zaidi.


Ummeandika: Hoja namba 5 pia si kweli. Hakuna ushahidi wa moja kwa moja kuwa Zanzibar ina watu asili wa kibantu. Wabantu nao walihama toka magharibi mwa Afrika kuja Mashariki mwetu.

Nikupe mfano, Historia inaonyesha huenda Zanzibar ikawa imepokea walowezi hata miaka elfu mbili nyuma. Wabantu nao walihamia kama walivyohamia waarabu na wasomali. Zanzibar ilikuwa na wenyeji wake. Wabantu kwa pale Zanzibar si wakaazi halisi bali nayo ni jamii iliyolowea na kuchangamanyika humo.

Najibu: Hoja yangu ni kuhusu "the right of first occupancy" kati ya Wabantu na Waarabu. Wabantu waliwatangulia Waarabu.

Umeandika; Hoja namba 6 nayo si kweli. Hakuna utamaduni wa pamoja kati ya Zanzibar na Tanganyika. Zanzibar kwa wingi wao ni waislamu. Hubebwa na utamaduni mwingi wa Uislamu na uchache mno wa dini za kitamaduni. Tofauti na Tanganyika ambapo utamaduni wake umejengwa kwa wingi katika misingi ya utamaduni wa kikabila na utaratibu wa wakoloni. Kama uliisoma sheria vizuri utagundua Gavana wa Tanganyika alizikubali tamaduni zote zile ambazo hazikuwa A Repugnant to justice and morality according to the British Views. Hivyo basi hakuna utamaduni mpya ulioundwa na waasisi wenye kubeba mema baina ya pande zote mbili.

Najibu: Huelewi maana ya neno "utamaduni." Kwa ufupi, utamaduni unayo mambo matatu makuu. Kuna "cognitive/existential beliefs," "evaluative/normative beliefs," na "affective/axiological beliefs." Katiba ya Tanzania na Katiba ya Zanzibar ni ushahidi kuhusu "overlapping consensus" iliyopo kati ya pande hizi mbili. Naongelea imani, tunu za kibinadamu na kanuni za kimaadili. Jisomee zaidi.

Umeandika: Hoja namba saba nayo pia ni Fallacy. Kuzaliwa katika mapokeo ya kimabadiliko hakukufanyi kutokuwa na mtazamo tofauti.

Najibu: Rejea maelezo yangu katika hoja ya nane. Your worldview is your interpretive framework. What it shows you is what you see. Unless you unlearn it you will never be able to see a different world. But your worldview, being a learned matter, it is not a part of your essential nature. So, essentially speaking, when we criticize your worldview we have not criticized you. Period.

Umeandika; Hoja kuu ni uwekezaji wa Bandari. Uwekezaji hufanywa na muwekezaji yeyote awe Mwarabu, Mswahili ama Mbantu. Pia kiasili kama ulikuwa unamaanisha uhusiano wa Mheshimiwa Rais na waarabu. Basi jua waarabu hao ni Waomani. Ambao ni waibadhi katika nyanja ya kidini. Si waarabu wa Dubai ambao kwa wingi wao ni wasunni. Mkataba haukutolewa kwa Waomani ambao ndio asili ya undugu wao. Si Wadubai. Waarabu wa Emirati wana utamaduni tofauti kabisa na Waomani. Hivyo hoja yako kuwa dhaifu mno.

Najibu; Waarabu ni waarabu bila kujali kama wanatoka Ommani au Dubai. And the only way to explain how here on earth some one can draft an onerous provision which asserts a right to eternal ownership of foreign land, is to invoke "settler colonialism ideology." Hakuna option nyingine. I stand to be corrected.

Umeandika: Hoja namba nane naweza kuziita chuki binafsi dhidi ya Wazanzibari. Walikuwepo Hai Wazanzibari wenye asili ya kiarabu ila walikuwa na fikra na itikadi za kijamaa. Ambazo kimsingi zilitofautiana pakubwa na fikra za waarabu wa wakati huo. Ndio waliopeleka mapinduzi pale Zanzibar kwa mshikamano wao. Hivyo basi Mheshimiwa Rais hahusiki nazo kabisa tuhuma ulizompa kuwa na mafungamano na Arab Setller worldview.

Najibu; Tunautammbua mti kwa matunda yake. Baada ya kuonyeshwa uwepo wa vifungu vya mkataba vinavyotafuta kuanzisha "ukoloni wa walowezi" amechukua hatua gani? Kama anaukataa "ukoloni wa walowezi" angecchukua hatua ya kuhariri mkataba ule. Hajafanya hivyo. Ukimya wake unaaanisha nini? Hitimisho langu ni kwamba huenda anaunga mkono "ukoloni wa walowezi" . Niahii maana yake ni kwamba huenda ni mwathirika wa "settler colonial ideology." Ni juu yake kuthibitisha kwa vitendo kwamba ukweli sio huu.

Karibu tena.
 

Dhana ya kuwepo kwa settler colonial view kwa Mheshimiwa Rais ni hoja dhaifu mno eti kwa sababu ya kukaa kwake kimya. Unaleta hoja za kitoto.
Rais aliunda tume ya majadiliano ambayo iliundwa na wanasheria ambao wametumika kwenye meza ya majadiliano kwa maslahi ya Taifa. Ulichokipinga wewe dhidi ya Serikali ni jambo zuri. Ni hoja lakini hata upande wa serikali katika kuunda mkataba nao wanazo hoja vilevile. Mwenye kuamua uhalali wa mkataba ni Mahakama pekee.
Unapoamua kuunda hoja kupitia ad hominem basi hoja yako tunaiita dhaifu na isiyo na msingi zaidi ya itikadi. Unatengeneza Argument from the ignorance.

Suala la mbantu ni native kwa kuwa ni first settler hilo ningetamani nikujibu lakini tutakapo unda mjadala mwingine tutajadili. Tusitoke nje ya lengo la hoja yangu ya msingi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Well done my dear patriotics a excellent piece of work thank you so much for this commendable thinking and analytical submission. 🙏🙏🙏
 

Hello!

Umemandika: Dhana ya kuwepo kwa settler colonial view kwa Mheshimiwa Rais ni hoja dhaifu mno eti kwa sababu ya kukaa kwake kimya. Unaleta hoja za kitoto.Rais aliunda tume ya majadiliano ambayo iliundwa na wanasheria ambao wametumika kwenye meza ya majadiliano kwa maslahi ya Taifa. Ulichokipinga wewe dhidi ya Serikali ni jambo zuri. Ni hoja lakini hata upande wa serikali katika kuunda mkataba nao wanazo hoja vilevile.

Najibu: Kuwepo kwa settler colonial view kichwani mwa Mheshimiwa Rais, au ndani ya mtu yeyote baki, sio hoja dhaifu. Na sijaibua hoja hii kwa sababu ya kukaa kwake kimya. Kuna matendo yake ya nyuma yanatilia uzito hoja hii. Sakata la Loliondo ambako Wamasai wamehamishwa limetekelezwa chini ya usimammizi wake. Sababu pekee ya kueleza kilichotokea ni "settler colonial ideology." Kama unayo sababu nyingine naisubiri.

Ummeandika: Mwenye kuamua uhalali wa mkataba ni Mahakama pekee.

Najibu: Mwenye kuamua uhalali wa mkataba sio Mahakama pekee. Huwa kuna mapatani nje ya mahakama. Mantiki yake huwa nini? Ni watu tofauti na mamlaka za kimahakama baada ya kuuona ukweli. Vivyo hivyo, ukweli kuhusu mkataba huu unaweza kutambua nje ya mmahakama.

Umeandika: Unapoamua kuunda hoja kupitia ad hominem basi hoja yako tunaiita dhaifu na isiyo na msingi zaidi ya itikadi.

Najibu: Nionyeshe wapi nimemmshambulia mleta hoja badala ya kuishammbulia hoja. Pia kuikosoa itikadi ya mtu sio kumshambulia mtu. Maana watu huweza kubadilisha itikadi zao bila wao kubadilika.

Msimao wangu ni kwamba, msingi wa maudhui ya mkataba wa Bandari yni "settler colonial ideology." Kama tunakubaliana hivyo na tukarekebisha basi hakuna tatizo.

Tukikubaliana hivyo, lakini urekebishaji ukashindikana kuwadi wa hiyo ideololgy anakuwa amefahamika, lakini kuikosoa itikadi yake hiyo hakumaanishi kumshambulia yeye. Anayo nafasi ya kukwepa mashambulizi hayo kwa kujitenga na itikadi hiyo.


Ummeandika: Unatengeneza Argument from the ignorance.

Najibu: Nionyeshe wapi kuna Argument from the ignorance.

Uemandika: Suala la kwamba mbantu ni native kwa kuwa ni first settler hilo ningetamani nikujibu lakini tutakapo unda mjadala mwingine tutajadili. Tusitoke nje ya lengo la hoja yangu ya msingi.

Najibu: Kusanya ushahidi, ukikamilisha anzisha uzi uni-tag. Nitatinga ulingoni kaa kawaida!

Mwisho:

Tusisubiri mahakama kuturekebisha.
Tujirekebishe wenyewe leo.
Linalowezekana leo lisingoje kesho
 
A casual search on Google reveals a great deal of the content in this posting is plagiarized verbatim from a variety of sources. Very disappointed to discover this fact, as stealing other people's ideas is just as bad or even worse. An outright and gross breach of intellectual property rights supposedly in defense of "land rights", "sovereignty", and what not, is paradoxical and simply NOT acceptable.
 
Anna Tibaijuka,

Hayo ungepeleka mahakamani.

Wewe na sheria wapi na wapi?

Umechelewa jamvini karamu imeshaliwa.

Usijali, Karamagi ana mihela mingi, siyo vijisenti, atakurudishia tu mtaji wako.
Kwani huyu ni Tibaijuka?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…