Badala ya kampeni ya Katiba mpya,eti kampeni ya BAKI fulani? Vijana tunapoteza uelekeo

MAHANJU

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2014
Posts
5,252
Reaction score
8,003
Hua kila nikiwafikiria baadhi ya vijana wenzangu napata shida sana. Yaani mtu anataka kuamka na kuanza kupoteza muda kuzunguka na kampeni ya hovyo kabisa tena yenye uchonganishi ulio kinyume na katiba ya nchi, eti unaibuka from no where na kampeni ya "BAKI MAHANJU". Ni unafki na usaliti wa taifa kwa kijana huyu, ni mawazo mfu yaliyofilisika. Yaani unataka uungwe mkono kupiga kampeni ili katiba ivunjwe?

Lazima tuwe tu wakweli, vijana tunaelewa kua tuko nyuma sana katika nyanja zote pengine ni kwa sababu ya uwepo wa katiba isiyoenda na mahitaji ya wakati tulionao. Mambo hayaendi kwa sababu ya ulazima wa baadhi ya vifungu ambavyo haviendani na wakati, katiba ya sasa inalazimisha mambo yasiyoendana na wakati ulipo.

Kijana kama angeanza na kampeni ya kuamsha vijana wenzake na watanzania kwa ujumla ili kuidai katiba mpya na bora leo hii angeonekana kama shujaa wa taifa. Mtu anataka aonekane tu na watu flani ili kesho apate ulaji tu,ni usaliti wa ajabu sana huu.

Kwanini wasijitokeze watu wenye uchungu na taifa lao tukiachana wale viongozi wa vyama vya siasa wakajitokeza na kuanza na kampeni ya katiba mpya? Ni nani atakayezuia kampeni ya aina hiyo? Hivi kuna mwenye uwezo wa kutoka mbele ya macho ya wananchi akasema kua hatuna uhitaji wa KATIBA mpya hivi sasa?

Ni bora kuona aibu kuacha kudai mambo yasiyo na umsingi wowote tukajielekeza kwenye kampeni ya kuidai katiba mpya ambayo ndiyo mahitaji yetu ya sasa, mahitaji yetu ya sasa sio "BAKI MAHANJU". Mimi MAHANJU nitamaliza muda wa kazi zangu kwa mujibu wa katiba na atakuja mwingine wa kunirithi. Tuache unafki vijana!!
 
Na wewe unafanya juhudi gani zaidi ya kutapika nyongo hapa?? Vijana kama wewe wenye kupenda kuongea sana mkiwa chumbani tu mnatakiwa 'mpotezwe' kabisa! Ni vijana waoga kabisa ambao hawafai kwa manufaa ya taifa.
 
Back
Top Bottom