kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Muungano wa serikali mbili (muungano na Zan.) bila ya kuwepo kwa Tanganyika ni vigumu kukubalika hasa kwa watu wenye akili njema. Nadhani hata Nyerere hakumaanisha serikali mbili, haikuwa mwisho wake wa kufikiri na kutenda juu ya muungano huu bali alikuwa na mpango wa kuwa na muungano wa serikali moja pole pole kadri siku na fursa zilivyokuwa zinatokea. Kuwa na serikali tatu ni jambo ambalo halitekelezi sana kwa sababu ya tofauti ya ukubwa na udogo wa Tanganyika na Zanzibar hasa kwenye kuchangia gharama za muungano. Nyerere nadhani hata yeye alilijua hili. Kuunganisha TANU na ASP kuwa CCM ulikuwa mchakato wa kuelekea serikali moja. Nyerere kaondoka kabla ya ndoto yake ya serikali moja haijatimia, je viongozi mliomfuata Nyerer mna ajenda gani? kuirudisha ASP na TANU tena au kuifuta serikali ya Zanzibar kama ilivyo ya Tanganyika? Kama kufuta mama (ASP) kuliwezeka kwanini kufuta toto lake (SMZ) kushindikane? Inavyoonekana kufuta SMZ kuko mbali sana katika zama hizi ambazo matoto ya wale waarabu waliopinduliwa (CUF) wanashirikiana na matoto ya waliopindua (ASP/CCM). Ndoto ya CUF ni kujitenga kama sio kwa Zanzibar basi angalau kwa Pemba ili kuwaalika babu zao.
Kama selikali moja imeshindikana basi njia muafaka wa kuunusuru muungano na kuwaridhisha watanganyika pia ni kuendesha nchi kwa njia ya majimbo. majimbo yanayojiendesha yenyewe japo kwa asilimia 60 yatafanana na SMZ. Ni upuuzi mkubwa kuona Zanzibar yenye watu 1m iwe na idadi sawa ya wajumbe na Tanganyika yenye watu 44m kwenye tume ya madadiliko ya katiba kwa kisingizio kwamba Zan ni nchi kamili. Kama Zan ni nchi kamili kwanini watu wa Zan wahodhi ardhi kwenye nchi nyingine (Tanganyika) bila hata ya mashariti yoyote? Kama Zan ni nchi kamili kwanini isilipe gharama sawa na Tanganyika katika serikali ya Muungano? Kama Tanganyika itakuwa na majimbo yenye angalau watu milioni 5 kila jimbo basi kelele za muungano na Zanzibar zitapungua kama sio kwisha kabisa. Tuachane na serikali mbili au tatu zinazotuumiza vichwa.