Badhi ya wanyarwanda, hawana wadhifa wa kuitwa wanyarwanda au kuhudumiwa kama wenzao

Badhi ya wanyarwanda, hawana wadhifa wa kuitwa wanyarwanda au kuhudumiwa kama wenzao

Marie Antoinette

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2019
Posts
426
Reaction score
412
Minisitiri ushinzwe ibikorwa by’ubutabazi, Maj Gen (Rtd) Albert Murasira, yasobanuye ko impunzi zirindwi Ishami ry’Umuryango w’Abibumbye rishinzwe Impunzi (UNHCR) rishinja u Rwanda kwanga kwakira, n’ibindi bihugu byanze kuzakira bitewe n’imiziro zifite.

Waziri wa maafa, Meja Jeneral mstaafu Albert Murasira,ameeleza kuwa wakimbizi 7,waliotetewa na shirika la kimataifa la wakimbizi(UNHCR),linalotuhumu serikali ya Rwanda kuwanyima makazi, hata mataifa mengine yaliwanyima makazi,chanzo kikiwa hawana tena wadhifa wa kuitwa wanyarwanda.

Ikumbukwe,watu hao walituhumiwa kuhusika na mauwaji ya kimbali dhidi ya kabila la watutsi Rwanda,mwaka 1994. Baada ya kumaliza kifungo,walihamishiwa nchi moja ya Afrika ya kati,huku wakiangalia utaratibubwa kuwatafutia taifa linaloweza kuwapokea.
Rwanda,ambayo watu hao ni raia wake, kipindi hicho,ilidai haioni sababu ya wao kutorudi kwao,kwa sababu inawatambuwa kama wanyarwanda.
Mataifa mengine hayakuweza kuwapa hifadhi,kitu ambacho mpaka leo kinaigharimu UNHCR. Hakika hata wao hawakupenda kurudi kwao,kwa sababu pengine hawakuwa na imani na usalama wao. Leo hii sasa, serikali imeweka wazi kuwa haiwahitaji. Je,hii ni haki?

Ikumbukwe,familia za watu hao waliohusika na mauwaji,wengi wao hicho ndo huwa kipengele cha maendeleo kwao,kwa sababu kuna badhi ya sehemu hawakubaliki. Kama kweli dhambi ni ya mwenyewe,watoto wao na wake/waume zao, ambao hawakuhusika na mauaji,iweje leo ndo watwishwe mzigo?Je,mtu asie na wadhifa,nchini kwake,atakuwa na maisha gani?
Pamoja tukemee
 
Waache waendelee kuvuna mavuno waliyopanda, ni bahati tu kwao mpaka sasa wapo hai, vinginevyo hawatakiwi kuwa hai, wamedhulumu maisha ya maelfu ya watutsi wasio na hatia mwaka 1994.
 
Waache waendelee kuvuna mavuno waliyopanda, ni bahati tu kwao mpaka sasa wapo hai, vinginevyo hawatakiwi kuwa hai, wamedhulumu maisha ya maelfu ya watutsi wasio na hatia mwaka 1994.
Waliouawa wengi ni wahutu
 
Back
Top Bottom