SoC01 Badili mtazamo wako na ushinde katika uwezo wako

SoC01 Badili mtazamo wako na ushinde katika uwezo wako

Stories of Change - 2021 Competition

Petermalema

New Member
Joined
Jul 14, 2021
Posts
1
Reaction score
2
Habari wana JF

Jamii inategemea uwepo wako ili uweze kuleta mabadiliko chanya, lakini haiwezi kubadilika kama hauto weza kubadili mtazamo wako unao kufanya ushindwe kutambua na kutimiza yale unayo takiwa utimize.

Mtazamo una nguvu na una athiri sana katika kufanya maamuzi mbalimbali hasa pale tunapo kumbana na matatizo yanayo tukabili katika MAISHA yetu, vile vile pia hakuna ambaye anaweza kuja na kubadilisha Hali ya maisha uliyonayo, kwasababu wewe mwenyewe ndiyo chanzo kikubwa cha mabadiliko ya maisha yako unayo yahitaji na jamii yako.

Kuna msemo unasema "ukitaka mabadiliko lazima utembee katika njia ya mabadiliko"

Kila mwanadamu amepewa Uwezo (potential) ambao akiweza kuugundua na kuutumia ipasavyo unaweza ukamletea mabadiliko makubwa katika maisha yake na jamii husika.

Asilimia chache wameweza kugundua uwezo wao na kuutumia vizuri na kuleta mabadiliko pia hapo hapo wapo walio gundua Uwezo wao lakini wameshindwa namna ya kuutumia na kuuendeleza ili kuweza kuleta mafanikio makubwa, na hii ni kutokana na sababu mbalimbali.

Kundi kubwa lililo baki ni watu ambao wao wameshindwa kugundua uwezo wao na wengi wao wanaishi kwa kufuata Dunia inahitaji nini pasipo kuangalia wao ndiyo Wana hitaji kuwa na kitu gani au uwezo upi walionao ili waitawale Dunia.

Tumia dakika chache kutafakari na kutathimini uwezo ulionao (potential).

Je, umetambua unauwezo upi?

Wewe ni mtaalamu katika eneo lipi?

Namna gani unaweza kufanya uwezo wako ukaleta ushindani na kukufanya uwe tofauti?

Njia zipi za kukuza uwezo wako?

Ndiyo Maana wewe ni wa pekee na unapaswa kuthamini, uwezo ulio nao haufanani na uwezo alionao mwingine kwasababu ufikiriaji wetu tofauti, utatuzi wa matatizo na maamuzi pia ni tofauti, utendaji ni tofauti. Mfano, "juma ana uwezo mkubwa wa kuimba", pia "John ana uwezo wakuimba" hawa wote Wana uwezo lakini uwasilishwaji wa uwezo wao au utendaji lazima utatofautiana.

Baada ya kujiuliza maswali mbalimbali unaweza kugundua kuwa wewe unauwezo mkubwa katika Mambo Fulani, mfano bisahara, uimbaji, uwandishi, uzungumzaji, ushauri, ubunifu, pamoja na uwezo mwingine.

Je, ukishatambua ufanye nini?

Fahamu kuwa hakuna mtu anaye weza kutambua uwezo ulio nao au ujuzi fulani pasipo wewe kuamua au kuruhusu ulimwengu wako wa ndani uweze kukubali kupeleka uwezo wako katika ulimwengu wa nje (sehemu ya utendaji), na hapa ndiyo tunakutana na vita vikuu 2 vinavyo msumbua binadamu na una hitaji kushinda hivyo vita, hivyo vita havihitaji utafute mchawi au utumie nguvu bali maadui wa vita hivyo ni:

1. Hofu ya akili, hii inakufanya usiweze kufanya maamuzi ya kuonesha uwezo wako inaweza kuwa unahofu kuwa watu watakuonaje, watakufikiriaje, au nani atakaye kusaidia. Ukweli ni kwamba hofu nyingi tunazo zitengeneza hazina ukweli wowote bali inatakiwa tuzipige vita ili kushinda na kuleta mabadiliko makubwa.

2. Kukata tamaa, epuka vita hii ili uweze kufikia sehemu husika. Tambua ya kwamba wewe ndiyo mwenye wajibu wakuweza kutimiza hilo ambalo unahitaji kutimiza, fahamu kuwa kukata tamaa siyo njia ya kukimbia tatizo bali ni kuongeza tatizo juu ya tatizo kubali kuwa katika maisha "kuna wakati utashinda na Kuna Wakati utahitaji kujifunza."

Kwanini ukate tamaa?
Hayo magumu ni njia ya kukufikisha Kama njia unayo pita nimbaya jaribu kubadili ili ufikie pale una stahili (lengo). Bali usiache kujaribu kuonesha Uwezo wako.

AMUA KUONESHA UWEZO WAKO
Je, baada ya kuonesha Uwezo wako uliambiwa nini?

Ulichukua hatua gani?

Malanyingine kunawakati Sasa unaamua upigane vita ili kuonesha Uwezo wako, lakini baada ya kuonesha huo uwezo ulionao (potential) mapokezi huwa mazuri lakini majibu huwa Katika makundi tofauti kuna wale wanao kubaliwa juu ya uwezo wao na Kuna wale wanao kataliwa juu ya uwezowao, wakati huo wao Wana amini kuwa bado wana uwezo mkubwa wa kuweza kufanya hilo jambo na wengine kati yao hukata tamaa na kuona kuwa wamekataliwa, hivyo wanashindwa namna na kuendelea kujituma Katika kile walicho nacho na wengi wao imani na hamasa huanza kupungua kabisaa.

Je, ufanye nini baada ya kukataliwa?

Jambo la msingi ni kuendelea kuamini ya kuwa wewe bado unauwezo kukataliwa siyo mwisho wa maisha yako, siyo mwisho wa Kipaji chako.

Tumia neno kukataliwa kama sehemu ya kukufanya wewe uongeze juhudi zaidi, ubunifu, pamoja na maarifa zaidi juu ya uwezo ulionao kuhakikisha ya kwamba hauwezi kukata tamaa. Hii itakufanya uweze kufika pale unahitaji kufika na kuwa vile unataka.

Anza kujiamini sasa kuwa bado unanafasi ya kuwa vile unataka kuwa, bado haujachelewa.

PIGANIA UWEZO WAKO
Baada ya kutambua kuwa unauwezo katika eneo fulani hapa utakutana pia na maisha ya aina mbili ambayo yana hitaji uwe mwangalifu katik kukuza uwezo (potential) wako, yaaani Kuna maisha ya kawaida na maisha yasiyo ya kawaida.

Je, kwanini watu wengi wanaishia maisha ya kawaida lakini Wana uwezo (potential) hii ni kwasababu maisha ya kawaida ni maisha ambayo mtu ameamua kuishi pasipo kufanya juhudui zozote au ubunifu zaidi juu ya uwezo alionao ili kuhakikisha anaenda katika hali ya juu.

Hapa ndipo watu wengi walio na vipaji mbalimbali wanashindwa kuwa na upekee kwa sababu ya kuridhika na kujiona kuwa wao wanaweza kwasababu Wana uwezo pasipo kujua kuwa jinsi siku zinavyo zidi kwenda ndivyo uwezo hufa kutokana na kukosa hali ya kujituma au mwendelezo.

Hivyo basi maisha yasiyo ya kawaida ni maisha ambayo watu wachache wame amua kuishi hayo maisha kwa kuhakikisha ya kuwa uwezo wao (potential) unahitji ubunifu zaidi, kujituma, kuto kata tamaa, kujifunza kila siku.

Ndiyo Mana utakuta ukifika sehemu utaambiwa fulani ni Bora zaidi kuliko Fulani siyo kwamba yeye ila ubora upo katika kazi zake anazo zifanya. ili jamii yoyote iweze kukubali nilazima kwanza itambue na ione thamani ya huduma uliyo nayo.

mfano wa wafanya bishara waliopo katika Mtaa moja na wanafanya biashara ya aina moja, lazima Kuna mmoja ila kitakacho watofautisha ni ubunifu walio nao katika biashara moja.

TAFUTA HAMASA YAKO
mala nyingi binadamu tunafanya vitu mbalimbali kulingana na hamasa inavyo tupeleka juu ya mambo hayo. Siri moja ambayo itakufanya ugundue uwezo (potential) ni kuangalia jambo lipi unapenda kulifanya, linakupa furaha zaidi, au Muda mwingi umekuwa na shauku ya kulifanya hilo jambo, tambua kwamba hutakiwi kwenda mbali saaana.

Kwasababu hapo ndipo uwezo wako (potential) ulipo chunguza kwa makini na utagundua kuwa hakika hilo jambo lipo na kinacho kwamisha ni kuto jiamini Kama kweli wewe una uwezo huo. Nataka kukwambia kuwa amua kutengeneza mazingira ya kujiamini ili uweze kufanya kile unacho weza na kuweza kuleta mabadiliko.

Hivyo hamasa uliyo nayo itakusaidia kutambua Jambo lipi una uwezo nalo zaidi kuliko mengine na uchukue maamuzi thabiti.

EPUKA MATATIZO YA KUSHINDWA KUTUMIA UWEZO WAKO (POTENTIAL)
Je, umewahi kujiuliza nini kitatokea endapo utashindwa kutumia Uwezo ulio nao?

1. Utashindwa kufanya maamuzi sahihi juu ya maisha yako. Malanyingi Mtu asiye weza kugundua na kuendeleza Uwezo wake huwa Katika hatari ya kuhangaika katika kufanya maamuzi sahihi kipi anatakiwa afanye na kipi hatakiwi kufanya (kukosa mwelekeo sahihi was maisha yake)

2. Kuwa mtumwa, kwa kawaida kukosa kutambua Uwezo wako(potential) kutakufanya uwe mtumwa na utatumika Katika kuendeleza kusudi la mtu mwingine pasipo kushughulikia lakwako na kujikuta unapoteza muda mwingi kuishi maisha ya Watu wengine.

Fahamu kwamba kiwango cha elimu siyo sababu ya wewe kushindwa kugundua na kuendeleza Uwezo ulio nao, ndiyo maana unaweza kusoma Sana na ukashindwa kutambua Uwezo (potential) ulionao, usishangae mtu kasoma kufanya kazi Fulani lakini unamkuta sehemu nyingine kabisaa na aliyo somea.

Amini ya kwamba unaweza kubadilisha hali ulinayo na ukabdilisha jamii yako kutokana na huo uwezo(potential) ulio nao.

Je, nini kifanyike?

1. Kutengeneza mazingira mazuri, mazingira yanaweza kusaidia kutambua Uwezo (potential) aliyo nayo mtu katika mazingira husika. Mfano mazingira ya nyumbani haya yanaweza kutengenezwa na wazazi katika kugundua na kuendeleza Uwezo wa mtoto katika namna mbalimbali ili kumuwezesha kukua katika hali ya kutambua Uwezo wake. Hivyo basi mazingira lazima yawe rafiki katika kufanikisha hilo.

2. Serikali lazima ifanye maboresho ya elimu katika kutengeneza waalimu wanao weza au walio bobea Katika kugundua Uwezo wa mtoto Katika sehemu tofauti tofauti na kusaidia kuendeleza Uwezo wao. Mfano mtoto asipimwe Katika kigezo Cha ufaulu tu bali pia Katika shughli nyingine nje ya darasa.

3 .Serikali lazima pia iangalie watoto waliopo mtaani ambao wamekosa kupata elimu kwa sababu tofauti tofauti lakini Wana Uwezo (potential) katika sehemu Fulani ambao unaweza kusaidia katika kuleta mabadiliko katika jamii na kuwa endeleza juu ya Uwezo wao.

4. Kutambua haki za makundii tofauti tofauti, hasa wanawake katika
  • Kumiliki Mali
  • Haki ya kuishi
  • Haki ya kuongoza
  • Haki ya Elimu
  • Haki ya kufanya maamzi ndani ya familia na katika masuala mbalimbali ya kijamii
  • Haki ya kulinda na kutetea nchi
Mtoto wa kike anauwezo mkubwa sana wa kiakili hivyo apewe nafasi Kama mtoto wa kiume ili kujenga jamii endelevu.

Jambo kubwa la kufanya
  • Mpe mazingira mazuri ya kusomea
  • Mwamini
  • Mtie moyo
  • Epuka unyanyasaji wa kijinsia
  • Mpe nafasi aoneshe Uwezo wake
UNAWEZAJE KUTUMIA UWEZO WAKO KATIKA KUJENGA JAMII
Kwa kawaida huwezi kuibadilisha jamii yako kama wewe hautaki mabadiliko. Hivyo kutambua Uwezo wako kutakufanya uweze kubadili hali yako kwasababu hautaweza kufikiri juu ya kutumika katika kuendelaza kusudi la mtu mwingine, hivyo basi unaweza kutumia katika kutatua matatizo mbalimbali yaliyomo Katika jamii yako hasa Yale ambayo kunawakati yalikosa majibu fulani katika jamii lakini umeweza kutatua.

JAMBO LA MSINGI
Kwanini mtazamo ni muhimu Katika kuonesha uwezo wako (potential)
Amua kutawala mtazamo wako
Wengi wanaoshindwa na kuamua kukata tamaa kabisa ni watu ambao mara nyingi wameshindwa kutawala mitazamo yao.

Kushindwa kutawala mtazamo wako
Kiuhalisia unaposhindwa kutawala mtazamo wako na ukajikuta una mtazamo hasi, elewa kabisa maisha yako yatakuwa magumu sana katika kila eneo Fulani na hauto weza kuonesha like ulicho nacho.

Kwa hiyo unaona kabisa mtazamo una nguvu kubwa sana ya kubadili maisha yako, inategemea tu wewe unautumiaje huo mtazamo wako ulionao. Matatizo mengi huanza na mitazamo mibovu. Kwa jinsi unavyokuwa na mtazamo mbovu ndivyo maisha yako yanazidi kuwa mabovu pia, lakini kuwa na mtazamo mzuri kwa sababu una siri kubwa ya kugeuza chochote kuwa kile unacho taka.

Peter Julius Malema
 
Upvote 3
Back
Top Bottom