Phestus Million
New Member
- Nov 2, 2021
- 1
- 3
Tanzania nchi ya amani, taifa lenye watu wapendwa amani, ukarimu, taifa lililoundwa na Mungu Kwa mapenzi yake, uoto wa asili, wanyama wa mwituni na wafugwao, misitu mikubwa ya asili, mito isiyokauka, madini na Kila chenye thamani machoni pa Mungu na mwanadamu, mbona wajiharibu mwenyewe?
Taifa Tanzania umeundwa Kwa vyama vya siasa mbalimbali kwa kutumia katiba, fanya yafuatayo nawe utafanikiwa na kuheshimika duniani kote.
Kumbuka kutenganisha Serikalini (utumishi wa umma ) na vyama vya siasa kiutendaji, maana yangu ni kwamba Serikalini na utumishi wa umma iunde mfumo wa uongozi utakaosimamia uendeshaji wa sera zote za kuijenga Tanzania. Chama chochote Cha siasa kitakapoingia madarakani, kinapaswa kufuata mungozo na dira iliyowekwa na Serikali na utumishi wa umma katika kuhakikisha Tanzania unaendelea mbele daima, mwiko kurudi nyuma. Chama Cha siasa kitakapoingia madarakani kitawakilisha mpango kazi wake Kwa Serikali na kujadiliwa na jopo la wataalum wa Kila sekta wasiogemea upande wowote wa siasa ili kuona manufaa Kwa ukuaji wa Tanzania. Fanya hivyo hivyo Kwa vyombo vyote vya usalama, jeshi la polisi, usalama wa taifa na jeshi la wananchi wa Tanzania.
Rasilimali za Tanzania zisaidie Tanzania kukua, usitegemee mikopo ya nje ya nchi, hii ni cancer iuayo taratibu hatimaye utaharibikiwa Tanzania nikupendae.
Tanzania tega sikio jambo hili ni uzima wako, usipende kupokea vilivyotayari tu, hujua walitumia gharama Gani kuvipata, tengeneza vya kwako mwenyewe.
Ikiwa huna wa taalamu wa kutosha Kwa Kila secta, ingia gharama za kuwasomesha watanzania wapate maarifa Kutoka Kwa Kila nchi yenye mafanikio makubwa Kwa Kila sekta hitajika, fanya hivyo Kila mwaka kulingana uhitaji wa sekta husika.
Sikia Tanzania nikupendae, kuhusu uhitaji wa mitambo na wataalamu unda kampuni yenye usimamizi wa Serikali kwenye sekta husika, ingia ubia na kampuni zisizo na usimamizi wa Serikali za nchi hizo, Kwa mkataba wenye ukomo, na hakikisha mwisho wa ukomo wa mkataba ume adapt technolojia Yao yote pamoja na utaalamu wa kuunda hiyo mitambo hitajika hapa mchini.
Tanzania nikupendae amka usingizi wa mauti uliolala, kweli unaruhusu madini kuchimbwa kwenye ardhi Yako ilihali una uwezo wa kuyachimba mwenyewe na kuyahifadhi katika benki yako ya taifa na mengine ukauza kwenye soko la dunia? Kumbuka wewe huna ruhusa ya kwenda nchini kwao na kuwekeza kwenye nchi zao.
Tanzania ipende maliasili zako, mbuga, wanyama wa porini. Siku utaamka usingizini na wao Wana mbuga za wanyama, utalii utahamia kwao.
Tanzania ifufue sekta ya kilimo, tengeneza mbegu asilia, mbole na viuatilifu pia wataalamu wa kutosha Kila eneo. Hakikisha unakuwa na chakula Cha kutosha ili wewe uongezeki idadi na kuwa na Afya njema, baada ya hapo Anza kuzalisha chakula Cha kuwauzia majirani zako na wale waishio kwenye barafu na jangwa.
Tanzania nikupendae, unao wazalishaji wa kutosha, kama huwajui nikutakie, vijana wanaomaliza shule ya msingi, kidato Cha nne na Cha sita wale ambao hawako tayari kuendelea na masomo, waingizwe kwenye sekta za serikali za uzalishaji, kama kilimo, viwanda, wafanye kazi za ujuzi, zenye kuizalishia nchi, Kwa mikataba mifupi mifupi, muda wa kurudi shuleni ukifika warudi shuleni, wasiruhusiwe kukaa nyumbani bila kazi na hili lingeondoa wimbi la vijana wavuta bangi, walevi, wezi, watumiaji wa madawa ya kulevya, wavivu n.k
Tanzania nikupendae tumia wataalamu katika JKT kujenga majengo ya watumishi wa umma, hospitali, shule n.k ili kupunguza gharama za ujenzi.
Tanzania nchi yangu watumie wafungwa ulionao katika magereza mbalimbali nchini katika kuizalishia nchi Kwenye sekta mbalimbali kulingana na ujuzi walionao, wasiokuwa na ujuzi wowote wafundishwe, ili siku wakitoka kutumikia vifungo vyao magerezani watoke wakiwa na ujuzi na kuajiriwa kwenye sekta za umma. Wafungwa wenye kiu ya kusoma kuwe na vyuo vya magereza wasome wakiwa gerezani.
Tanzania nchi yangu, tumia wataalamu wa ndani kutengeneza barabara zote zinazounganisha mikoa Kwa kiwango Cha kimataifa, na zile za vijijini pia maana mali ghafi zote hupatikan hapa nchini, rasilimali watu wapo na mitambo hitajika waweza kununua Kwa gharama nafuu, tumia jeshi la JKT tu, Kila mkoa kuwe na Head Office za kusimamia na kujenga barabara zote za mkoa Kwa kiwango hitajika.
Tanzania nchi nipende na Mimi mtanzania tafadhali, hakikisha bidhaa zinazozalishwa hapa nchini ziwe halisi, tumia vihifadhio halisi kama asali n.k wekeza zaidi katika matumizi ya tiba lishe na mimea yenye virutubisho vinavyosaidia kukinga Afya ya mwili kuliko kusubiria mpaka mtu anaugua. Ambapo jambo hili ili lifanikiwe vizuri kuwepo na kipindi Cha lishe ya mimea asili kwenye runinga ya taifa, mtaalam huo uandaliwe na kupitiwa na mamlaka za tiba na dawa. Ikiwa Kuna mtu atagundua mmea wenye dawa basi, mamlaka husika zikue hatua ya kufanyia utafiti hatimaye lengo la kupata solution ya magonjwa sugu itimie.
Sekta ya uchakataji Mali ghafi iundwe, zao la pamba na mkonge linaweza kutusaidia Kuanza viwanda vya nguo zote, magunia, vifungashio vyote, zikatengenezwa hapa nchini.
Wekeza kuzalisha umeme wa kutosha viwandani ili uzalishalishaji bidhaa uwe mkubwa na Bei zipungue,
Tanzania nchi yangu Anza kuzalisha chuma uondokane na wimbi la mfumuko wa Bei wa bidhaa za chuma kutoka nje.
Tanzania nchi yangu unauwezo wa kuwaunganishia umeme watanzania wote bila malipo Kisha wakalipia matumizi ya Kila siku, kuliko kuweka gharama kubwa za kuunganishwa umeme, hatima yake watu wachache tu ndio wanaweza kuhimili gharama hizo.
Tanzania nchi yangu chukua ufahamu huu, wale wanaojitokeza katika jamii Kwa kugundua vitu mbalimbali hata kama ni vitu hatarishi, msiwachukue na kuwafunga magereza, Bali wapelekeni kwenye vyuo maalumu waendeleze ujuzi wao, hata wale wanaojaribu kudukua mifumo msiwafunge magereza Bali waendeleze I.
Tanzania Jenga mahusiano mazuri baina ya Serikali, vyama vya siasa, vyombo vya ulinzi na usalama na wananchi. Uwajibikaji, upendo, umoja, Amani na haki.
Ondoa siasa za chuki, acha kuwalinda wanaovunja Sheria na katiba ya nchi, acha Kila mtenda uovu awajibishwe sawasawa na Sheria za nchi na katiba.
Hakikisha mihimili ya Serikali inajisimamia yenyewe bila kuingiliana, Serikali, Bunge na mahakama.
PLEASE, PLEASE, PLEASE TANZANIA WEWE, BADILI TANZANIA POLICE FORCE KUWA TANZANIA POLICE SERVICE.
Tanzania nikupendae fufua sekta ya viwanda, hakikisha wananchi wako wananunua bidhaa zote Kwa Bei nafuu, safuji, mondo, mabati, petroli, diseli n.k.
Tanzania wewe, BANDARI BANDARI BANDARI tafadhali badilisha kabisa mfumo wa BANDARI kuanzia watendaji, mifumo, mitambo na ongeza ukubwa wa badhari.
Hakikisha urasimu wa kuchelewesha wa upakuaji na upakiaji wa mizigo unaondoka. Bidhaa zinapanda Bei kwasababu ya kuongezeka Kwa storage fee.
JENGA BANDARI YA BAGAMOYO HARAKA IWEZEKANAVYO. Hakikisha Tanzania inakuwa na TRANS-INDIAN ATLANTIC OCEAN PORT. Meli zote kubwa duniani ziwe na uwezo wa kuja tanzania kupakua mizigo ili meli ndogo ndogo zije kwako Tanzania kuchukua mizigo.
Tumia mfumo wa kuunga kampuni itakayosimamiwa na Serikali itakayoingia ubia na kampuni ya nchi zenye uwezo wa kuijenga hiyo BANDARI yenye viwango hivyo.
Hakikisha mkataba uwe wa asilimia hamsini Kwa Kila pande, na uwe na ukomo, na baada ya ukomo wa mkataba, uwe umejijenga kujiendesha na kujitawala katika raslimali watu, wataalamu, mifumo na mitambo.
HITIMISHO
Unapochaguliwa kuwa kiongozi Haina maana kuwa wengine hawawezi kuongeza zaidi Yako, Bali umepewa nafasi ya utumishi, tumika Kwa uaminifu, unganisha watu, cheo ni dhamana tu, cheo ni koti tu, ipo siku utalivua.
PLEASE TANZANIA OPEN YOUR INTERNAL EYES.
Tanzania All we Are One!! In God we Trust. Amen 🙏.

Upvote
2