Badilisha mwenendo

prince22

Senior Member
Joined
May 8, 2015
Posts
188
Reaction score
217
Mwezi June niliwahi kusimulia kisa hapa

Msaada juu ya PEP


Wiki saba zimepita sasa toka nilipopata exposure na pia ni wiki tatu Sasa tangu nimalize dose ya PEP, nimeenda kupima tena nimeambiwa sina maambukizi nirudi baada ya miezi mitatu

TUJIFUNZE
sometimes unaweza ukaona kama maigizo mpaka yakukute na usiombe yakakuta, wengi hupenda kuja kufanya mizaha hapa jukwaani. Usiombe yakakuta maana hata kama ulikuwa mbabe saana au mjanja sana basi lazima uwe mdogo kama piritoni.

Ninachotaka ujufunze ni kuzishinda tamaa za kimwili na kuachana na uzinzi kwani hakuna bingwa wa ngono wala kombe utakalopewa.

Epuka kupima kwa macho maana huyo niliyemsimulia hapo juu ukimwona huwezi mdhania kwani alivyonielekeza mnene na makalio ya haja.

Si kazi rahisi hata kidogo kumaliza dose ya PEP kwani zinalevya mno na kuchosha. Unakuwa kama mgonjwa Mgonjwa, kichwa kuuma, kutapika na kuharisha. Ukilala usiku ndoto za kutisha, pia hata ubongo haufanyi kazi ipasavyo.

Naomba kupitia mm ujifunze na ubadili mwenendo
 
Mimi nilibadili mwenendo toka siku nlipokoswa kugongwa na treni tena wife alikuwa na kibendi,nilirudi home nikamuangalia mama watoto nikasema hizi mambo sirudii tena



Ule mchepuko ulitaka kuniua
 
Mimi nilibadili mwenendo toka siku nlipokoswa kugongwa na treni tena wife alikuwa na kibendi,nilirudi home nikamuangalia mama watoto nikasema hizi mambo sirudii tena



Ule mchepuko ulitaka kuniua
Hongera saaana mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…