Bado sijaona wa kumfunga Uhispania hadi sasa

Jackwillpower

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2017
Posts
2,467
Reaction score
3,687
Hadi mechi za leo, sijaona cha Brazil au Uingereza mwenye kiungo cha kupambana na Uhispania ya Luis Enrique Martinez.

Mechi dhidi ya Costa Rica alipiga pasi 1045, sijui kama kuna timu imepiga pasi kama hizi kwa miaka 10. Huyu Brazil aliyecheza na Serbia akamfunga 2-0 na tukaambiwa limepigwa samba, ni pasi 500+ tu ndiyo zilipigwa huku Serbia akipiga pasi 400+.

Kwenye mpira wa kisasa kitu cha kwanza kabisa kabla ya yote kamata kiungo. Hii ndiyo falsafa ya Pep na wafuasi wake kina Arteta, Luis Enrique n.k. Spain ya Enrique ina watu hawa Rodri Bosquet Pedri na Gavi.

Picha linaanza Rodri anawekwa CB kivuli, ndani ya uwanja anakuwa kiungo, lengo kuu nikufanya 'overload'. Kinachotokea kunakuwa na umbo la mstatili la Rodri Bosquet, juu yao kuna Pedri na Gavi.

Pale City Pep Guardiola anamtumia Cancelo kama beki lakini ndani ni kiungo, sawa na Mikel Arteta msimu huu anamtumia Zinchenko kama LB, lakini ndani anacheza kama kiungo.

Kwa nilichoshuhudia anachofanya Luis Enrique Martinez (Lucho) timu nyingi zitateseka kama alivyoteseka Costa Rica.

Timu nyingi bado zinaamini sana katika majina na siyo mifumo, Uhispania kuna mfumo unaokufanya uwe 'overloaded'.

Kwa umbo la mstatili ya Rodri Bosquet Pedri na Gavi wewe njoo na viungo wako Declan Rice na Jude Bellingham 'overrated', kuna aibu Ulaya inaenda kutokea.

Jumapili Ujerumani anaenda kufangashiwa virago na Uhispania. Fikiria Uingereza na makelele yao kwa viungo wao Rice Mount na Bellingham wanateseka kwa viungo wa USA Weston Mackenie, Yunus Musah na Tyre Adams.

Habari gani wakikutana na mstatili wa Uhispania? Brazil mnayoisifia ni wazuri kwenye 'flanks'. Kwa 'combination', Tite anazoziamini za Casemiro Fred, Casemiro Paqueta, hizi 'combination' hasa ya Fred na Casemiro imekuwa amefunikwa mara kibao hapo EPL na timu kama Brighton, Southmpton n.k.

Habari gani wakikutana na ile umbo la mstatili wa Lucho? Unapomuona Rodri na Busquet, hawa wote huwezi kuwakandamiza siyo wapotezaji wa pasi, halafu juu kidogo unawekewa Pedri na Gavi, hawa watoto wawili wanajua hadi wanakera.


Uhispania kwa nilivyomuona, ili uweze kumpiga tumia 'counter attack' ukiwa na winga zenye kasi na maamuzi ya haraka, ila suala la kubishana nao eneo la kiungo sahau.
 
Ghana wana mpira mbaya sana muulize Christiano
 

Utakuja kuwakataa hao watoto soon
 
Punguza mbwembwe World Cup sio game moja una judge tulia kabisaaa, msiwe na mdomo kama wa England

Sent from my LM-Q730 using JamiiForums mobile app
 
Sss
 
Aina ya uchezaji kama ule wa Spain na Barcelona pamoja na Manchester city umepitwa na wakati alishawahi kusema Mourinho wakati Barcelona ameshinda tatu kwake akaenda kufa nne Anfield na Manchester city kwa Madrid ni aina ya mpira unaofaa kwenye league tu ila sio kwenye mashindano kama UEFA champions league pamoja na world cup ni mpira usio na mbinu zaidi ya kushambulia tu wakifungwa wanashambulia wakifunga wanashambulia wakikutana na France wale Spain utawakataa
 
Angalia na opponent pia, Costa Rica hawana team ya kutisha ndomana Spain alitamba Sana, mfano mzuri angalia game ya England v Iran, England waliubonda Sana Ila Jana v U.S.A performance Yao ilishuka ni kutokana na opponent, sasa level ya Serbia siyo sawa na Costa Rica, ngoja Spain na Brazil wakutane tuone nani atamu outshine mwenzie..
 
Mkuu umetolea mfano wa Fred na Casemiro kupotezwa na Brighton unasahau kuwa hao viungo wa Spain uliowataja wote wako Barca na wameshindwa hata kuivisha team kwenda group stage ya UEFA tena waliteseka Sana Kwa viungo wa Bayern kina kimmich, Goretzka, Sabtzer Barca anafungwa nje ndani
 
Hiyo Spain iliyopigwa na Serbia national lig, Spain wapo vzr ila hawajakutana na wababe bado
 
nani kakudanganya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…