Ili swali nimeweka hapa naona wale wana ccm wanakwepa sana kujibu.
Wanajua Afghanistan ilikuwa maskini sababu ya urusi.
wanajua kwa kiduku ni sababu ya urusi.
Yugoslavia mpaka kuvunjika ni urusi.
Syria kuwa magofu ni urusi.
Hapa ni mifano michache.
Mi nachoomba kupewa majibu kuwa urusi ni msaada wa kitu gani hapa duniani.
Maana wamefikia kuchukua wafrika kwenda kuwapiganisha ukrain na mwisho wa siku hakuna cha kuwalipa wala kuwapa chochote na ndio wanaongoza uminyaji wa vyombo vya habari.
Kumbuka telegram ilitokea urusi sababu ya ukandamizaji wa habari.
Mbona telegram imefungwa Tanzania.Si inatokea urusi .
Urusi na China zitawezaje kuondoa umaskini wa nchi nyingine wakati zenyewe bado zina idadi kubwa ya wananchi maskini!
Mwanzoni mwa miaka ya 1990 Serikali ya Urusi ilifilisika mpaka kufikia hatua ya kuomba msaada toka Marekani na Ulaya. Masharti ya msaada ilikuwa ni lazima uhuru wa wananchi uheshimiwe. Urusi ikaridhia, na ndipo nchi mbalimbali zilizokuwa kwenye USSR zikajitoa. Marekani na nchi za Ulaya zikaipa msaada Urusi, na makampuni mengi ya Ulaya na America yakaenda kuwekeza Urusi ili kuokoa uchumi wa Urusi. Uchumi wa Urusi ukapaanza kukua kwa 7%.
China mpaka miaka ya mwanzoni mwa 1990 ilikuwa hoi bin taabani kiuchumi, chini ya sera zake za Ujamaa. Iaenda kuzililia nchi za Ulaya na America. Masharylti ikawa China iondokane na sera za ujamaa, ikaridhia. Kisha makampuni zaidi ya laki 5 ya Ametica na Ulaya yakaenda khwejeza China.uchumi wa China ukaanza kukua kwa 12%.
Fikiria mpaka leo hii, Marekani ina watu 349 milioni lakini ina uchumi wa dola trilioni 32.38 trillion, mkubwa zaidi ya 1.5 ya ule wa China ambao ni dola trilioni 20.85, nchi ambayo ina idadi ya watu 1.412 bilioni, zaidi ya ya mara 4 ya idadi ya Warekani. Katika uhalisia wa maendeleo ya watu, China inatakiwa iwe na uchumi angalao kufikia dola trilioni 120 ili kulingana na Marekani yenye idadi chini ya robo ya wachina.
China, kwa upande wa Serikali, inaweza kufanya makubwa, kwa sababu makusanyo yake ni makubwa, lakini kwenye maendeleo ya mtu mmoja mmoja, bado ina uchumi mdogo sana.
NI afadhali ya China kuliko Russia yenye ukubwa wa uchumi wa dola trilioni 2.66. Lakini ina idafi ya watu milioni 143. Ipo mbali sana kutoka nvhi duni kama Tanzania, lakini ipo chini sana ukilinganisha na mataifa mengine yaliyoendelea.