Bado unatumia dawa hii ya kusafishia kinywa?

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363



COLGATE TOTAL

Triclosan 0.3% w/w, Sodium Fluoride EP 0.32% w/w (1450ppm F)



TRICLOSAN ni kemikali inayotumiwa kama kiambata katika bidhaa nyingi ikiwa ni pamoja na sabuni, vipodozi, nguo, vyombo vya kupikia, samani na toi za watoto kwa lengo la kupunguza au kuzuia uvamizi wa bakteria. Tafiti za hivi karibuni kabisa zinaonyesha hata hivyo kuwa kemikali hii inaweza kuwa na madhara makubwa sana kwa binadamu.


Tafiti hizi zimeonyesha kuwa triclosan :


• Inaingilia na kuvuruga utendaji kazi wa mfumo wa tezi na hivyo kuathiri uwezo wa mwili kuzalisha na kutumia homoni mbalimbali.


• Ina uwezekano mkubwa wa kuchangia katika janga lililopo hivi sasa la kuibuka kwa bakteria wenye uwezo mkubwa wa kuhimili vijaua vijasumu (antibiotics) vinavyotumika sasa


• Ina uwezekano mkubwa wa kuathiri utendaji kazi wa mfumo wa kinga za mwili.


Wanasayansi wana hofu kubwa na kemikali zinazoathiri mfumo wa tezi kutokana na imani kuwa kemikali hizi zinaweza kuwa kichocheo kikubwa cha matatizo mbalimbali ya kiafya ikiwa ni pamoja na:


• Saratani za mfuko wa mayai na matiti kwa kina mama;


• Saratani za kibofu na korodani kwa wanaume;


• Watoto kuzaliwa njiti na wakiwa na uzito mdogo; na


• Mabinti kuvunja ungo wakiwa na umri mkubwa


Ni muhimu kujua kuwa unapotumia bidhaa yoyote yenye triclosan, kiasi fulani cha kemikali hiyo kitapenya kwenye ngozi au kinywani na kuzifikia seli zako za ndani ya mwili. Kwa mfano, utafiti uliofanywa mwaka 2008 nchini Marekani katika sampuli za mkojo, uliokuwa na lengo la kubaini kiwango cha kuathiriwa na triclosan kwa wananchi wa nchi hiyo, ulionyesha kuwa kiasi cha 75% ya wale waliofanyiwa utafiti walikuwa na kemikali hiyo katika miili yao.


Hivi sasa taasisi ya Chakula na Dawa la Marekani (FDA) linafanya mapitio upya ya hatua zilizopelekea taasisi hiyo ikaruhusu matumizi ya dawa ya meno inayoitwa COLGATE TOTAL, kiasi cha miaka 17 iliyopita, kuingia sokoni na kuuzwa.


Hatua hii imetokana na taarifa moja inyoitwa the Bloomberg Report, iliyotolewa hivi karibuni inayodai kuwa taarifa nyingi za madhara ya triclosan (kiasi cha kurasa 15 nzima!) ziliondolewa katika nyaraka zilizowasilishwa TFD wakati huo kuomba dawa hiyo kuruhusiwa kuuzwa na kutumika.


Uwezekano ni mkubwa kuwa mwisho wa siku FDA itatoa taarifa yenye kuonyesha kuwa imekosa ushahidi wa kutosha unaoonyesha kuwa triclosan inasababisha kweli madhara kwa binadamu.


Hivi ndivyo historia inavyoonyesha. Mamlaka hizi zina mahusiano ya karibu sana na makampuni makubwa yanayotengeneza bidhaa mbalimbali hivyo ni muhali kutarajia matokeo tofauti. Umuhimu ni kuchukua hatua wewe mwenyewe kujilinda dhidi ya bidhaa zenye madhara na hutapata hasara yoyote kwa kubadilisha aina ya dawa ya meno unayotumia na kuachana na COLGATE TOTAL.
 

Attachments

  • colgate.jpg
    15.4 KB · Views: 967
hii mada imenigusa sana, nadhani nimekuwa victim wa hili swala la dawa za meno, nimekuwa nikitumia napatwa na kikhozi, kuwashwa koo vibaya mno, na makohozi uwa rangi nyekundu na kutoa kama usaha na homa kali, yaani mwili mzima uhuma na hii imetokana na kutumia dawa nyingi za hapa pamoja na Whitedent, lakini nilipo jaribu white dent herbal ikawa nafuu kidogo...lakini baadae nazo nikagundua baadhi yake ni matatizo hayo hayo na ninasikia dawa nyingi za meno zina tengenezwa mitaano hivyo ni fake...kusema kweli hata sijui nawezaje kukwepa hili janga la matumizi haya ya dawa za meno? kwangu ni tatizo kubwa sanaaaaaa!
 
Solution ni mswaki wa mti na mkaa au majivu bass tupa kemikali kulee. Na kila u kimaliza kula sukutua kinywa na maji safi achana na mouthwash. Vitu asilia ndo mpango mzima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…