Bado unayo nafasi

Saint Anne

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2018
Posts
76,039
Reaction score
230,142
Habari

Najua unapitishwa katika magumu, mazito na maumivu ni makali hayastahimiliki lakini nakuomba mno usivunjike moyo.

Usiwaze kunywa sumu
Kunywa sumu si suluhisho,wapo watu wengi sana nyuma yako wanakutegemea. Kunywa sumu hakutatatua Shida unazopitia.

Usiwaze kuacha kufanya
Inawezekana kabisa umeshajaribu mara nyingi kufanya lakini umejikuta umeishia kushindwa. Usiache kujaribu tena..ipo siku utaweza.

Usiwaze kufunga biashara
Hata kama wateja hawaonekani na kila siku unaishia kupata hasara. Ukiwatazama wenzio wanaofanya biashara Kama yako wanafanikiwa lakini kwako ni tofauti...Ipo siku utafanikiwa.

Usiende kwa mganga,usikubali kabisa shetani akakudanganya,Endelea kumuomba Mungu naye atatenda.

Bado lipo tumaini,bado unayo nafasi,Mungu analo kusudi na Wewe.
-Unayo nafasi ya kurekebisha makosa yako.
-Unayo nafasi ya kujipanga upya.
-Bado unayo nafasi ya kufanya vizuri zaidi.

Mungu amekuamini kwamba unaweza na Ndiyo maana bado Amekupa huo uzima.
Usikubali kuishia njiani,
Hakikisha unafanya zaidi ya ulivyofanya Jana.

Be blessed
 
Nendeni kwa waganga
Kuroga lazima jamani haya nyie danganyeni
 
Lete mifano
Mkuu hapa tutaanzisha mjadala mwingine ndani ya mada tofauti.

Kwa kifupi tu wewe Saint Anne ungekuwa ndio una mamlaka na uwezo alionao Mungu ungechukua hatua gani juu ya mateso na mahangaiko wanayopitia viumbe vyote? Viumbe vyote si binadamu tu!

Mungu alikuwa anao uwezo wa kuumba ulimwengu usiowezekanika kufanyika mabaya lakini hakufanya hivyo kwanini?
Sifa za huyu Mungu ni;
1) Muweza wa yote
2) Mjuzi wa yote
3) Mwenye upendo sana
4) Hutujua vyema hata kabla ya kutuumba.

Sasa ndugu yangu katika sifa zote za huyu Mungu anaonekana kupwaya sana kiasi kila mwenye akili timamu kujiuliza kama huyu Mungu yupo kweli au ni hadithi tu.

Mimi ni binadamu lakini nimeweza kuyaona na kuyaishi mapungufu ya huyu Mungu/kama yupo kweli.

Mashaka yangu ya kwanza juu ya huyu mwenye enzi ni pale alipomuumba kiumbe wake kipenzi/lucifer/shetani/ibilisi/mchonganishi na maneno mengine mengi anayoitwa huyu kiumbe wake.

Hivi huyu Mungu wakati anamuumba huyo kiumbe wake hakujua tarehe fulani atamuasi? Kama alijua, kwanini hakumboresha ili asiasi au kughairi kumuumba?

Kitendo cha lucifer kuja kumbadilikia Mungu, moja kwa moja hayo tunayaita ni upungufu wa Mungu kwa sababu hatutegemei kazi mbovu kutoka kwa Mungu.

Kama tuaminivyo ni kwamba, tecnolojia ya Mungu ni bora kuliko ya mzungu. Mzungu akitengeneza kitu hujitahidi kukifanya kiwe bora japo hana uwezo wa kukifanya kiwe bora milele.

Mungu huyu mwenye tecnolojia ya kufanya au kuamrisha kazi zake ziwe bora milele hajaweza kufanya hivyo japo anajipa sjfa za kufanya mambo mkamilifu huku akijisifu kuwa mwenye upendo na mwenye kutambua hatua zote watakazopitia viumbe wake.

Sasa huyu Mungu baada ya kufanya makosa yake huko mwanzo, tunaona makosa yaleyale kayarudia kwa kumuumba mwanadamu mkamilifu mwisho nae akawa si mkamilifu.

Swali linarudi palepale sababu Mungu ni yuleyule mwenye sifa zilezile za kutenda mambo mkamilifu, mwenye upendo, mwenye kutambua yote hata miaka Billions kadhaa ijayo.

Wakati anamuumba kiumbe wake mpendwa/Adam hakujua huyu kiumbe atarubuniwa na kiumbe wake muasi shetani? Kama alijua kwanini asingeghairi tu kumuumba au kumboresha zaidi ili aweze kuruka viunzi vya shetani?

Kwasababu hakuweza kung'amua hayo au kuyafikiria na kughairi, moja kwa moja tunauona upungufu wa kazi zake kwa mara nyingine.
Je, huyu Mungu yupo kweli au ni hadithi tu za wanadamu?

Kama mimi nimeweza kuyafikiri hayo, kwanini Mungu mjuzi wa yote, muumbaji na mwenye upendo hakuweza kuyafanyia kazi? Leo hii wewe hapo una mifano kibao ya watu wanaoteseka na maisha haya ambayo wamelazimishwa tu na huyo Mungu kuishi pasipo kuchagua.

Hapa duniani kuna watu wamebambikiwa kesi ambazo si zao, kuna watu wanaishi maisha mabaya sana na kila muda wanaona heri wasingezaliwa, kuna ambao wapo mateka wanateswa na hawana msaada hata wa kukatiza uhai wao, kuna ambao wanaishi katikati ya vita kila sekunde wwpo pressure juu na ndugu zao wanauawa mbele ya macho yao na wengine kutiwa ukilema, kuna ambao wanazaliwa na kufa papo hapo, kuna wanaoteseka na magonjwa mabaya sana miaka mingi mwisho wanakufa, kuna wanaopewa mimba na kukimbiwa mwisho maisha yao yanakuwa ni machungu sana, kuna wanaodhulumiwa huku wakiwa hawana msaada na mengineyo mengi.

Sasa Mungu huyu yu wapi mpaka viumbe wake wapendwa wanateseka namna hii ingali hawakuomba kuwepo duniani?
Mungu huyu yupo kweli au ni hadithi tu?

Kama huyu Mungu yupo, bado nitarudia kauli yangu ya mwanzo kwamba Mungu ameumba watu wake na kuwatelekeza!
Pia inaonesha Mungu huyu ni mwongo na mwenye kuburudika kwa yale machungu wanayopitia wanadamu na viumbe wengine.
 
Kwahiyo unaamini kwamba Mungu hayupo?

Kila alichokiumba Mungu na tazama aliona chafaa.

Hayo yote uliyosema yanatokana na anguko la mwanadamu.
Go and read Genesis chapter three..Go through the whole chapter..
It's all about "The fall of man"
 
Kwahiyo unaamini kwamba Mungu hayupo?

Kila alichokiumba Mungu na tazama aliona chafaa.

Hayo yote uliyosema yanatokana na anguko la mwanadamu.
Go and read Genesis chapter three..Go through the whole chapter..
It's all about "The fall of man"
Sio hayupo tu, bali hawezekani kuwepo kwasababu yale machache kumhusu yameonekana ni hadithi zisizo na maana kwenye mizania ya ukweli.

Kila alichoumba aliona ni chema kumbe sivyo alivyotegemea. Je, ni mjuzi wa yote kweli na ni muweza wa yote?

Mwanzo sura ya tatu nimekwisha isoma mara nyingi tu na nikaona ni blah blah zilezile za Mungu huyu kutaka kulaumu vitu alivyovitengeneza mwenyewe baada ya kazi yake kuonekana imepotoka kwa kiwango kikubwa.

Kwanza kitendo cha yeye kuwaachia maagizo viumbe wasiojua jema na baya ni upumbavu kwasababu hata wewe huwezi kufungia kuku ndani pamoja na visahani vingi vyenye vyakula tofautitofauti kikiwemo chenye mchele alafu uwaambie kuku wako, vyakula vyote vilivyoko kwenye visahani mwaweza kula isipokuwa kisahani chenye mchele, kwa kuwa siku mtakapokula mchele mtakufa hakika!.
Sasa chukulia kuku watakuelewaje ilihali hawajui jema na baya. Kumbuka kama ilivyoandikwa ni kwamba, kabla ya wazazi wetu/Adam na Hawa hawajala tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya walikuwa hawajui jema na baya ndio maana hata hawakujua kwamba wapo uchi.

Baada ya kula walichokatazwa na Mungu ndipo fahamu hizi tulizonazo zikawajia wakaamua kujificha.

Je, wewe ukiwaachia kuku maagizo ya namna hiyo watakuelewa? Huoni kuna uhuni wa hali ya juu katika maelezo tunayoambiwa ni ya muumbaji?

Ndugu kama hunielewi nitakuwa na wasiwasi na akili yako katika kupambanua mambo au utakuwa mmoja wa wale wanaoabudu uoga na si Mungu wa kweli.

Mimi tangu nimesoma vitabu hivi vinavyoitwa vitakatifu nimeamua kuacha unafiki na kusimama pamoja na ukweli!

Kwa akili yangu ndogo tu sidhani kama kuna kiumbe chochote kingeteseka endapo ningekuwa na uwezo huo wa Mungu inaesemekana anao
 
Aiseee[emoji134]
Mkuu unafika hatua ya kumkufuru Mungu namna hiyo??

Uzuri ni kwamba mawazo ya Mungu si kama mawazo ya binadamu.
Kwa hiyo usitake Mungu afanye vile unavyotaka wewe.

Yeye Anasema si mwanadamu hata aseme uongo..
Cha muhimu ni wewe kufuata kanuni na maagizo yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…