Bado wakulima na korosho zao na wanunuzi na pesa zao

mbj

Member
Joined
Jun 24, 2013
Posts
39
Reaction score
44
Ifikie hatua soko liwekewe bei dira ili kila anakuja kununua korosha ajue anaanzia wapi, Au kitaalamu imekaaje watu wanapoambiwa mnada halafu hakuna bei dira?
 
Ifikie hatua soko liwekewe bei dira ili kila anakuja kununua korosha ajue anaanzia wapi,Au kitaalamu imekaaje watu wanapoambiwa mnada halafu hakuna bei dira?
Kuna sehemu wananunua kilo 1 ya korosho Tsh 1,400 aisee huu ni ukatili.
Mimi sio mkulima ila nawahurumia wakulima. Imagine unauza kilo 1 ya korosho unapata pesa ambayo haiwezi kununua hata kilo 1 ya unga.
 
Kuna sehemu wananunua kilo 1 ya korosho Tsh 1,400 aisee huu ni ukatili.
Mimi sio mkulima ila nawahurumia wakulima. Imagine unauza kilo 1 ya korosho unapata pesa ambayo haiwezi kununua hata kilo 1 ya unga.
Very sad!
 
Kuna sehemu wananunua kilo 1 ya korosho Tsh 1,400 aisee huu ni ukatili.
Mimi sio mkulima ila nawahurumia wakulima. Imagine unauza kilo 1 ya korosho unapata pesa ambayo haiwezi kununua hata kilo 1 ya unga.
Tunaambiwa nchi inafunguliwa hapo... kiukwel wakati wa magufuli bei za korosho zilikuwa mzuri na pale wahuni walipokataka kushusha bei serikali ikaamua kununua na wote tukapata hela zetu ila ukiingia humu mitandaoni wahuni wakina zito kabwe wanadai watu hawajalipwa pesa
 
Very sad!
Kama msimu huu tumeletewa pembejeo ambazo kwakweli hazina matokeo mazuri na tunahisi kama zimepitwa muda wake, fikiria mimi nilijiandikisha nina mikorosho 570 ila kila wakigawa dawa napata lita 2 na siku wakigawa ya unga napata mfuko mmoja tu,kiasi kwamba hizo dawa ninazopewa hazitoshi kuhudumia shamba langu hata robo ya idadi hiyo
 
Ifikie hatua soko liwekewe bei dira ili kila anakuja kununua korosha ajue anaanzia wapi,Au kitaalamu imekaaje watu wanapoambiwa mnada halafu hakuna bei dira?
Bodi ya korosho ni wajanja wanaofanya udalali kwenye zao la korosho. Katika vitu vinavyoshangaza ni kuona wakulima wanakusanya korosho zao halafu tajiri ndo anaenda kuzinunua, nadhani hii inapingana na soko huria linavyotakiwa liwe. Ilitakiwa matajiri waweke bei yao ya kubunulia mezani na iwe updated Kila mwisho wa wiki halafu mkulima achague kuuza korosho kwa bei hiyo au akaushe asipeleke korosho zake sokoni. Sasa Bodi ya Korosho hili hawalioni kuwa ni tatizo kweli au au wamejitia upofu?
Tumechoka kuwanufaisha wachache korosho ni Miongoni mwa mazao ambayo gharama za uendeshaji ni kubwa. Rekebisheni hapo kwenye utaratibu wa mauzo (minada).
 
Dunia hii ndugu ni mbaya sana na isitoshe kwa sasa tajiri haoni hatari kumtibulia life mwenye maisha duni na ya chini,huwez kuleta bei unayotaka ww kununulia bila kuafikiana na upande wa unaeenda kumnunulia zao lake na kibaya zaidi kuna watu wanatokea sub tena ndio wasimamiz wa uuzaji wa mazao na wako kimya tu wanakubaliana na unyonyaji unaoendelea,lakini ipo siku mawe yatapiga kelele.
 
Bora serikali iwaokoe wakulima hii sio poa kabsa,nadhani kunaujanja mdogo tu unafanyika kumuumiza mnyonge!imani yangu ni kua wanunuzi wanazihitaji korosho ili biashara yao ifanyike na ss tunahitaji kuuza ili kuendeleza uzalishaji so pasiwe na ukandamizwaji kwa mkulima.Wasijekununua korosho za wakulima kanakwamba wanafanya msaada tu.
 
Mm najua na ninawaona pia wanavyohangaikia kupambania zao hlo,yaan kama wangekua na umoja wangeamua kitu wanachokifanya now ili hatma ipatikane.
 
Ifikie hatua soko liwekewe bei dira ili kila anakuja kununua korosha ajue anaanzia wapi,Au kitaalamu imekaaje watu wanapoambiwa mnada halafu hakuna bei dira?
Had Sasa wameshindwa kukubaliana?
 
Nadhani serikali imechagua kuua zao la korosho ili kulinda masilahi ya mfanya biashara. Tuendako kama wakulima tuwe na mipango mkakati.
1. Tuboreshe zao letu Kwa kukata mikorosho ya zamani na kubebesha mbegu za kisasa ambazo ni kubwa na zina ujazo wa kutosha.
2. Tuvune mazao yetu tuanze kubangua wenyewe Ili kuongeza thamani.
3. Soko letu la ndani linatosha na korosho bei iko juu Kwa soko la ndani,Kwa waokaji tunauziana Kwa bei ya 2000-2500 Kwa kilo hii haina kipengele,hakuna makato ya Tanecu,mamcu Wala Tozo za serikali.


Hao madalali tuwaoneshe Kwa vitendo ndo watajua hawajui. Na mwaka huu wasipokuwa makini wanaenda kuikosesha serikali pesa nyingi Sana kizembe na serikali kupitia waziri mwenye dhamana amefumba macho kama vile haoni.
 
Mtwara wamegoma kuuza
 
Ifikie hatua soko liwekewe bei dira ili kila anakuja kununua korosha ajue anaanzia wapi, Au kitaalamu imekaaje watu wanapoambiwa mnada halafu hakuna bei dira?
Mwaka Jana korosho iliuzwa mtwara na dar,kwaiyo mwaka huu wakulima wanataka mnada ufanyike mtwara pekee.

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
 
Ifikie hatua soko liwekewe bei dira ili kila anakuja kununua korosha ajue anaanzia wapi, Au kitaalamu imekaaje watu wanapoambiwa mnada halafu hakuna bei dira?
Uko ndio tuliko anzia wahuni walikua wanaweka bei ndogo sana elekezi ili wapige cha juu..bodi ya korosho ilijaa wahuni watupu.

Ndio ukaja huu mchongo wa minada kwamba wafanyabishata ndio watakua wanacompete kwa kuweka bei zao siku ya mnada.

Hili nalo limeingiliwa wafanyabiashara wakishirikiana na wahuni wametengeneza cartel wanenda na bei zao ambazo zitawanufaisha wao huku wakimlalia mkulima.

Kimsingi mkulima wa nchi hii asipoa amka na kiwa aggressive hakuna atakachobambulia zaidi ya kulialia kila siku.

Wakulima watengeneze umoja strong ambao hautayumbishwa na wanasiasa au wafanyabiashara.

Zaidi waanze kubangua korosho zao hii ndio itakua pona yao.

#MaendeleoHayanaChama
 
U have a point hata hivyo hizi bodi lengo lao ni kunufaisha serikali na wafanyabiashara sio mkulima.

Kumbuka hao wafanyabiashara na bodi hukaa meza moja kabla msimu kuanza.

#MaendeleoHayanaChama
 
Serikali ipi hii inayokaa na wafanyabiashara kabla ya msimu kuanza.

Serikali hii iliyojaa madalali kupitia bodi ya korosho..mkulima wa kusini asipo amka na kusimama imara ataendelea kuumia tu.

Hao serikali na wafanyabiashara wapo hapo kumvuna mkulima na kujipata faida huku mkulima akiachwa hohe hahe.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mtwara wamegoma kuuza
Kote wamegoma..suala la kujiuliza watagoma mpaka lini??njaa haina baunsa watalegeza tu ngoja ijumaa hii tuone.

Hapo wataongezewa 200 basi watalainika wahuni watajibebea korosho.

Mana tayari wameshajua ni aina gani ya wakulima.

#MaendeleoHayanaChama
 
Had Sasa wameshindwa kukubaliana?
Worse enough!kuna watu wanatumika nadhani,just imagine mtu anakataa kuuza mazao yake kwa bei isiyokua na manufaa kwake,ila kunamtu anakuja nakusemanuzeni tu maana soko la dunia kwa upande wa korosho limeshuka hii haiko sawa,kwa sababu biashara hii sasa imegundilika kua niya baadhinya watu hapa mjini na wananufaika wao tu,Kulima na kuhudumia shamba la mkorosho ili ipatikane korosho hailingani na kuinunua na kuipeleka kiwandan the uifinalise ikatumike kulima jaman ni kugumu,wakulima wa tz ni tofauti na mataifa mengine kabsa,ukiangalia kwingine kote unakuta mkulima ana nafasi ya pili katika ubora wa maisha lakini hapa mkulima ni futionla miguu,na hii ni kwa sababu ya kulima kwa mazoea,wakulima wanapaswa kubadilika eti asipokuja mnunuzi hakuna cha kuzifanyia korosho, nonsense indeed.WAKULIMA WAACHE MAZOEA WALIME KIBIASHARA NA SIO WAMTEGEMEE MNUNUZI,HII INATAKIWA WATEGEMEANE KATI YA MKULIMA NA MNUNUZI HAPO NDIPO VALUE YA MAZAO KAMA KOROSHO YATAPANDA NA KUWA NA TIJAILA SIO MNUNUZI ANAKUJA KUNUNA KOROSHO KAMA HISANI KWA MKULIMA(MSAADA)AFU KUNA BODI YA KOROSHO INAYOTAFUNA USHURU NA KUWA NA UHAKIKA WA KILA MKULIMA AUZAPO CHAO KIPO,
 
Duh mateso aisee na ziliivo na gharama kwenye kulima
 
Reactions: mbj
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…