Wasalaam,
Tunakiri huenda hatujakidhi mahitaji yako, taasisi zote zinaendeshwa kwa hali ya kupenda kujiboresha. Kwa uungwana na unyenyekevu wa dhati kabisa, tungefurahi kufahamu taarifa ulizozitarijia lakini hukuwa umezipata. Pia tunapenda kukufahamisha ya kwamba, katika uuzwaji wa mali hapo mtandaoni, hatuhusiki katika mauzo kwa vyevyote vile, madalali na wenye mali ni sehemu ya wateja wetu, tukiwa na jukumu kuu la kuwawekea jukwaa la hao watajwa kujitangaza na kuwakutanisha na wahitaji kiurahisi zaidi.
Mtandao wetu umesheheni makala mbalimbali ambazo kwa idadi zinafika walau 100, tumeweka taarifa, miswada na matamko ya serikali ili kuhabarisha umma, wadau na wawekezaji wa ndani na nje, tunatangaza mali zilizopo zaidi ya mataifa 120 duniani.
Tunakushukuru kwa kututembelea tunatarijia ushirikiano wako wa dhati kati uboreshaji wa huduma zetu.
Wako katika ujenzi,
Afisa habari.