Bahalul mwenye hekima 2

KABAVAKO

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2011
Posts
229
Reaction score
32
BAHLUL NA CHAKULA CHA KHALIFA
Siku moja Harun al-Rashid alimpelekea Bahlul sinia iliyojaa kwa vyakula mbalimbali. Mfanyakazi alipomwakilishia Bahlul vyakula hivyo, alimwambia: "Hivi ni vyakula makhususi vya Khalifa na amekutumia wewe uvile."

Bahlul alimtupia mbwa aliyekuwa ameketi karibu, vyakula vyote alivyoletewa.

Alipoyaona hayo, mfanyakazi wa Harun al-Rashid alighadhabika mno na kusema kuwa hiyo ilikuwa ni kumvunjia heshima Khalifa na angalimjulisha hivyo.

Hapo Bahlul alimjibu: "Wewe kaa kimya! Iwapo na mbwa atafahamu kuwa vyakula hivyo vinatoka kwa Khalifa, naye pia ataacha kuvila!

Fundisho: Inatupasa kukatalia zawadi kutoka kwa waonevu na wadhalimu ili visituathiri sisi kutotimiza wajibu wetu wa ukweli na haki.
 
Ahksante kabavako kwa hadithi yako yenye hekima na busara tele mungu akuzidishie maarifa
 
Ahksante kabavako kwa hadithi yako yenye hekima na busara tele mungu akuzidishie maarifa

shukrani ndugu yangu kwa kuutambua mchango wangu, hii inanipa nguvu zaidi ili niandike thread nyingi zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…