Baharia alivyokamatwa kama Muasi akiwa Guinea Bissau

Baharia alivyokamatwa kama Muasi akiwa Guinea Bissau

Nafaka

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
12,154
Reaction score
31,246
Ninaendelea kuwadonolea visa vya Bwana baharia mzamiaji.
Akiwa anataka kusafiri kwenda spain huku akiwa hata hata passport. Akiwa kafanikiwa kufika Libya na kupata maswahibu, mpaka kaka yake akamtumia dollar 2000 aondoke pale Tripoli baada ya raia wengi wa kigeni kuawa.
Baharia anaona ili aweze kufika Spain hata kama ni kwa njia za magendo ni muhimu awe na passport. Kutokana na habari za kiintelijensia walizokuwa wanapeana mabaharia wa nchi kavu wenzake, aliambiwa passport rahisi anayoweza kuipata ni ya Guinea Bissau. Hivyo ikamlazimu alipoondoka Libya, asafiri aingie Algeria, halafu Mali, Halafu, Guinea then adondoke Guinea Bissau.
Kweli safari yake ilikuwa safi akafanikiwa kufika kwenye hako kanchi kadogo, akapata passport yake kama kawaida.
Lakini kwa bahati mbaya kipindi hicho ndipo kulikuwa na mapigano nchini Guinea Bissau baada ya Jenerali wa jeshi la Guinea Bissau wa wakati huo aliyejulikana kama Ansumane Mane ambaye alikuwa akfukuzwa kazi na raisi wa Guinea Bissau wa wakati huo aliyejulikana kama Vieira. Hii ilikuwa mwaka 1998 na kumbuka huyo jenerali alishiriki kumweka raisi madarakani.
Kufukuzwa kwake kazi kulipelekea jaribio la mapinduzi ambalo halikufanikiwa hivyo likapelekea nchi kuingia vitani.
Baharia alifanikiwa kupata passport, sasa wakati anatoka Guinea Bissau anarudi Guinea akiwa kakaribia mpakani yuko kwenye basi, mara jeshi la serikali linasimamisha lile basi. Wanalipekua kisha wanamchukua yeye na kuanza kumhoji. Baadae wanaanza kumtuhumu kuwa yeye ni askari wa kukodiwa waliokuwa wanakodiwa na kundi la waasi lilikuwa linaongozwa na huyu jenerali kutoka nchi za kigeni..
Wakaanza mpiga huku lile basi likiwa limezuiliwa lisiondoke kwanza. Jamaa akajitetea, sana lakini hawakumwelewa. Akapigwa sana akavuliwa mbele ya watu. Baada ya kumtesa sana wakagundua kuwa hakuna analojua, maana kwanza waasi walikuwa na tatoo ya ng'e mgongoni kwao kama alama yao.
Basi jamaa akaachiwa aendelee na safari akawa kaokoka kwenye mtutu wa bunduki.
Safari yake ikampeleka Guinea, akaingia Guinea ambapo kwa bahati akaja kukutana na jamaa waliokuwa wame stuck wote Tripoli miezi sita iliyopita aliondoka, akamkuta jamaa yuko hapo na anaoneakana ana vijisenti na ana mahali pa kuishi tena ana mwanamke.
Jamaa akamkaribisha kwake na kumpa hifadhi, na kumbe alikuwa amefanikiwa kupata kazi ya kufundisha chuo pale, halafu akawa ni mhubiri pia. Tatizo jamaa akaanza kumlazimisha baharia aachane na safari zake akae pale naye awe mhubiri.
Baharia akaona jamaa mbona anamletea habari siyo wakati yeye ana mawazo ya kufika ulaya. Baharia siku moja akamwambia yeye hawezi uwa mhubiri na wala hana mpango huo. Yeye nia yake bado ni kwenda Spain. Jamaa kusikia hivyo akakasirika akamtimua baharia kwake.
Baharia hakuwa na pesa alikuwa kamaliza ela yake kwenye passport, akarudi mtaani na kuwa chokoraa na kuwa analala sokoni chini ya meza, mara kwenye mabaa n.k.
 
Halafu asilimia kubwa ya wazamiaji walikuwa vichwa sana na Elimu zao kabisa
 
Halafu asilimia kubwa ya wazamiaji walikuwa vichwa sana na Elimu zao kabisa
Yes huyo mwenyewe alikuwa amemia lakini alikuwa kala kitabu alikuwa ana kidegree chake
 
Degree ni nini kama sio elimu?
Nadhani utakuwa ni wa jana wewe!.

Miaka iliyopita wilayani kwenu ukichaguliwa kuendelea na masomo (form one, six au chuo) ilikuwa ni furaha sana kila ukipita au mzazi wako lazima apewe sifa.

Na ukimaliza six au chuo ilikuwa unapitia kazini kabisa na ukirudi home ndiyo usiseme kabisa yaani utaelewa tunachokiongelea hapa.

Nowdays bora kumaliza tu ili uwe na cheti geto baaasi.
 
Back
Top Bottom