Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,497
- 4,775
Kwa muda mrefu sasa,Kampuni ya Ukopeshaji Pesa ya Mtandaoni ijulikanayo kama BahariPesa imekuwa na Tabia ya Kutoa siri za wateja wao hasa wale wanaodaiwa na kutuma taarifa zao kupitia namba za watu wengine bila kuwahusisha watu hao pindi wanapotumiwa taarifa hizo. Pamoja na BahariPesa licha ya kuwa inachakata taarifa za watu na kudhalilisha wale wanaowadai,lakini pia imekuwa ikitoa lugha chafu na za matusi na za kudhalilisha pindi watu waopokea meseji za wadaiwa wanapotaka kuhoji juu ta matumizi ya namba zao kwa kampuni hiyo.
Kampuni ya BahariPesa mbali na kutumia lugha za hovyo kwa watu wanaohoji juu ya uhalali wa wao wa kama kampuni kuchakata taarifa za watu kinyume na taratibu na makubaliano ya wahusika, kampuni imekuwa kimya bila ya kujibu malalamiko wa watu.
Nimeambatanisha hapa record ya sauti ya mtu kutoka katika kampuni hiyo ya ukopeshaji ambae inatumia application za plastore kuwakopesha na kisha kumwaga siri za wateja wao hadharani.
Huu ni udhalilishaji wa hali ya juu,lakini pia serikali iwapige marufuku kampuni hiyo kututumia ujumbe wa watu wanaowadai.
Tumechoka matusi yao.