Siku za hivi karibuni nilibahatika kutembelea nyumba anayoishi mwanamuziki wa nyimbo za Injili, Bahati Bukuku iliyopo maeneo ya Kibamba, kwa kweli niliogopa, Bahati anaishi kwenye ghorofa la kifahari mno na la kisasa.
Hakika huyu mwanamuziki anaishi maisha mazuri sana, hongera zake, ila nilijiuliza ni mziki tu wa Injili ndio umemuwezesha kujenga ghorofa la thamani kiasi kile? Nilitamani kupiga picha mbea mie sema haikuwezekana kutokana na mazingira yaliyokuwepo, ila Bahati sasa ivi ni millionaire.