Bahati Iliyoje hii jamani

sayoo

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
5,280
Reaction score
7,930
BAHATI ILIOJE HII JAMANI.
××××××××××××××××××

Kuna siku nilikuwa maeneo ya Mjini kati
(City Center), nikaipenda suruali moja ya
shilingi 15,000/= na pesa sikuwa nayo
ikabidi niende kutoa kwenye ATM ya
Postal.
Nimefika pale sikukuta mtu hivyo
niliingia moja kwa moja, nimefika mle
ndani nikakuta Pesa Kibao zimemwagika
pale kwenye kitundu cha kutolea pesa,
ATM Card ilikuwepo pale imetokezea na
Pembeni kulikuwa na Pochi ya Kike
iliyoonekana kutuna vilivyo.
Kwa woga mimi huku nikitetemeka
mapigo ya moyo yakiwa yameongezeka
nikatizama nyuma yangu sikuona mtu,
nikachukua zile Pesa harakaharaka, ATM
na ile pochi.
Ile natoka nje kuna dada mmoja alikuwa
anakuja kwa kasi maeneo yale nikapata
uoga nikamuuliza “Samahani dada, kuna
kitu umesahau humu”, yule dada
hakunijibu kitu kaingia kwenye chumba
cha ATM akachomeka Kadi kutoa hela
mi nikaondoka zangu fasta kuelekea
home.
Nimefika home nikajifungia ndani na
kuzibwaga zile pesa kitandani,
nikafungua wallet nikakuta imejaa
dollar, Vipodozi, iphone na ki-Nokia
kidogo cha tochi, ATM Card mbili za
Benki tofauti ambazo zilikuwa
zimezungushiwa karatasi iliyokuwa na
namba za siri za ATM zote, moyo
ukanilipuka paaaa!!! Nikaona bora
Nipumzike kwanza kitandani!!
Muda si mrefu ile iphone ikaanza kuita,
nilipoangalia halikutokea jina nikaona
bora nipokee nimsikilize anasemaje,
ilikuwa sauti ya kike iliyoongea kwa
huzuni kwa kubembeleza huku akilia na
alijitambulisha vizuri kuwa ile mali ni ya
kwake! Huruma ilinijia nikamwelekeza
nilipo aje kuchukua...
Hakuchukua muda akawa amefika nami
nikamkabidhi vitu vyote naye
akavihakiki na kukuta viko sana: Milioni
3 za Kibongo na Dollar 500. Dada
kanishukuru na kunipa ile Millioni 3 ya
kibongo mi nikazikataa kwasababu ni
mali yake na alizisahau tu.
Alinitoa hofu kwa kunisihi nichukue tu,
mi kama binadamu mwenyezi Mungu
atanilipa, nikakataa... Mwishowe
akaomba namba yangu na kuondoka
zake, akawa ameniacha ndani huku njaa
sasa nikaanza kuisikia, nilikuwa na buku
mbili nikaenda kula viepe kavu na soda
nikawa powa.
Sasa jana kanipigia simu kuwa anakuja
nimsubiri, dakika tano tu akanipigia tena
kuwa ameshafika yupo nje yupo ndani
ya Prado mpyaa nikaingia tukaondoka
akaenda kunionyesha kwake kisha
tukaelekea kwenye nyumba nyingine
iliyokuwa ndo imekamilika kujengwa
akaniambia hii itakuwa yako
akanikabidhi baadhi ya nyaraka na
funguo zote sikuamini...!!
Akanisindikiza kwangu, kufika home
ananiambia hiyo gari (Prado) nayo
ananiachia ni kwa mema tu
niliyomfanyia, ndani ya ile gari kulikuwa
na brifcase iliyokuwa na pesa
akaniambia pia hii pesa itakuwa yako ya
kuanzia maisha, na kumbe yule dada
alikuwa kanipenda akanikumbatia kwa
nguvu nikiwa pale kwenye seat oooh!!
umasikini baibai...
Akiwa kanikumbatia akihema kwa kasi
juu ya kifua changu. Mara nikahisi kubanwa na haja ndogo, nikakimbia fasta chooni na kuanza kukojoa, nasikia raaaha mkojo hauishi mara nikahisi mtu
akinishika begani na kuniita kwa sauti.
“kaka Will weee kaka will

KAKA will llllllll
Kakaaaaa."

Kwa sauti ya usingizi "naaam"

"Amka bwana unaharibu godoro"

Alikua ni mdogoangu wa mwisho ananiamsha hizi ndoto nyingne za kisengerema sana[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

*PUMBAVU KABISA*
 
Mmh kweli tulipofikia Mheshimiwa atasababisha vifo kwa watu km nyie....vuta subira neema inakuja hiz ni stress tu
Mkuu acha kabisa ivi ndo natoa godoro nje nikalianike maana limeloa balaaa, hizi ndoto za hivi zizitaki tena
 
Lala uote tena umekua kuku unataga yai....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…