Bahati (luck) ni nini ?

kidole007

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2012
Posts
3,094
Reaction score
1,876
Wana jamii intelligence

Bahati sio neno jipya
tumezoea kusikia misemo kadha wa kadha kuhusu bahati mfano ana bahati nzuri ana bahati mbaya nk


Napata maswali mengi kuhusu hii bahati

1. bahati ni nini

2. bahati mtu huzaliwa nayo (inborn) au unaweza jipatia bahati yako katika kipindi cha maisha

3. kwann baadhi ya watu wanaonekana kuwa na bahati kuliko wenzao
Je kuna namna mtu anaweza jitengenezea bahati yake

4. inafahamika kuwa bahati inaweza kua mbaya au nzuri
je hizi bahati mbili zina tegemeana?

karibuni kwenye mjadala..
 
Hiyo ni nature tuu!!!
Ni sawa na faida vs Hasara!!
Carl Max aliwahi kusema hili ktk kitabu chake alichozungumzia juu ya ubepari

"Everything on earth exist in opposite direction"

Mfumo wa maisha yetu no matter what, vitu vipo viwili2 kiukinzani!!
Chema vs Kibaya
Usiku vs. Mchana
Juu. vs Chini
Bahati mbaya vs Bahati Nzuri
kifupi vs kirefu ...............................LIST NDEEEEEFU!!!
For me swala la bahati linaingia hapa!!!
Natural thing....everyone has equal chance to share or not share in life!!!
Whether born with or otherwise!!!!
Theory of Probability can help us more to understand this concept!!!!
 
Mkuu MziziMkavu, Pasco na Rakims hamjapita mitaa hii?
Mkuu CharmingLady , asante kunitonya hii mada!.

Kwa kuanzia, in reality, hakuna kitu kinachoitwa bahati, lucky, wala hakuna bahati nzuri, good lucky wala hakuna bahati mbaya, bad lucky, zote hizi ni "works of powers" from within!. There is nothing new under the sun, everything that happens ni premeditated move, it had to happen that time, na vivyo hivyo ilivyotokea!, ndio manna unashauriwa always shukuru kwa yote, liwe zuri au baya, lilikuwa litokee tuu!.

Mambo yote kwenye maisha yetu yako controlled by the will within us, sasa hii will iki fanya mema, inajenga kitu kinachoitwa "good will" na hii ndio wanaiita bahati!, kismat etc. Ukifanya mabaya unapata "bad will" ndio inaitwa bahati mbaya, balaa au majanga!.

Hii will inakuwa influence positively kufanya mambo mazuri na negatively kufanya mambo mabayo, na ukumbuke lolote linalokupata, it's your own making!.

Kwenye hayo mazuri na mabaya ya will na hapa ndipo kitu kinachoitwa "karma" kina play part, ukifanya maovu, utalipwa maovu na majanga yatakukuta na kuishia kusema ni bahati mbaya, mikosi, majanga, na mabalaa!. Ukifanya mema, utalipwa mema, ndio hiyo inaitwa bahati nzuri, mambo super, neema tele!.

Tatizo la karma, kama haijabance, fidia in a transfer to next generation, hii ndio watu wanaita curse, laana!, yaani unajikuta unamikosi mwanzo mwisho, kumbe ni makosa ya mababu zako!.

Ukisha realise you are on the control of your destiny, be positive with affirmatives you want the best, you'll get the best!.Hata ukiingia casino, unaweza ku will machine ikatema on your favour, ukavuna pesa!.

Ila pia kuna kitu kinaitwa mikosi ya kujitakia, ni mtu kutokuwa mwangalifu na kitu kinachoitwa love compatibility, ambapo uki date na a compatible, unatengeneza goodwill, kismati, life ina shine, mnapata mafanikio makubwa na furaha milele!, uki date na incompatible unajiletea nuksi, ni majanga, na ma balaa kwa kwenda mbele!, siku zote unapokutana na mtu ambaye sio, kuna signs kibao zinakuambia sio, ila una zi ignore, na hata yanapokukuta, unaweza usijue uko na mtu mwenye nuksi, unabakia kujisemea sijui nina mahati mbaya gani!.

Darasa kuhusu mambo haya ni hili hapa

Psychic Powers: Ni nguvu za kufanya miujiza. Wengi wanazo ...

"Will Powers!", "Faith Healing!"-Nguvu za Kufanya Miujiza Ya

The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki Kamili Hapa

Angalizo: Kuna Wengi Wanamwabudu Shetani Wakidhani ni ...



Pasco
 
.......Kwa mtazamo wangu, bahati mtu unazaliwa nayo pia inaweza kuja kwa kujitoa kwako.

Unaweza kujitoa kwa kusaidia wale watu wasiojiweza, wakikupa neno shukrani kutoka moyoni basi nawe utabarikiwa.

Vile vile juhudi zako mwenyewe kwenye kutafuta zaweza leta bahati, utafanikiwa hadi utashangaa!!
 

umenisema, asante Pretty!
 
Last edited by a moderator:

possibility inapokuwa ndogo kinachofata hapo ni bahati tu
kwamfano ni kama bahati tu unapochelewa airpot unakuta nayo flight imechelewa hivyo unaingia. Au ni kama bahati tu kuokota dola 100 asubuhi ..
Katika rundom selection ambapo wengi mnakuwa na equal chance bahati inaweza ikakuangukia
 
So far as itconcern hakuna kitu kinachoitwa Bahati nzuri wala bahati mbaya! Bahati ni kitukizuri always kwa hiyo kiita nzuri ni kuipa sifa isiyokuwa na ulazima, ni sawana kusema ''mama yangu mzazi ninayempenda sana'' hata ungeondoa neon ninayempendasana haiondoi fact kwamba ni mzazi wako!

Upande wapili hautakuwa na maana kujadili kwa phenomenon kwamba bahati ikishakuwa mbayasio bahati tena ni kitu tofauti, kama nidhanivyo ndivyo ni sawa na kumwita aduirafiki kitu ambacho hakileti mantiki!

Kuna watuwamezaliwa na karama zao ukipenda waite gifted,hawa wapo na kuna watuwamezaliwa kwenye fungu la kukosa,kwamba kwanini huyu ni gifted na huyu wakukosa Mungu ndo sababu zake. Ila pia tusisahau kuna watu walizaliwa na karamazao ila kutokana na sababu Fulani Fulani karama hizo zikapotea,labda kwakutozitambua ama kwa kushindwa kuzishappen.
 

Ndiyo maana nikasema "may be it's about the timing or rather choices"
Mfano, flight ilichelewa, yes lakini njia na usafiri uliotumia pengine ndiyo uliosaidia ukaiwahi.
Mfano wa kuokota dola 100,
Kumbuka kilichokufanya ukaikuta na kuiokota ni kile kitendo cha wewe kuchagua kuwa katika hilo eneo kwa wakati huo, iwe ulikuwa njiani kwenda kwa jamaa yako au ulikuwa njiani kwenda kazini. Kumbuka pia njia na mode of transport uliyotumia inahusika.
 

Mbona sijakuelewa naona kama unakubali na kukataa kitu hichohicho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…