Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,611
Nigeria wanaye tajiri mmoja anaitwa Tony Olumelu. Huyu bwana anao mradi maalum (foundation) kwa ajili ya vijana wa kiafrika wenye mawazo mazuri ya kibiashara (entrepreneurship).
Kwa miaka kadhaa amekuwa akihamasisha ujasiriamali miongoni mwa vijana wa bara la Afrika. Waafrika wa mataifa ambayo yameshajitambua kama vila Ethiopia wamekuwa wakifaidika sana na foundation ya Olumelu.
Nimetamani sana jambo kama hili lingekuwa linafanyika nchini mwetu kwa kasi kubwa, ukizingatia kuwa mazingira ya kibiashara ni rafiki licha ya uwepo wa changamoto mbalimbali zinazohusiana na mazingira ya uwekezaji.
Taasisi ya Olumelu inaandaa wajasiriamali vijana wa kiafrika, inawapa changamoto nzuri sana.
Inakera sana kuwaona vijana wa kiethiopia wakiwa kwenye harakati za kuwa wajasiriamali wa kimataifa halafu vijana wa kitanzania wanakalia kununua simu za mikononi kwa ajili ya umbeya wa facebook na instagram.
Inachukiza sana kuwaona vijana wa afrika ya magharibi wakijiunda kwenye vikundi ili waweze kupata mikopo mikubwa kutokana na mawazo yao ya kibiashara, halafu vijana wa kitanzania wamekalia majungu ya kina Mange Kimambi na wengine wasio na adabu.
Vijana wa kitanzania wanasubiri matukio ya wanasiasa ili wapate cha kuongea na kujadili kwenye makundi wa whatsapp wakati huo huko Nigeria vijana wa rika lao wanaumiza vichwa ili waingie kwenye kundi la wajasiriamali wa kesho wa bara la Afrika.
Ni kweli tunao kina Mohamed Dewji, Reginald Mengi na Mzee Bakhresa, lakini hawa bado hawajawa na msukumo mkubwa kwa kundi la vijana ambalo halioni aibu kuishia kwenye mijadala ya kisiasa badala ya kuhangaikia ubunifu wa kwenye ujasiriamali.
Wakati sisi watanzania tunaendekeza kejeli za kitoto kuhusiana na dunia ya viwanda, huko Nigeria watu wanaumiza vichwa ili kufaidika na teknolojia inayobadilika kila kukicha.
Hizi kejeli za mitandaoni na upuuzi mwingine wa kitoto, ni vitu ambavyo haviwezi kuwasaidia vijana wa Tanzania.