SoC01 Bahati mbaya ya elimu na ajira

SoC01 Bahati mbaya ya elimu na ajira

Stories of Change - 2021 Competition

Tailings

New Member
Joined
Sep 20, 2021
Posts
1
Reaction score
1
Habari zenu wapambanaji, hii ni salamu kwa wote wanaopambana kuhakikisha hawafi kwakukosa kitu tumboni ila kwa mapenzi ya Mungu.

Salamu hii ni kwa wale wanaotoka jasho (hata lisiloonekana) katika kutafuta mafanikio ya maisha.
Wengi tunatamani mafanikio. Wapo wanaotamani mafanikio kwa njia yeyote ya halali au haramu. Wapo wanaotamani mafanikio kwa nguvu zao wenyewe na kwa njia ya halali. Wapo wenye fikra kuwa mafanikio yanatokana na elimu walizonazo lakini wapo wanaoamini mafanikio ni kutokana na juhudi wanazofanya katika kile walichodhamiria kukifanya kwa lengo la kupata mafanikio hayo. Ila wapo wanaoamini kuwa mafanikio yapo kwenye ajira na hasa ajira ya kile alichosomea tuu na hapo ndio natamani kupaelezea vizuri nikaeleweka kwasababu yamenikuta.

Ntaelezea kwa mifano ambayo ni hai na wewe mpambanaji mwenzangu utatoa majibu ya lile unalowaza. Tuanze na mfano wa kwanza, mfano huu unapande mbili za kupima. Upande wa kwanza muangalie Muhandisi wa madini katika mgodi mkubwa wa dhahabu nchini Tanzania anaelipwa zaidi ya milion 3 au 4 pesa ya kitanzania kwa mwezi, anaemiliki usafiri mzuri (hauwezi kufanywa uber au bolt), ana nyumba mbezi beach au sehem ambazo chumvi haiombwi dirishani, mwenye uzoefu wa miaka zaidi ya 7 katika fani hii ya madini, akiwa anafanya kazi wiki 6 mgodini na wiki 3 akitumia kupumzika nyumbani na kufurahia mshahara wake mnono na upande wa pili ni kijana mdogo aliesomea fani hiyo hiyo ya uhandisi wa madini ambae hana uzoefu hata wa miaka miwili, ambae alitafuta ajira hiyo hiyo akaishia kumaliza pesa yake ya maji kuprint cv na kununua bundle la airtel kwa ajili ya kutuma vyeti vyake kwa wajomba ili apate hata kazi ya laki 3 kwa mwezi.

Kijana ambae anakata tamaa ya ajira na anaamua kuingia katika biashara ya mazao na kuanza kuuza mchele kwa mali kauli bila mtaji. Kijana ambae kwasasa anasambaza mchele zaidi ya tani 200 kwa wiki jijini Dar es Salaam na Zanzibar akijihakikishia faida ya zaidi ya pesa ya kitanzania milion 4 kwa wiki na milion 16 kwa mwezi baada ya VAT.

Jee kati ya huyu muhandisi mbobezi anaetambulika na makampuni makubwa ya uchimbaji madini na huyu muhandisi muuza mchele nani ana mafanikio? Najua swali hili halina majibu rasmi kutokana na aina ya mafanikio tunayotaka lakini nafahamu wapo wanaowaza huyu muhandisi muuza mchele anawajibika kwa nani kama sio yeye mwenyewe, anaulizwa na nani kuhusu kazi yake kama sio yeye mwenyewe, Analikizo (roster) ya wiki ngapi kwa wiki ngapi?

Biashara yake inauwezo wa kukua mpaka wapi? Lakini hapo hapo yapo maswali kwa muhandisi mbobezi jee ile akiba yake ya milioni 85 bank akitaka kuingiza katika biashara, atamuachia nani kazi yake muhimu ya kuandaa mashimo ya mlipuko? Huu ni mfano hai ambao unaishi, kwa upande wangu wote wamefanikiwa na kama swali la kwanza lingekua kukamilisha ndoto zetu basi Muhandisi mbobezi amekamilisha ndoto yake ila muhandisi muuza mchele ameing'arisha ndoto yake.

Ila kama swali lingekua nani ana mafanikio zaidi ya kiuchumi jibu ni jepesi na wewe mpambanaji unalo jibu hilo. Mfano wa pili hebu tuone kati ya mzee bakhresa mmiliki wa makampuni ya AZAM akisimama upande mmoja na upande wa pili asimame meneja wake mwenye MBA kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam mnakiita mlimani. Mfano huu sitouelezea ila ntawaachia wapambanaji muujadili wenyewe kwenye mamlaka ya vichwa vyenu ila mimi nakuja na hitimisho langu.

Ajira ni muhimu ili biashara ziendelee. Lakini biashara ndio msingi wa ajira zote.
Chagua vizuri aina ya mafanikio yako na ujue tuu wengi tuna sifa lakini hatuna mafanikio.

Ahsanteni
 
Upvote 1
Back
Top Bottom