Bahati nasibu katika mitandao ya simu ipo kwa ajili ya maskini tu?

Striker0011

Member
Joined
May 21, 2011
Posts
63
Reaction score
17
Mitandao ya simu ipo mingi tu, na kila kukicha utasikia mtandao umeanzisha bahati nasibu kwa mfano sasa airtel utasikia shinda gari aina ya IST au vodacom JAY milioni. lakini concern yangu ni kwamba je bahati nasibu hizi ni kwa ajili ya maskini tu au watu wenye kipato cha chini?

Nasema hivi kwa sababu ukiangalia matangazo ya watu wengi walioshinda wakitoa ushuhuda utasikia 'sijui mimi nilikuwa mkaanga mihogo or muuza genge' mfano mzuri ni hii ya Airtel na IST, wengi ni wa hali ya chini wanaotoa ushuhuda tuseme watu wa hali ya kawaida hawashiriki?

Nionavyo mimi hizi ni fix tu hakuna chochote kinachoshindaniwa lile au yale magari ni show tu ili wajiongezee kipato lakini hakuna hata moja linalotoka kwa watu rather yanabaki kuwa mali ya Airtel tu au waendesha bahati nasibu.

Mchezo mchafu kama mazingara tu.
 
Bahati nasibu siku zote nyie washiriki ndio mnamchangia yule mshindi ile zawadi lakini cha kushangaza zaidi wanaoshinda wote ni wa hali ya cchini sijawahi kusikia WAZIRI, RAIS, au Tajiri (Bakhressa au Manji) wameshinda bahati nasibu. CHUKUA HATUA
 
Nadhani sababu ya watu hao kutokushinda ni Hali ya wao kupuuzia michezo Hii licha ya kujaa ulaghai lakini pia watu wa kipato cha kati na chini wamekuwa wakijaribu kucheza na kweli wengine wanashinda.
 
Hakuna lolote hiyo ni kamali tu mfano mzuri ni mtandao wa vodacom wanasema kila siku nicheki sh300 inatozwa wizi mtupu.
 
Mitandao ya simu ipo mingi tu, na kila kukicha utasikia mtandao umeanzisha bahati nasibu kwa mfano sasa airtel utasikia shinda gari aina ya IST au vodacom JAY milioni. lakini concern yangu ni kwamba je bahati nasibu hizi ni kwa ajili ya maskini tu au watu wenye kipato cha chini?

Nasema hivi kwa sababu ukiangalia matangazo ya watu wengi walioshinda wakitoa ushuhuda utasikia 'sijui mimi nilikuwa mkaanga mihogo or muuza genge' mfano mzuri ni hii ya Airtel na IST, wengi ni wa hali ya chini wanaotoa ushuhuda tuseme watu wa hali ya kawaida hawashiriki?

Nionavyo mimi hizi ni fix tu hakuna chochote kinachoshindaniwa lile au yale magari ni show tu ili wajiongezee kipato lakini hakuna hata moja linalotoka kwa watu rather yanabaki kuwa mali ya Airtel tu au waendesha bahati nasibu.

Mchezo mchafu kama mazingara tu.

waza kwa mapana, maskini ni wengi kuliko "matajiri".
 
Naungana na mtoa uzi, hizi ni fix tu, system yao ya uchezeshaji ni very technical so kwa kuwa ni computerised huwa wanaset who wins, utafiti wangu binafsi nimegundua namba zote zinazoshinda huwa special au standard numbers in most cases... Jamaa mmoja kitaa akanidokeza eti huwa wanaset mtu wanampa ushindi wa gari ya Mil 16 may be afu badae au kabla ya ushindi huwa anapewa kama Mil 2 then ile gari inachukuliwa kiulainii na mdau wa system...
 
Mitandao ya simu ipo mingi tu, na kila kukicha utasikia mtandao umeanzisha bahati nasibu kwa mfano sasa airtel utasikia shinda gari aina ya IST au vodacom JAY milioni. lakini concern yangu ni kwamba je bahati nasibu hizi ni kwa ajili ya maskini tu au watu wenye kipato cha chini?

Nasema hivi kwa sababu ukiangalia matangazo ya watu wengi walioshinda wakitoa ushuhuda utasikia 'sijui mimi nilikuwa mkaanga mihogo or muuza genge' mfano mzuri ni hii ya Airtel na IST, wengi ni wa hali ya chini wanaotoa ushuhuda tuseme watu wa hali ya kawaida hawashiriki?

Nionavyo mimi hizi ni fix tu hakuna chochote kinachoshindaniwa lile au yale magari ni show tu ili wajiongezee kipato lakini hakuna hata moja linalotoka kwa watu rather yanabaki kuwa mali ya Airtel tu au waendesha bahati nasibu.

Mchezo mchafu kama mazingara tu.
Masikini ndio wansibiwa zaidi nchini.
Huo mchezo wa Jay Millions uko hivi:
Voda wanawapagsisha watu kununua gari kwa kupiga sms 1544
watu sema miloni moja wanapiga hiyo message na kukatwa shs 400/- kila mtu
Fedha inayopatikana KWA SIKU MOJA NI TSHS 400 MILLION
Wso wananunua ki IST kimoja cha milioni 10
Faida ni Tshs 390 million KILA SIKU.

ZINDUKA!!!
 
Huo ni wizi wa mchana kweupe; fuatilia vizuri wanaodaiwa kuwa washindi wengi wanatoka Dar, na kidogo mikoa ya mwambao wa pwani. Huo ni wizi wanaofanyiwa masikini ili matajiri waendelee kutajirika zaidi.
 
Watanzania Na uvivu wa kufikiria !! Tuna safari ndefu sana kuja kuelewa!! Acha tu!!
 
Back
Top Bottom