KABAVAKO
JF-Expert Member
- Apr 5, 2011
- 229
- 32
Ilitokea siku moja Bahlul na Harun Rashid kukutana katika bafu. Khalifa alimfanyia mzaha kumwuliza Bahlul: "Je iwapo ningalikuwa mtumwa, ningalikuwa na thamani gani?" Bahlul alimjibu: "Dinar hamsini." Harun Rashid katika kughadhabika alisema: "Ewe Mwehu! itawezekanaje hivyo? Mavazi yangu tu yamezidi thamani hiyo! Hapo Bahlul alimwambia: "Kwa hakika mimi nimesema kuwa hiyo ni thamani ya nguo zako tu ama Khalifa hana thamani yoyote!"