Bahlul na harun kwenda kuoga pamoja

KABAVAKO

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2011
Posts
229
Reaction score
32
Ilitokea siku moja Bahlul na Harun Rashid kukutana katika bafu. Khalifa alimfanyia mzaha kumwuliza Bahlul: "Je iwapo ningalikuwa mtumwa, ningalikuwa na thamani gani?" Bahlul alimjibu: "Dinar hamsini." Harun Rashid katika kughadhabika alisema: "Ewe Mwehu! itawezekanaje hivyo? Mavazi yangu tu yamezidi thamani hiyo!” Hapo Bahlul alimwambia: "Kwa hakika mimi nimesema kuwa hiyo ni thamani ya nguo zako tu ama Khalifa hana thamani yoyote!"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…