Mi navyoelewa kwanza samahani katika kukujibu sitatumia maneno uliyotoa, nianze na neno ainisha, hapa maana yake ni kueleza ama kutoa aina ikiwa ni aina za maneno tungo, virai, vishazi nk mf. Ainisha vishazi katika sentensi hii; Ng'ombe aliyevunjika mguu amekufa. Hapa tungo -aliyevunjika mguu ni kishazi tegemezi na Ng'ombe amekufa ni kishazi huru hapo nimeainisha. Tukija sasa kubainisha navyoelewa mimi ni kuweka kitu bayana, kufichua mf. Bainisha aina ya maneno yaliyoandikwa kwa herufi kubwa, BABA YANGU alinunua BAISKELI nzuri, kwahiyo BABA-jina au nomino, YANGU-kivumishi,BAISKELI-nomino, nadhani utanielewa nakaribisha changamoto au maboresho