Tetesi: Bajaji & bodaboda Authority inahitajika?

Tetesi: Bajaji & bodaboda Authority inahitajika?

Tabutupu

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2010
Posts
13,206
Reaction score
18,549
Kwa kuwa latra wameshindwa kusimamia bajaji na bodaboda japo wanawapa leseni, kuna uhumuhimu wa kuwa na chombo cha kudimamia hawa vijana maana wasipo simamiwa na janga la taifa.


Bajaji na bodaboda wanafanya kazi nzuri sana hasa maeneo ambayo mabasi na usafiri mwingine haufiki. Pia wanafanya kazi 24 hours.

Tatizo ni kwamba hawana ruti na ssa hivi hawana utaratibu. Badala ya kukaa kwenye vijiwe vyao kama zamani sasa hivi wanajazana kwenye zebra crossing kuvizia abiria hadi inakuwa kero kwa wapita kwa miguu na vyombo vingine.

Kama wameruhusiwe kufanya kazi kama public transport wapewe TLB kama daladala na kila bajaji iwe na ruti yake ili wawe na mipaka.

Bajaji na bodaboda zinakwenda kuua BRT pamoja na daladala, kitu ambacho kitaleta kero kwenye baadhi ya miji mikubwa.

Bajaji na bodaboda zinataliwa zibaki kwenye maeneo ambayo hakuna TLB ya latra na pia kwa kukodishwa na siyo inavyo fanyika sasa.

Chombo kipya cha kusimamia bajaji na bodaboda kitasaidia sana kulinda ajira za hawa vijana lakini pia kwa ustawi wa miji yetu ambayo serikali inawekeza ili kuifanya iwe morden na yenye usalama zaidi.
 
Sisi wapita kwa miguu mbona hatujalalamika mkuu vijana wanatusaidia wanakufuta mpaka ulipo ..........Uza costaa yako nunua bajaji mkuu life ni simple usi complicate
 
Boda na madereva bajaji wasiguswe mbaka itakapopatikana katiba mpya Mkuu Wazo lako ni zuri ila kwa sasa litakua shida kwa maana uhuru / haki vitapotea tu kwa awo jamaa ambao pia ni watafutaji

Alafu nakushauri siku nyingine ujikite zaidi kwenye kutoa solution ambalo ata wewe ndio ungekua boda boda usingeona unafanyiwa vibaya mkuu kuliko kuleta riport au mikasa ya namna iyo uliyoleta yawezekana kwako imekua kero ila kundi kubwa la watu wanaona poa kwa maana ni msaada kwao

Namaliza pambania katiba bro /mengine yatakua mepesi sana kwenye ili taifa

Note: sijakwambia uwe mpinzani ila katiba mpya ni muhimu kwa vizazi vyote .
 
Back
Top Bottom