Bajeti inayothibitisha azma ya kuwa na Tanzania ya viwanda na taifa linalojitegemea

Bajeti inayothibitisha azma ya kuwa na Tanzania ya viwanda na taifa linalojitegemea

Environmental Security

Senior Member
Joined
May 21, 2020
Posts
181
Reaction score
261
Habari wanaJF,

Sina shaka na weledi wa wanaJF wengi humu jamvini, ndio maana nina ujasiri wa kuleta thread hii njema kabisa kwa mustakabali wa taifa letu.

Tukiondoa tofauti zetu za kiitikadi na kuja pamoja kama taifa tutatambua kuwa kwakweli bajeti hii ya 20/21, imelenga moja kwa moja kulifanya taifa letu kuwa la uchumi wa viwanda, taifa linalojitegemea kiuchumi (katika hili utaona jinsi ambavyo serikali imewekeza katika kuimarisha vyanzo vya mapato pamoja na kuimarisha sana ukusanyaji na udhibiti wa mapato yote ya serikali eg; mapato ya TANAPA, NCAA &TAWA) lakini pia bajeti imejikita katika kutengeneza mazingira rafiki kwa wawekezaji wa ndani na wa nje wanaotaka kuwekeza mitaji yao katika taifa hili linalokua kwa kasi kiuchumi hapa utaona tozo na ada mbalimbali zimepunguzwa na nyingine zimefutwa kabisa, ni bajeti ambayo imegusa kwa uhalisia sio kwa kucopy na kupaste, imegusa kila eneo la kimkakati kwa kukuza uchumi wa taifa letu, hakuna eneo ambalo limeachwa bila kuwa addressed ili taifa liweze kusonga mbele katika sekta zote.

Ni vema sisi waTanzania kukumbuka kuwa tumebakiwa na miaka 5 tu ili kuhakikisha tunatimiza malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2000-2025, ambayo kwa kupitia bajeti hii unaona dhamira ya kweli ya kuifikia na kasi inayotakiwa, sio kupanga mambo bila kutekeleza au unayasahau unadakia mengine.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu mbariki Rais wetu Magufuli na kila mTanzania anaelitakia meme taifa letu hili.

CCM imara
 
Back
Top Bottom