Let Think BIG.
Msafara wa Waziri Mkuu utakuwa na haya yafuatayo:-
1. Gari ya Mheshimiwa Waziri Mkuu
2. Gari ya Wanausalama
3. Gari lingine la wanausalama
4. Gari la RPC
5. Gari la RC
6. Gari la DC
7. Gari la OCD
8. Gari la Mkugurugenzi wa Halimashauri
9. Gari/Magari ya Wabunge wa Mkoa/Jimbo husika
10. Gari la Polisi
11. Ambulance
12.
13,
Sasa ukisoma hapo utaona kwamba tunaongea upuuzi tu na sisi kwa maana wa could do better kwa kuongelea mambo mengine ya maana!
Let's think SMALL.
Gari la Wasaidizi wa Waziri Mkuu limesahaulika kwenye orodha au wanajumulishwa kwenye magari ya wana usalama?
Msafara huu wa:
Gari 4: 2 za Wanausalama, moja ya polisi, 1 Ambulance.
Gari 2 zingetosha.
Ni vigumu kuelewa ni kazi gani inahitaji kufanywa na wanausalama walio kwenye magari mawili. Kama kuna tishio ama wasiwasi wa majangili kujaribu kuuteka nyara msafara wa kiongozi ni bora viongozi wetu wakifanya ziara mikoani wapande helikopta. Chopper itaweza kubeba kiongozi mwenyewe, walinzi wawili, msaidizi mmoja. Kwa maana hiyo kutakuwa hakuna ulazima wowote wa kusindikizwa na hao akina RC, DC, RPC, OCD etc wa mkoa anaotoka. Viongozi wa Mkoa anakokwenda, watampokea atakakotua.
Kama kuna ulazima wa kwenda na magari na kuandamana na hao wote.
Je, RC na DC hawawezi kupanda gari moja, kwa nini?
Kuna mwiko gani RPC na OCD kutumia gari moja?
Mkurugenzi wa Halmashauri naye apande gari la Gari na Mbunge/Wabunge.
Kinacholalamikiwa ni matumizi yasiyo ya lazima ya magari, gharama za mafuta n.k. kutokana na wingi wa magari katika msafara wa Waziri Mkuu. Kwa nini kila msindikizaji awe na gari lake? Twataka ufahari katika nchi maskini?