Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Watanzania wengi vijijini wanalipa fedha nyingi zaidi kununua nishati ya mafuta, ambayo pia sio safi na salama. Kutibu kadhia hiyo, Serikali imebuni mradi wa uwezeshaji na uendelezaji wa vituo vidogo vya bidhaa za petroli kwa maeneo ya vijijini ambayo hayana vituo vya mafuta kwa njia ya mkopo nafuu. Mradi huu ni mpya na kazi zitakazotekelezwa ni pamoja na kuandaa wigo wa mradi, kutangaza zabuni na kuwapata waendelezaji wadogo wadogo wa vituo vya mafuta vijijini ili kuanza ujenzi wa vituo hivyo.
Uanzishwaji wa Ukanda maalum wa Uchumi.
Serikali ina mpango wa kuanzisha Ukanda Maalum wa Kiuchumi (Special Economic Zone) katika eneo la mradi wa LNG - Lindi, ambapo maeneo yatatengwa na kuendelezwa kwa ajili ya uwekezaji, uzalishaji na biashara. Hatua hii, pamoja na kuimarisha shughuli za kiuchumi wakati wa utekelezaji wa mradi, pia itawezesha manufaa ya mradi kuendelea kupatikana hata baada ya ukomo wake.
:Hifadhi ya Kimkakati ya Mafuta
Uanzishwaji wa Hifadhi ya Kimkakati ya Mafuta (Strategic Petroleum Reserve - SPR) unahusisha uratibu wa uagizaji, uhifadhi na usambazaji wa bidhaa za mafuta kwa kipindi mahsusi. Uanzishwaji wa SPR ni muhimu ili kuwezesha usalama na uhakika wa usambazaji mafuta nchini wakati wote. Ushiriki wa Serikali katika kuwezesha kuwepo kwa SPR utawezesha nchi kuwa na akiba ya mafuta muda wote na kuwezesha shughuli za uchumi kutoathiriwa na matukio yanayovuruga mwenendo wa bei za mafuta.
#DiraMpyaNishati