Hata hivyo, hoja hizo zilipingwa na wabunge wawili ambao ni Dk Omari Mzeru (Morogoro Mjini-CCM) na Dk Abdallah Kigoda (Handeni-CCM), ambaye ni mwenyekiti wa kamati hiyo ya fedha na uchumi.
Dk Mzeru alifafanua kwamba hakuna mantiki watu kuhoji ujenzi wa barabara ya Msata-Bagamoyo wakati ndiko anatoka Rais Kikwete, ambaye anapaswa kupita katika barabara salama yenye lami.
Kwa mujibu wa Dk Mzeru, hajaona duniani sehemu ambako wananchi hawathamini heshima ya rais wao na kuongeza kuwa eneo hilo ni la kiuchumi kwani litafungua utalii.
.
Mzalendohalisi,It is high time mashirika ya dini yalipe kodi!
Maaskofu wanaishi maisha ya kifahari na mashangingi ya nguvu kama mawaziri..ni kwa nini wasamehewe kodi!
Wote walipe kodi!
Hizo hospitali na shule wanaweza kuomba ruzuku ya serikali..ila kodi walipe!
Ya Kairasi mpeni Kaisari!!!
It is high time mashirika ya dini yalipe kodi!
Maaskofu wanaishi maisha ya kifahari na mashangingi ya nguvu kama mawaziri..ni kwa nini wasamehewe kodi!
Wote walipe kodi!
Hizo hospitali na shule wanaweza kuomba ruzuku ya serikali..ila kodi walipe!
Ya Kairasi mpeni Kaisari!!!
Kama kawa TBL TCC cocacola na viwanda vya spirits jiandaeni na bonge la kodi. Ila mjua hata mpandishe Kodi vipi Bia hatuachi. Kuna maeneo mengi sana y akupata mapato ila serikali haiko creative. Hivi nchi hii kuna TUME YA MIPANGO?
ndio maana kuna umuhimu wa kuwa na utaratibu wa kuteua mawaziri nje ya bunge. mbunge anapokuwa waziri, anakosa ule uhuru wa kuisimamia serikalikwa sababu na yeye anakuwa sehemu ya serikali anayotakiwa kuisimamia.Hili ndiyo moja wapo la tatizo la waziri kuwa mbunge pia. Waziri yoyte ata taka afanye walau kitu cha maana jimboni mwake ili apate cha kusema wakati wa kuomba kura.
Bajeti itazingatia zaidi uchaguzi mkuu ujao. Mengine yote ni baadaye.
Kulipisha mashirika ya kidini kodi ni kosa. Tusiharibu. Uwadai kodi kisha uwape ruzuku? Huo ni mpira usio na magoli.
Kuna Askofu na Askofu. Wako watu wengi wamejipachika cheo cha Askofu wenyewe. Hao wadai kodi. Lakini mtu aliyeteuliwa kwa namna zinazofahamika na kukubalika kuwa Askofu, apewe heshima yake. Kwa mfano, Askofu wa Kikatoliki ana fedha za Kanisa, sio fedha zake. Ni fedha anazotumia kusomesha watoto wako, na kukutibu unapougua. Utamdai kodi ya pato lipi? Utamwambia achukue baadhi ya fedha za kuwalipa waalimu wa Marian College akulipe kodi? Si utaonekana ni ngumbaru wa kutupwa?
Mzalendohalisi,
Are you serious? Atakayeumia ni nani? Serikali itakusanya kodi ya kiasi gani kwa maaskofu? Na kama serikali imeshindwa kutoa mikopo kwa wanafunzi wachache wa vyuo vikuu wataweza kutoa ruzuku ya kutosha kuendesha mahospitali na mashule yanayoendeshwa na mashirika ya dini. Mashirika ya dini yatozwe kodi kwa kupeleka miradi ya maji vijijini? Fikiria tena!
Hilo muulize "mchapakazi" Magufuli
I would say perfect reason. The right time is now. At least to the MPsBasi tuangalie ramani ya Tanzania. Kuna Barabara ya lami inayotaka kujengwa kutoka Handeni kupitia Kilosa, Mikumi, mpaka Iringa. Barabara hiyo inapita jimboni kwa Mkullo, lakini inapita majimbo mengi. Lakini vile vile sehemu ya barabara muhimu kwa sababu itarahisisha usafiri.
Barabara kubwa iliyopo Bagamoyo ni ya kutoka DSM kwenda Morogoro na Arusha. Hii barabara ni kiungo muhimu kwa taifa. Kwa barabara hii pesa nyingi ni lazima zitengwe tu. Kwanza ilitakiwa kuwa 4 lane.
Diallo anatakiwa kutuonyesha ni barabara gani maana barabara zingine ni muhimu kwa taifa.
Na kama kulivunja bunge, richmonduli was a perfect timing.
Ni kweli Mkuu Magufuri knows the answer,
Lakini kama ulisha wahi pita barabara ya Tabora kwenda Kigoma.. ambayo kimsingi ni muhimu sana kwani inauunga mkoa wa Kigoma kwa sehemu nyingine hivyo kuharakisha maendeleo yake,
I mean kama umepita huko hasa wakati wa mvua, leo hii ukaja ona mabilioni yanatengwa eti kutengeneza barabara kama ya msata and whatever.. haingii akilini kabisa! Huu ni uhuni na ubinafsi wa hali ya juu!
Na sidhani kwamba ni busara kuipendelea sehemu moja ya nchi wakazi wake wapate maisha mazuri ili hali wengine ni fukara wa kutupwa! Wakati kodi unazifata huko huko kwa mafukara hao bila huruma.
Tuliona pia wakati wa Mramba barabara za lami zikapelekwa Rombo kule Kilimanjaro!
Je sasa ni wakati wa upendeleo Kilosa kwa Mkulo??
Pia nimepita Chalize- shirika la nyumba limejenga nyumba ya gorofa kule tena porini kabisa kuelekea Moro: na hakuna hata mtu anaishi pale (White elephant!). Sii utumiaji mbaya wa pesa za Watz? Why Chalinze kule porini???
Sasa kama kila mtu anavutia kwake- maeneo yasiyo na mawaziri itakuwaje?
Hatuwezi kuiga hata kidogo msimamo wa mwal. Nyerere kutopendelea Musoma?