Tuandamane
JF-Expert Member
- Feb 2, 2008
- 1,221
- 55
Date::6/8/2009
Bunge la bajeti lafupishwa Kikwete kuhutubia wazee, wabunge
Wakati ratiba hiyo ikionyesha idadi ya siku za vikao hivyo kupungua kesho Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwahutubia wabunge wote na wazee wa mkoa wa Dodoma katika ukumbi wa Kilimani mjini hapa baada ya kipindi cha maswali na majibu.
Kweli hapa kazi ipo. naona Sasa JK anataka kuwamaliza kimya kimya
kama ningekuwa mbunge ningepiga usingizi wakati jamaa anaongea ujinga!!
Ah wabunge wetu wanashangaza kila siku, eti saivi 2010 inakaribia wanajifanya wanaumwa na majimbo yao. pretenders!!
Asalaam Aleykum, Bwana Asifiwe.
Wakati wowote kuanzia sasa, Rais Jakaya Kikwete, atalihutubia taifa kutokea ukumbi wa Kilimani hapa mjini Dodoma.
Hotuba hiyo itatangazwa moja kwa moja na TBC Taifa, TBC One na Star TV. ITV pia watajiunga kupitia Star TV, Channel Ten na TV watajiunga kupitia TBC-1.
Mpaka sasa ukumbi wa Kilimani umefurika, mpaka watu wengine imebidi wabaki nje, kundi kubwa la watu ni wana CCM ambao wamevalia sare unaweza fikiri ni mkutano wa Chama.
Waheshimiwa wabunge, wamekuja karibu wote hali inayoashiria kulitolewa kama kaji amri fulani lazima wawepo.
Makamo wa Rais na Waziri Mkuu pia watakuwepo.