Bajeti ya 2024 - Nyongeza ya kima cha chini cha Pensheni ni takwa muhimu kwa wastaafu Tanzania

Bajeti ya 2024 - Nyongeza ya kima cha chini cha Pensheni ni takwa muhimu kwa wastaafu Tanzania

danimutta

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2011
Posts
273
Reaction score
351
Tangu July, 2015 wakati wa utawala wa Rais Kikwete kima cha chini cha Pensheni za wastaafu hakijawahi kuongezwa kutoka Tsh. 100,000/=.

Tokea 2023 Waziri Mwigulu amekuwa akiongelea zoezi la mapitio ya mifuko ya pensheni na kuwapa matumaini kwamba jambo hili linafanyiwa kazi lkn tumeona juzi akisoma Bajeti bila kugusia kima cha chini cha pensheni ambacho ni sawa na USD. 28!

Hali hii ni lazima iwe aibu kwa Waziri Mwingulu. Iliwezekana kama siyo busara na hekima Mama Sada Mkuya akiwa Waziri wa Fedha aliweza kuwaongezea wataafu pensheni kutoka tsh.50,000 hadi 100,000 zaidi ya miaka 8 sasa?

Hili boresho la kokotoo kutokana agizo la Rais Samia ni sawa na serikali kutatua mgogoro iliyosababisha yenyewe kutokana na matumizi mabaya ya pesa za mifuko ya pensheni.

Waziri Mwigulu bado hujachelewa - to do the right thing. Kama Waziri wa Fedha 2015 aliweza kuongeza kima cha chini cha pensheni kwa wastaafu na wewe pia 2024 unaweza kufanya hivyo.
 
Serikali inatengeneza tatizo alafu inalirekebisha kidogo kisha inakuwa eti ndiyo point ya kujisifia majukwaani😂😂 na mazuzu yanashangilia!!!

Hatajana kunamijinga iligonga meza saana kushangilia!!! SHAME!

**Nchi hii tunashida kichwani kwakweli kuendelea ningumu mmno!

Kunakipindi wastaafu waliwekewa pensheni iliyozidi na kutakiwa kilichozidi wakikabidhi kwa maafisa flani utashangaa takukuru hawayajui haya mpaka mfuko unafilisika kabisa!!
Makonda apelekwe takukuru huko anapenda mapambano angekabidhiwa tuu takukuru sio eti wanajeshi ambayo hawana utendaji wowote wamaana taasisi zinakufa sio psssf,NHIF,tanapa,etc.

Mfano uchafu unaofanyika chama Cha walimu CWT hatakipofu anaona lkn etii takukuru hawaoni??!!?!😏😏
 
Back
Top Bottom