In about 2 days Kinana anazungumza kwamba kama Chadema itatekeleza suala la elimu bure basi hiyo itakuwa sawa na 70% ya bajeti ya serikali as of now. Wakuu are we that poor? Au takwimu hizi zimechakachuliwa kama kawaida yao akina kinana, CCM and the apologists.
Lets do a bit of a homework:
Bajeti as of current ni 11 trillion Tshs. 70% ya hiyo ni kama 7.70trilioni Tshs. Ok tukija kwenye suala zima la uchangiaji wa elimu, I believe more than 90% ni kutoka elimu ya juu.
Tunaambiwa kwamba tuna wanafunzi elimu ya juu about 100,000. Lakini I am sure wanaolipiwa na serikali kwa asilimia 100 hawafiki 50%. Let us assume all 100,000 wanalipiwa na serikali kama CHADEMA inavyosuggest. At about 3,500,000 average kama ada ya elimu ya juu kwa mwaka unapata Total of 350 billioni Tshs. Does this represent anything near 70% of the budget???????????
350billion Tshs is just about some 5% of 7.7trillionTshs ok say 10% uki include na ada za vijana wa sekondari, hiyo 70 % inatokea wapi???????
Na je Kinana anaamini vyanzo vya mapato vya serikali vitaendelea kuwa vilevile traditional yaani bia, sigara, soda, PAYE, VAT???????
Nna wasiwasi na takwimu hizi za kinana, CHADEMA mnaweza kufuatilia hizo heasabu za CCM tuziasses kama hazikuchakachuliwa?????????????
Nawasilisha!!!!
Wala Nyambala usitie shaka, hesabu hao Fisi Wenu (Nyie emu) hawazijui. Ikiwa gharama ya kusomesha watoto wote wa Tanzania ni TZS trillioni 7.7 wao wanafanyaje? Ukisoma bajeti ya serikali ya Fisi Wenu 2010 hadi 2011 wanaeleza kuwa "Elimu imetengewa shilingi 2,045.3 bilioni" sawa na trilioni 2.045. Ikiwa elimu inagharimu hizo trilioni 7.7 kama kilaza Kinana anavyotaka Watanzania wamuamini kabisa basi ili kufikia mahitaji kamili ya elimu ina maana kuwa Watanzania baada ya kuichangia serikali kwa kodi na ada mbalimbali, wanaichangia elimu tena kwa shilingi trilioni 5.7 (nusu nzima ya bajeti ya serikali ya mwaka 2010/11).
Ukichukulia kuwa kuna wanafunzi milioni kumi kutoka chekechea hadi vyuo vikuu, basi kila mmoja kwa wastani anachangiwa shilingi 570,000/=. Hii ni ziada ya fedha zinazotolewa na serikali (trilioni 2.045). Huu ni uwongo uliokithiri. Tuna kila sababu ya kuukataa uwongo na uzandiki huu.
Tujiulize tu kama kweli kila mwanafunzi kwa wastani Watanzania tunamchangia kiasi hicho cha fedha?
Msingi wa hesabu zilizofanyika hapo ni kuwa mwaka huu wanafunzi wanaokadiriwa kufika laki tisa wamefanya mtihani wa darasa la saba. Huwa wanapungua wanapoenda sekondari na wanapungua zaidi vyuo vikuu (ambapo mwaka huu wanakwenda wanafunzi 35 alufu). Kwa hiyo utaona kuwa nimetumia wastani wa juu kwelikweli wa wanafunzi milioni kumi. Ukweli ni kuwa kuna wanafunzi pungufu ya hao.Ikiwa na maana kuwa ili kufikia hesabu batili za Kinana mchango kwa kila mwanafunzi unazidi hapo.
Kama kweli Kinana ana hakika ya hesabu alizofanya atueleze ni vipi watanzania (wazazi/ walezi na watu wazima wenyewe) wanaweza kuwekeza trilioni 5.7 kwenye elimu na serikali yao itumie trilioni 2? Nini ilikuwa msingi wa hesabu zake huyu kilaza Kinana. Bila shaka baada ya kutoa elimu duni ya kuchakachua kwa miaka 49 wanaamini kuwa hakuna awezaye kuuona uwongo wao kama walivyofanya kwenye mishahara ya wafanyakazi kwa kuwaaminisha watu kuwa ukiongeza kima cha chini mara tatu basi mishahara ngazi zote inapanda mara tatu. Yaani hata wale washauri wa mkulu wao wanaonyaka US$ elfu kumi basi wataongeaewa mara tatu. Katika hali halisi haifanyiki hivyo. Kwa kawaida asilimia ya ongezeko inapungua kadri ngazi ya mshara inavyoongezeka.
Kinana na wapinzani wote wa mfumo wa kutoa elimu bure wanapaswa kupuuzwa hasa baada ya wao wenyewe kusomeshwa bure (kwa kodi za wananchi).
Swala lingine katika mjadala huu ni ukweli kuwa wazee wetu walitafuta uhuru kwa malengo ya kupambana na maadui watatu: Ujinga, maradhi na umasikini. Mwalimu wangu aliwahi kunieleza kuwa ukiwa na afya na elimu basi umepata silaha ya kupambana na adui umasikini. Hivi maana ya adui Kinana na vilaza wenzake wanaijua? Wakumbuke jinsi tulivyowachukulia makaburu enzi zile kama adui au nduli Idd Amini. Inabidi utumie nguvu zako zote unapopambana na adui kama kweli umepania kumshinda. Kutoa elimu na matibabu bila malipo kwa kila Mtanzania ni njia sahihi ya kuwatokomeza maadui ujinga na maradhi. Ni Watanzania wangapi ambao wanapoteza maisha yao kwa kushindwa kulipia matibabu katika nchi hii? Wangapi leo maisha yao yameharibika au yamekwama kwa kushindwa kulipa ada za kuendelea na masomo? Hata kwenye ngazi ya vyuo vikuu bado kuna watu wanashindwa kulipa sehemu ya ada ambayo hawapewi mkopo. Hivi hawa Fisi Wenu wako Tanzania kweli? Au ndio Watanzania waliopata maisha bora?
Maana kuna mheshiwa mmoja mingoni mwao, aliwahi kuniambai kuwa unadai maisha bora kwa kila Mtanzania kwani wewe ni Mtanzania? Nikajidai kujibu ndiyo. Akauliza kama nina cheti cha kuzaliwa, nikamwambaia sina, akauliza kama nina pasi ya kusafiria, hapana, akauliza kama ninaisha maeneo yaliyopimwa, jibu langu la. Akanieleza kuwa mimi si miongoni mwa Watanzania ambao walilengwa na kauli ile. Nilishia kucheka, lakini meseji ilifika.
Elimu na Matibabu bila malipo inawezekana. Anayetaka kupanga ikulu kwa miaka mitano ambaye hayo yamemshinda, ajitoe mapema!
Dawa ya mjinga ni kuumia