Kwakua haujawahi kupika. Ngoja nikupe tips:
1. Anza kununua vitu cheapest kwanza uone kama utaweza. Usiamze na mbwembwe za kununua jiko la oven, plate 4, au mtungi mkubwa.
2. Achana na appliances za umeme kama microwave, rice cooker, pressure cooker, brenda etc hivyo utanunua ukiona kupika iko damuni.
By experience niliamua kama ww nikanunua pressure cooker, rice cooker, Sufuria non-stick etc nimevipark nakula kwa mama ntilie.
Ukitaka kununua kabisa electric appliances basi rice cooker instosha kabisa. Inapika hadi ugali.
3. Lengo la mtoto wa kiume kujipikia ni either kusave hela (gharama) au kula vizuri na salama. Kwahiyo akikisha unapika vyakula ambavyo ngumu kuvipata kiurahisi usije anza tena kupika chips.
4. Usinunue unga robo, mchele robo.. Nunua atleast kilo 2 kwenda mbele. Utasave zaidi. Mafuta usinunue ya kupima, ishi na atleast lita 1. Pia nunua makontena ya kuwekea vitu kama unga, mchele, sukari usiache kwenye mfuko utaharibika.
5. Hauhitaji vyombo vingi. Vijiko viwili tu, vikombe viwili, sahani 2, bakuri 2 etc tosha kabisa. Haulishi taasisi.
Na Mwisho kabisa:
UKIPIKA, UKIMALIZA TU KULA OSHA VYOMBO. USISEME NGOJA NIPUMZIKE KIDOGO. USIJARIBU. KAMA HAUWEZI HII BASI KUPIKA WEWE BADO.