Bajeti ya kuleta mageuzi sekta ya elimu yapita kwa kishindo

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
BAJETI YA KULETA MAGEUZI SEKTA YA ELIMU YAPITA KWA KISHINDO

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania laidhinisha zaidi ya shilingi Trilioni 1.97 zilizoombwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa ajili ya kutekeleza vipaumbele vitano vya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 ili kuleta mageuzi ya Elimu nchini.

Vipaumbele hivyo ni pamoja na;

(i) Kuendelea na utekelezaji wa sera na mitaala, mapitio ya sheria na kuandaa miongozo ya utoaji elimu na mafunzo nchini

(ii) Kuongeza fursa na kuimarisha ubora wa elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi (amali na amali sanifu).

(iii) Kuongeza fursa na kuimarisha ubora wa elimu ya msingi, sekondari na ualimu.

(iv) Kuongeza fursa na kuimarisha ubora wa elimu ya juu na kuendeleza tafiti, matumizi ya sayansi, teknolojia na ubunifu.

(V) Kuendelea na utekelezaji wa Sera na Mitaala, Mapitio ya Sheria na kuandaa Miongozo ya Utoaji Elimu na Mafunzo Nchini.

Mwelekeo wa Wizara ya Elimu kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 ni kuweka mkazo kwenye Elimu ya Ujuzi (Skillis Oriented) ili kuwawezesha wahitimu wa ngazi mbalimbali za Elimu kujiajiri na kuajiri wengine.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…