Bajeti ya Serikali 2008/09 - Exclusive Thread


Thanks Insurgent!! This is exactly what i wanted to say and it's what Azimio asked above.... good thing we've brainy and willing JF members to put it into perspective....

....i now can say, the closet is wide open!!!

SteveD.
 
Ni habari nzuri but its strange...Ghafla hayo yanawezekana?

Swali ni .... nini hasa kimepelekea hayo kuwezekana?

Mipango na strategies nzuri yote yanawezekana.Pia support kutoka kwa wananchi
mimi nafikiri mtu/kiongozi anapokuja na mawazo/mipango safi inabidi tumuunge kwa fikra na mbinu za kumtia nguvu ili yafanikiwe mawazo yake na si kum diskareji kwa vidonda.

Vidonda tuvikumbushe wakati anapoongelea swala muafaka
 
Kwa taarifa tu wakuu ni kuwa ile bajeti ilizotangazwa kwa mbwembwe ya mwaka wa fedha 2006/7, mwaka ulipita bila fedha zilizokusudiwa kutolewa kwa baadhi ya idara kwa matumizi yaliyokusudiwa, angalao kwa idara chache ambazo nina access nazo. Sitashangaa nikisikia kuwa ni majority ya idara zilikumbwa na zahama ya "kutotimiziwa", yaani mnashiriki kuandaa bajeti pamoja na waziri, inasomwa bungeni na inapita, mnahakikishiwa zitapatikana fedha kwa matumizi mliyoainisha, lakini mwaka unaisha bila fedha hizo kupatikana! Mwaka 2007/08 ikasomwa tena bajeti "nene" kuliko mwaka uliotangulia, watu wakawa wanajiuliza yale ya mwaka jana yalitushinda, mwaka huu yatawezekanaje, au kitakuwa kibarua kilekile cha "carry forward" hadi kiama? Na sasa Mkullo anatuletea usanii wa "kujitegemea", miaka 2 iliyopita tukiwa na wafadhili bado "tuliahirisha" mengi tu, sasa katika "kujitegemea" utalipa mishahara (kichele) tu na yatakayobaki yote tusubirie miujiza ya Subhanna! Huu usanii wa kusomeana bajeti "nzuri" zinazopendeza machoni ili mpigiwe makofi tu utaisha lini?

Wakuu mkitaka kupata picha ya ninachokisema hapa, sasa hivi ni miezi 2 tu imebakia mwaka wa fedha kumalizika, hebu fuatilieni muone katika zile trilioni 3.8 zilizotengwa kwa matumizi ya kawaida kwa mwaka huu ni kiasi gani kimeshapelekwa kunakohusika! Mtashangaa sana. Wakati wa Mkapa serikali ilikuwa na hela nyingi, lakini bado kulikuwa na uzembe wa kulundika hela nyingi za bajeti kwenye mwezi wa mwisho wa mwaka wa fedha, basi kipindi hicho maafisa wa serikali hawapatikani kabisa maofisini, wako busy wanamalizia bajeti la sivyo hela itarudishwa hazina! Ulizia bajeti inamaliziwaje, mbona utachoka! Ni safari zisizoisha Morogoro, Dodoma, Bagamoyo kwenye warsha, semina, kongamano nk zisizo na mbele wala nyuma, za kulipana tu "posho". Wakati mwingine ofisa mmoja anaweza kushiriki "kongamano" hata tatu kwa muda huohuo, na zote analipwa full "posho", mtachoka msio na "vitengo"! Nasema maendeleo hayawezi kupatikana kwa njia hii.
 
Kithuku,

Mimi sina access na serikali na mahesabu yake kama wewe, lakini kwa hunch tu nilishawahi kusema several times hapa kuwa hizi budgets siziamini sana na sitashangaa kuwa ni kama michezo ya sarakasi tu kuwatuliza wananchi ambao wengi wao wakiona mi figure mingi inawaboa tu.

Sasa maandishi yako hapo juu mkuu yanaendelea ku validate fikira zangu.

Shukurani.
 
Hapo inabidi bongo kujitayalisha kufunga mikanda.Maana wasipo fanya kama wachangiaji wa budget wanavyotaka basi ndio hivyo itakavyokuwa.Wanashindwa kusema fungu la pesa za maendeleo kuna wasiwasi hazita kuwepo badala yake wanatumia lugha inayoonekana kuwa tamu kumbe siyo pesa za zitatoka kwetu wenyewe.Naona kuna wajumbe wamelichambua hili vema tu.Shukrani kwao!
 
Hakuna kisichowezekana....maadamu nia ikiwepo na mikakati madhubuti.........lakini nachelea kusema yaani Mkullo huyu huyu tunayemfahamu ndiye anasema maneno haya..........haya bana.......kwa sasa yangu macho!
 
Hakuna kisichowezekana....maadamu nia ikiwepo na mikakati madhubuti.........lakini nachelea kusema yaani Mkullo huyu huyu tunayemfahamu ndiye anasema maneno haya..........haya bana.......kwa sasa yangu macho!

yawezekana kaamua kubadirika yote yawezekana.
Mkumullo pekee hawezi fanikinisha bila ushirikiano na wananchi pia wafanyakazi.

Yawezekana wafanyakazi wakawa hawatii presha kuomba fedha za bajeti yao kitu kinachotoa taswira ya kua hawakua na vipau mbele ktk uandishi wa bajeti yao zaidi ya kuindika bajeti hiyo ili kutimiza wajibu tu.

Mimi bado naamini tukiamua tunaweza
 

Mtu mzima, you hit the nail on the head! Tutasema mengi lakini kiini cha maneno yote ya Mkullo ni hii: wafahdili sasa hivi wamesema hawako tayari kutoa misaada mpaka hapo watakaporidhika na Richmond na EPA, hususan hii ya EPA ndo bomu sana! Sasa nawaambia tukae hapa tukiwapongeza wasanii hawa lakini tujue kwamba mwaka 2008/2009 itakuwa chungu sana na mambo mengi sana yatasimama. Mtakuja kuniambia.
Mkullo anajihami tu mapema! Ili wananchi wasije wakashtukia kwamba tatizo ni EPA! Mi naomba tuendelee kuanika ukweli hapa na si kuleta propaganda za kupongeza serikali. Serikali hii imechemka vibaya SANA na uchumi utaendelea kushuka, worse hakuna strategy yoyote ya kuokoa uchumi. Ukusanyaji wa kodi hauwezi kuongeza kwa asbabu kila kampuni sasa inasua and omney is drying up fast. Kwa hiyo ahadi zile za kupandisha mishahara ndo hivyo tena! Wanafunzi kupata mikopo ya kusoma ... sorry, mtaanza kuona dalili zote mpaka mshtuke mwaka 2010!
 
Nakubaliana na Maelezo ya Mtu Mzima, ni kwamba fedha za wafadhili zipo hazipo, so to be in the safe side, serekali wameamea angalau waiendeshe serekali kwa kulipa mishahara na stationery , hayo maendeleo tusubiri bahati nasibu.Sasa zile barabara zetu sijui itakuwaje
 
Wazee hii ni hadithi, haiwezekani kamwe, nadhani ni wale wafadhili, kale kamsimamo kao ndiko kanapelekea Tz kuanza kujihami, wanashindwa kushughulikia mambo yaliyopo, ooooooooooooo!!!!!hatari!!!
 
Sijui Mkullo kama anajipya katika hii ahadi,budget zinazopangwa bila utafiti na upembuzi yakinifu wa mahitaji na vyanzo vya mapato kwa serikali tutaishia pale mama Meghji alipotuachia,kupanga badhet na kuongeza hata kodi zisistahili na zilizo mzigo mkubwa kwa watanzania waliowengi ukiacha mafisadi...Mfano ni hii kodi itwayo Road licence iliyopandishwa toka TZS 20000.00 na kufikia zaidi ya laki tatu.HII HAIKUWA KODI BALI ILIKUWA ADHABU KWA WOTE WANOTAKA NA WANOMILIKI MAGARI
 
2008//09 budget around the corner: Mining sector up for major tax overhaul

- ’We could increase revenue from mining companies by 10 times if they all pay taxes’

- ’Cabinet will soon meet to discuss recommendations of the mining sector review committee chaired by Judge Mark Bomani’

- ’We need to change the current framework in which most mining companies operating in the country are exempted from payments including a 30 per cent corporate tax and customs duties’

THISDAY REPORTER & AGENCIES
Dar es Salaam

THE government is likely to make a major announcement in its 2008/09 budget proposals next month on key revisions to the country’s tax structure for mining companies.

’’We could increase revenue from mining companies by up to 10 times, if they all pay taxes,’’ Finance Minister Mustafa Mkulo said in an interview with the Bloomberg news agency yesterday, on the sidelines of the annual African Development Bank (AfDB) meeting in Maputo, Mozambique.

’’The (mining) companies agree that there are anomalies, and they are working with us. We are not going to chase any company away,’’ Mkulo added.

Mkulo is expected to unveil his maiden budget speech in June, after taking over the finance portfolio from Zakia Meghji in a Cabinet reshuffle by President Kikwete earlier this year.

President Kikwete has already declared that his government is seeking to create a ’’win-win’’ situation that would be mutually beneficial for both the country and multinational mining companies.

Mkulo said he hadn’t yet seen the recommendations from the mining sector review committee appointed by President Jakaya Kikwete to propose new royalties and taxes in the mining industry.

However, he confirmed that the committee?s much-anticipated report would soon be discussed by the Cabinet.

The committee, chaired by former attorney general Judge Mark Bomani, is understood to have already completed its work and expected to submit its report to President Kikwete soon.

Mkulo said Tanzania, Africa’s third-biggest gold producer, wants to benefit from record metal prices by boosting government revenue from mining to pay for more schools and hospitals.

He said the government needs to change the current framework in which most mining companies operating in the country are exempted from payments including a 30 per cent corporate tax and customs duties.

Gold mining companies in Tanzania currently pay royalties of three per cent on profit, while a five per cent royalty is levied on diamonds and gemstones.

Companies including Barrick Gold Corp., the world’s largest producer of the precious metal, and Tanzanite One Ltd, the only miner of the rare blue gem, operate in Tanzania.

Zambia, Africa’s biggest copper producer, increased the effective tax rate on mining firms to 47 per cent from 31 per cent this year by introducing a range of measures including windfall and variable-profit taxes.
 
Samahani wandugu nimeiweka hii haopa kwa sababu jukwaa la uchumi silioni.

Waziri Mkullo leoametangaza mwelekeo wa bajeti ya 2008/09. Itakuwa ya sh trilioni 7.126. Utegemezi utapungua kutoka asilimia 42 za mwaka unaoisha hadi asilimia 34.
Fedha zinazotengwa kwa sekta ya afya na miundombinu zimeongezwa wakati maji na kilimom zimepungua.
Makusanyo ya mapato ya ndani yatakuwa tr 4.7
Fungu la maendeleo litakuwa sh tr. 1.9
 

Hivi kweli hatuhitaji mapinduzi ya kilimo ili kujikwamua na janga la njaa linalotukabili? Je fedha za afya mara hii zimewekewa mkakati gani wa kutoishia wizarani walau aspirin na ALU zikapatikana kwenye zahanati....ILA MNISAMEHE siamini maneno ya Mkullo na mipango yao ya bajeti siiamini kabisa maana usikute katika bajeti hii, fungu la kuipigia debe bajeti kuwa ni nzuri pia limeshawekwa tayari.

Sikuwa PESSIMISTIC kiasi hiki, nimelazimika tu kwa mwenendo wa bejeti za awamu ya 4
 
Donor dependency sasa 34% kutoka 41% kwenye bajeti ya 2007 - 2008...

Nukuhu ya habari zaidi kutoka thisday:


Source link: http://www.thisday.co.tz/News/4114.html

SteveD.
 
Kumbe Tanzania Viongozi Wake Wote Wajinga Sana, Budget Yatrilion 7.2 Kwa Nchi Nzima Hii Sawa Na $7 Billion Ambayo Ni Sawa Mishahara Ya Kampuni Moja Ya Bp/ Or Exoon Mobor /siemens/or Walmart. Profit Ya Walmart Kwa Mwaka Ni $72 Billion Ambayo Ni Sawa Kuendesha Tanzania Yenye Madini Ya Dhahabu/almasi/maziwa/mbuga Za Wanyama/samaki/kilimo Kwa Miaka Kumi. Kumbe Mtu Ambaye Amezoeya Kuomba Omba Akili Zake Mara Nyingi Ni Finyu Sana. Viongozi Wetu Wamezoea Kuomba Omba Ndo Maana Badala Ya Kampuni Za Madini/coca/simu Zilipe Kodi Wanabaki Kuwa Omba Omba . Faida Ya Kikampuni Kimoja Kidogo Cha Marekani Kinaweza Kuendesha Nchi Yote Kwa Tanzania Bila Tatizo, Hao Wasomi Wa Ccm Wanafanya Nini Jamani: Mapinduzi Ni Lazima Kwa Damu Au ???
 
Walala hoi tutaendelea kukamuliwa ile mbaya ona mfano betri N70 mwaka mmoja uliopita ilikuwa inauzwa elfu 55 leo hii ni laki 130,000/= kisa kodi tutakamuliwa kufidia pengo la mafisadi na fedha zao za matumizi (maendeleo ziro)
 
Mimi sifahamu kama tanzania kuna bajeti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…