Bajeti ya serikali 2023/24. Yatakuwa maumivu au unafuu?

Mtu_Mzima

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2014
Posts
1,164
Reaction score
1,134
Imekuwa sasa ni kama kawaida nchi zetu kila kiongozi anapoingia madakani kuunda serikali ya ukubwa anaoutaka na kila mwaka kuongeza bajeti anavyotaka kwa kisingizio cha kuhudumia wananchi.

1. Hivi haiwekekani kuwepo na ukubwa wa serikali ( idadi ya wizara) kikatiba?
2. Idadi ya watumishi ( japo ceiling) wa serikali kuepuka kuajiri mpaka hewa?
3. Kikomo cha ongezeko la bajeti ya serikali ( ceiling) kwa mwaka badala ya mtindo wa sasa ongezeko la matrilioni kila mwaka?
4. Hizi ahadi za fedha na miradi zinazotolewa na viongozi baada ya bajeti kupita mbona hatuoni zikiletwa bungeni kujumuishwa na kuombea fedha? Si kulidharau bunge na sheria za fedha?
5. Misaada tunayoona inasainiwa katikati ya mwaka wa fedha, je, inapelekwa kwenye bajeti ijayo au inatumika nje ya bajeti kimyakimya? Si ingeletwa bungeni kujumuishwa kwenye bajeti?
6. Si wabunge wa chama tawala au upinzani wanaohoji matumizi ya serikali nje ya bajeti ?
Haya si ndio yanayotusababishia kodi kupanda kila mwaka kujaza tumbo la serikali linalopanuka kila mwaka?
 
Unategemea mapya kutoka miguu ya chemba?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…