Bajeti ya serikali imeshaanza mbona ajira kimya sasa

Bajeti ya serikali imeshaanza mbona ajira kimya sasa

Nyanda Banka

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2023
Posts
304
Reaction score
1,054
Mwaka mpya wa kiserikali umeshaanza, nadhani hapo nyuma tulishapokea shadi mbalimbali kutokana na suala la ajira hususani hizi za ualimu na afya lakini naona bado ubao umenuna

Mbona hili suala la ajira limekuwa kizungumkuti tunasubiria mpaka kichwa kinauma, jamani hawa wenye mamlaka ebu wajaribu kukumbuka zile ahadi zao tusije kuwa tunaishi kwenye nchi ya ahadi

Kweli kula kulamba lamba kushiba imani, tunaomba watoe ajira ili watu wapungue kusubiri mtaani, tena ikipendeza tuanze kupata sisi tunazozingoja kwa hamu
 
Ajira subiri ukifa zipo huku motoni tunaitaji watu watakao fanyia serikali ya motoni
 
Kuwa na amani,ila unauhakika utapata ? Mana unaweza sumbua humu ndani ajira zikatoka na ukakosa.
 
Kuwa na amani,ila unauhakika utapata ? Mana unaweza sumbua humu ndani ajira zikatoka na ukakosa.
Unakuta zilizoahidiwa 12300 saiz wanazigawana kabla hazijatangazwa Kwa ndugu zao na Koo zao Hadi ziishe wakihakikisha Kila ndugu Yao kapata ndo wanatangaza kama ushahidi 🤣
 
Jiongeze mkuu. Wenye digrii na dip wapo zaidi ya 300,000 wote wanawinda nafasi 50,000
 
Back
Top Bottom