BAJETI ya siku

BAJETI ya siku

Jr. Gong Mira

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2017
Posts
1,281
Reaction score
1,300
Mfano umeamka asubuhi pesa uliyobaki nayo ni shs 4,600. Huna pesa nyingine.
Panga BAJETI yako ya chakula kwa siku nzima.
cloudstv-20200212-0001.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
1000 Nauli kwenda na kurudi nyumbani
Chai nakunywa ofisini
3000 chakula na maji
600 akiba
 
buku nne mia sita! pesa ndefu sana iyo kwa madogo wa chuo, sana sana college za diploma hizi!
madogo wana bajeti za buku 2 kwa siku, alafu ile safii tu wanaishi
 
Nitakwenda kazini kwa mguu(kibishi)
1000 breakfast na lunch(usiulize maswali)
Usiku najua unga,mchele,tambi,viuongo na mboga vitakuwepo hivyo napika chakula changu cha usiku freeesh tu nakula nalala. Siku imeisha.
 
Inategemea hiyo siku nashinda wapi.
Niko job au jobless

Mchana nakula buku, usiku buku.
2000 vinywaji
Alafu 600 nafanya kumoka. Siku imeisha.
 
Kabadilishe upate 2 us dollars...Moja Nenda kwa mamantilie weka bili ya mwezi nyingine fanyia mambo mengine.... Kuna mamalishe aliniambia ukipata dola ww ni tajiri.
 
Nyingi hiyo asubuhi supu na chapati mbili 1500

3100 natumia ifuatavyo
Nanua njegere za 1000 mafuta kibaba 500 nyanya na kitunguu 600

Mchele nusu 1000 nakula mchana na jioni
Nb: source ya moto kama tayari ipo, kama sina nakula mgahawani tu hiyo hela inatosha sana.
 
Asubuhi unapiga nyutro,
mchana ugali na mchuzi kwa mama dogojanja tsh 700,inabaki 3900,
Usiku unapiga mchemsho wa ndizi na nyama 3500 pale kwa mpembaa cafe,
400 inayobaki unanunua matunda,
Hii ni bajeti ya baharia



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyingi Sana hiyo asubuhi chapati maharage 800
Mchana ugali wa buku jioni ndio siwazi unga niliosaga upo,mboga zipo,mafuta ya alizeti yapo, vitunguu nalima hapo labda naongezea Nazi ya pakti 800 na dagaa pakti moja la jero
 
Back
Top Bottom