Bakari Nondo Umepambana

Bakari Nondo Umepambana

redio

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2016
Posts
5,813
Reaction score
12,921
Captain Bakari Nondo Mwamnyeto nakupa maua Yako, Jana katika mechi dhidi ya Azam ulionyesha kitu kikubwa Sana na kwasasa Mimi binafsi naona unastahili Kuanza katika mechi upo tayari.
Jana ulicheza kama Kiongozi, mpambanaji , mfia timu licha yakua na shida kidogo katika ku kokota mpira na baadhi ya pasi ulipoteza ila ulifanya Kila lililo ndani ya uwezo wako kuipambania Yanga.

Sisemi wengine hawakupambana, hapana ila ulicheza kama Mwandamizi, Kuna muda sikuelewa unacheza namba ngapi maana ulishambulia, ulikaba, uli lazimisha na ulistahili kuwa Man of the match.

Nimefurahi kitasa kurudi katika ubora wako, wewe Bakari na Kibabage mmecheza kwa kiwango chajuu Cha kuipambania timu Asante ni Sana.
Naomba Kibwana Shomari asi Kate tamaa aangalie marudio ya hii mechi na Aanzie apo kurejesha ubora wake.

Kama ningekua na namba Yako ningekutumia zawadi , umeonyesha wewe ni mchezaji wa match kubwa
 
Mwamnyeto damu ya kunguni ingekuwa ile red card ni yake angetupiwa yeye zigo lote la lawama
Sasa Nime elewa aliye mchagua Mwamnyeto kuwa Captain alimaanisha Nini. Inahitaji Mapafu na brain viwe sawa kweli kweli.
Upo uwezekano Mwamnyeto Jana alikimbia 10km uwanjani.
 
Sasa Nime elewa aliye mchagua Mwamnyeto kuwa Captain alimaanisha Nini. Inahitaji Mapafu na brain viwe sawa kweli kweli.
Upo uwezekano Mwamnyeto Jana alikimbia 10km uwanjani.
Mwamnyeto ni beki mzuri sana Simba hawakuwa wajinga kutaka kumsajili.
 
Mwamnyeto ni beki Bora sana Jana kibabage angeanza Wala team isingepata shida
Mi nadhani Boka huwa anaanza kwa shinikizo la nje kocha ila uhalisia kibabage yuko vizuri kuliko Boka
 
Yote hayo yana maana gani ikiwa mlifungwa mkuu?
Kufungwa ni sehemu ya mchezo ila kama mwanayanga nimeunga mkono juhudi alizofanya kurudisha kiwango chake si jambo rahisi kwa mazingira ya kibongo.

Sisi mashabiki tumezoea kushutumu ila mchezaji anapofanya juhudi tunasahau kumpongeza.

Tunaelekea kwenye michezo ya kimataifa kunahitajika wachezaji wawe tayari kwa viwango vya namna Ile.
 
Naam Jana mwamba aliubonda Kuna muda alikua anakokota mpira hadi katikati ya uwanja na kutoa pasi yenye macho.. alikua anakaba kwa Akili nyingi sana..
Hongera kwake na kwa timu nzima kwa ujumla japo tulikua pungufu lakini Azam waliomba poo... Ikabidi watumie mbinu ya kupoteza muda
 
Wewe kolo mtiifu Leo utatamba Sana naona shemeji Yako kakuwezesha bando ni mwendo wa kuhara tu.
Bando ni la unlimited na hili ni juhudi zangu

Mi sio mtu wa kubustiwa kama nyie mnavyopewa supu za bure
 
Ahaahhahah wana Simba kaa mbaya na mtu wa utopolo...
Maaaanaaa wana hasira haooo
 
Back
Top Bottom