Bakhresa group mfano mzuri wa kuigwa


yupo mtu kama Saul wa Landmark, sidhani kama jamaa ana trace za ufisadi lakini ni tajiri
 
yupo mtu kama Saul wa Landmark, sidhani kama jamaa ana trace za ufisadi lakini ni tajiri

Kituko,

Pesa ya Sauli ni dili la Muluzi aliyekuwa Raisi Malawi ambae kesi ya Muluzi iko mahakamani sasa hivi!

Sauli sii msafi kiasi hicho!
 
Kwa msemo wa wafanyabiashara wengi ......ukifanya biashara halali kwa kulipa kodi inavyotakiwa Tanzania si rahisi kuwa tajiri kiasi hicho.....Malalamiko ni kuwa kodi ni kubwa sana na zinavutia ukwepaji kwa kila mfanyabiashara anayepata nafasi au kwa kupitiaajenti wake ndani ya TRA.....

Ninavyosikia mtego huu wa kukwepa kulipa kodi inavyotakiwa unawanasa wafanyabiashara wengi sana, na kwa namna inaweza kutoa picha kuwa wengi utajiri wao una walakini.

Sijui wana JF kuna ukweli wowote ju ya hili?
 


Hivi kumbukumbu zangu zinanikumbusha Mkemia Mkuu wa Serikali, somebody Fupi alikufa kwa kusema ukweli juu ya chakula kibovu !!! Hakukuwa na mkono wa Bahresa na Mohamed interprise?? hebu tukumbushane hapa!!!!
 
This JF.
 
This is JF.
 

Mi nadhani hizi ni fikra za kitumwa na tegemezi.

Let the man mind his own business as long as anafuata sheria za nchi.

Kuna mamlaka husika zilizopewa majukumu ya kukusanya kodi na kutoa huduma muhimu kwa umma.
 
Ushaleta suala la udini hapa.We kwako kila kitu ni waislam waislam...Kata issue,kama huna la maana just SHUT UP!

Relax mkuu.

Hapa JF we are free to talk openly on any subject. Constructively ofcourse.
 
Naskia ukitaka kufanya any business na Bakhressa at wholesale na sub-wholesale level, sharti uwe Muislam.

Kuna watu inabidi wajipachike majina ya kiislam ili wafanye biashara na Bakhressa.
 
mengi ana wazo zuri ila tatizo hii vita ya ufisadi imekuwa personalized mnoo..

siwapendi mafisadi lakini siungi mkono kelele za kupinga ufisadi zinavyofanyika.

mfano binafsi yangu hakuna ufisadi mbaya na mkubwa kama unaofanyika kwenye HALMASHURI ZETUU...fedha za maendeleo ya maji, barabara, afya, elimu hazifikii zaidi ya watu wachache (madiwani, watendaji wa halmashauri) kujilipa kwa vikao na tenda zao..

je mengi yupo wapi kukemeaa ufisadiii huu unaoumizaaa wananchi moja kwa mojaaaa kati maeneo husikaa...
 
Wadanganyika tuache mawazo ya kimaskini kwamba matajiri wengi tz ni mafisadi ama walishawahi kufanya dili chafu hapo nuyuma (either kukwepa kodi ama vypvyote vile). Kuna watu wanataka kujustify umasikini wao hapa (relatively) kwa kutuaminisha kwamba kila mwenye nacho basi kakipata ktk njia chafu.
Kuhusu ishu ya kodi, kwa jinsi ninavyofahamu biashara ama mfanyabiashara yeyote yule especially those who run their business professionally would manage their business in such a way to minimize tax thru legal means (Tax avoidance), na ndio maana kuna ma tax consultant wana JF.

Challenge ni kwa serikali ku manage vizuri hiyo kodi inayokusanywa ili iweze kufanya kazi inayotarajiwa na walipa kodi pamoja na wananchi kwa ujumla. Nawashangaa watu wanaomlaumu Bakharesa kwa kutosaidia shule,zahanati n.k huku pemba na unguja!! Jamani tuangalie ni kiasi gani cha vijana wa kitz waliopata ajira kupitia miradi ya Bakharesa, zunguka miji yote ya tz sasa hivi vijana wanashukuru uwepo wa huyu jamaa. Sasa hivi vijana wetu wabeba zege waliotapakaa mijini wanaweza angalau wakapata maji safi na salama kwa bei nafuu, na kuepukana na magonjwa mengi tu.

Kwa kifupi jamaa ameleta bonge la positive impact kwa watu wa chini kabisa!! Long live Bakharesa and your investments
"Hata foleni za darisalam sasa hivi hazichoshi sana kutokana na uwepo wa rambaramba kina kona ya jiji" (just kidding)
 
Nadhani wale waliotunga zile methali za kusema kiendacho kwa mganga.... na ile ya mavi ya kale..... walituandaa ktk hili maana walijua endapo kizazi kitafukuafukua na kupata mizizi ya shina (hata kama mti ukishakatwa) basi tujue kuwa shina hilo halitakua mti mkubwa tena... nani kasemaaa??
Hapa tunataka kuithibitishia dunia kwamba nchi yetu si masikini kihivyo ila tumekosa uongozi tulivu....
 
Kikojozi said:
Mi nadhani hizi ni fikra za kitumwa na tegemezi.

Let the man mind his own business as long as anafuata sheria za nchi.

Kuna mamlaka husika zilizopewa majukumu ya kukusanya kodi na kutoa huduma muhimu kwa umma.

Kikojozi,

..siyo mawazo ya kitumwa kumshauri Bakhresa kusaidia ktk shughuli za ujenzi wa taifa kama ujenzi wa mashule, vyuo, zahanati, au hospitali.

..Tanzania tuko nyuma ktk masuala ya Philantophy. kuna jitihada zimeanza kuonekana lakini zinaelekezwa zaidi ktk michezo na siyo huduma za jamii.

..nakushauri utafiti historia ya tajiri wa Marekani Andrew Carnegie ambaye alitoa mchango mkubwa ktk kuanzisha Carnegie Mellon Univ utaelewa nazungumzia kitu gani.

..uko sahihi kwamba kuna taasisi za serikali zinazoshughulika na utoaji huduma za jamii. lakini sidhani hata siku moja itafika tukaelemewa na wingi wa mashule,hospitali etc etc. kwa msingi huo bado tunapaswa kuhimiza michango ya watu binafsi.
 

Mkuu Joka,

Nakubaliana na wewe to some extent. Sina problem na Bakhressa kushauriwa.

Nnachosisitiza ni hiyo philanthropy afanye kwa hiari yake, sio kwa kushinikizwa eti kwasababu ana pesa nyingi.

Awe na uhuru wa kuitumia pesa yake atakavyo ilimradi havunji sheria za nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…