Bakhresa mfano wa kuigwa kutoka kuuza mbatata hadi kuwa bilionea wa kimataifa

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Posts
11,897
Reaction score
6,925


Matajiri wakubwa nchini ambao ni Rostam Azizi, Regnald Mengi, Mo na Bakhresa, katika kusoma historia ya maisha yao na jinsi walivyoanza kutajirika naelekea kuvutiwa zaidi na huyu Bakhresa ambaye kwa kweli ni sawa na kuanzia umachinga baada ya kuacha shule akiwa na umri wa miaka 14, na kwa umri huu dhahiri ni kama kiwango cha elimu ya msingi.

Mtaji wa kuuza Mbatata
Kwa umri aliokuwa nao wa miaka 14 kuamua kuacha shule na kufanya biashara ya kununua viazi vitamu kwa wakulima huko njiani na kupakia kwenye magari kidogokidogo kuleta kuuza Kariakoo na maeneo mengi ni jambo ambalo limo ndani ya uwezo wa walio wengi kati yetu. Hatua iliyofuata ya kuanzisha mgahawa dhahiri alifanikiwa kukuza mtaji huo wa kuuza mbatata, hatua ambayo ilisaidia kuwa na mapato zaidi yaliyomsaidia kufikia uamuzi wa kununua vinu vya kusaga nafaka vya kawaida tu kama wengi wafanyavyo. Serikali ilipokuwa bin taabani kushikilia mashirika ya umma, iliamua kulegeza kamba kuruhusu wazawa kuyanunua, ndipo Bakhresa alipoamua kununua vinu vya shirika la National Milling Corporation mradi mbao aliuendesha kwa ufanisi mkubwa hadi kufikia hatua ya kuwa na mitambo ya utengenezaji ice cream, pipi, vinywaji baridi, biasha ya madini nk. Hatua nyingine umiliki wa timu ya mpira ligi kuu taifa jambo la pekee katika nchi yetu ingawa ni jambo la kawaida katika nchi zilizoendelea kwa kampuni iliyopiga hatua kubwa kiuchumu. Kati ya matajiri wakuu wanne hawa, yeye pekee ndiye anayetoa ajira kubwa kwa vijana nchini.

Kwa kuangalia historia hii ya huyu Bakhresa dhahiri wengi tunaweza kujifunza kwake, kwano MO ametajirishwa na urithi wa wazazi wake, Mengi kazi ya uhasibu aliyofanya UK na Tanzania na hivyo kuna na upenyo wa kufikia alipo, na Aziz sina cha kuongeza kwani mengi yalishaandikwa hapa yanajulikana.

Njia za huyu Bakhresa nasema pametulia naweza kujifunza na kujaribu bahati yangu.
 
`Shukrani kwa historia fupi, ni wapi tunaweza kuisoma kwa undani zaidi?
 
`Shukrani kwa historia fupi, ni wapi tunaweza kuisoma kwa undani zaidi?

Hawa ndio mabilionea wanne vinara Tanzania
Mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Aziz (49), ametajwa kuwa ndiye tajiri namba moja Tanzania kwa sasa. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Jarida la Marekani la Forbes na kutoa taarifa yake juzi, Rostam amekamata nafasi hiyo na ya 27 katika Afrika akiwa na utajiri wa Dola za Marekani bilioni moja (Sh1.6 trilioni).


Mbunge huyo wa zamani wa Igunga, ameingia kwa mara ya kwanza katika orodha ya matajiri 50 wa Afrika ya jarida hilo, pamoja na wafanyabiashara wengine wa Tanzania, Reginald Mengi na Mbunge wa Singida Mjini (CCM), Mohamed Dewji ‘Mo'. Katika orodha hiyo pia yumo Said Bakhresa ambaye aliwahi kutajwa siku za nyuma. Rostam, ambaye aliachana na siasa mwaka 2011, amempiku Bakhresa, ambaye mwaka jana Jarida la Ventures Africa la Nigeria lilimtaja kuwa ndiye aliyekuwa tajiri namba moja wa Tanzania. Bakhressa katika kipindi hicho alikadiriwa kuwa na utajiri wa Dola 620 milioni (Sh971 bilioni).

Katika orodha hiyo ya Ventures Africa, Bakhresa alifuatiwa na Rostam, Mengi na mfanyabiashara mwingine maarufu, Ali Mufuruki. Mengi anashika nafasi ya pili kwa Tanzania na ya 34 Afrika akiwa na utajiri wa Dola 550 milioni (Sh861 bilioni). Forbes linaonyesha kuwa Bakhresa amefungana na Mo katika nafasi ya tatu ya orodha ya matajiri wa Tanzania na ya 38 kwa Afrika, wote wakiwa na utajiri wa Dola 500 milioni (Sh783 bilioni). Rostam, Mengi na Bakhresa hawakupatikana jana kuzungumzia suala hilo huku Mo akisema kwamba asingeweza kuzungumzia suala hilo kwa kuwa jana alikuwa katika mapumziko ya Sikukuu ya Ashura.

Tajiri wa Nigeria, Aliko Dangote, ambaye anajenga Kiwanda cha Saruji huko Mtwara ndiye anayeshika nafasi ya kwanza katika orodha ya Afrika, akiwa na utajiri wa Dola20 bilioni (Sh31.7 trilioni), akifuatiwa na familia ya Johanny Rupert ya Afrika Kusini yenye utajiri wa Dola7 bilioni (Sh10.7 trilioni) na Nick Oppenheimer, pia wa Afrika Kusini mwenye utajiri wa Dola 6.6 bilioni (Sh10.3 trilioni).

1)Rostam Aziz
Jarida la Forbes limeripoti kuwa utajiri wa Rostam unachangiwa zaidi na biashara ya mawasiliano ya simu za mkononi, ujenzi na uchimbaji wa madini. Anamiliki asilimia 35 ya hisa katika Kampuni ya Simu za mkononi ya Vodacom. Ni kampuni inayoongoza kwa biashara ya simu za mikononi nchini Tanzania ikiwa na wateja zaidi ya milioni 9.5. Pia anamiliki Kampuni ya Caspian, ambayo inafanya kazi za kuchimba madini katika migodi inayomilikiwa na Kampuni za BHP Billiton na Barrick Gold. Pia ana hisa katika Kampuni ya Hutchison Wampoa inayofanya kazi za kupakua mizigo bandarini na anamiliki majumba nchini na katika nchi za Mashariki ya Kati.


2) Mengi
Ni Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni za IPP. Utajiri wake unatokana na kumiliki vyombo vya habari, kiwanda cha vinywaji baridi na madini. Mengi anamiliki magazeti kumi na moja, vituo vitatu vya televisheni na takriban vituo 10 vya redio. Pia ana mgodi wa madini ya dhahabu na viwanda vya CocaCola. Kwa mujibu jarida hilo, Mengi alizaliwa katika familia maskini na baadaye kusomea uhasibu huko Uingereza na kufanya kazi huko. Alijiunga na Chama cha Wahasibu cha Uingereza kabla ya kurejea Tanzania mwaka 1971 na kuajiriwa na Kampuni ya Ukaguzi ya Coopers & Lybrand Tanzania (sasa Price Water House Coopers) hadi mwaka 1989, alipoacha kazi na kujikita zaidi katika biashara.


3) Bakhresa
Said Salim Bakhresa ni mwasisi na Mwenyekiti wa Kampuni ya Bakhresa Group na ana utajiri wa Dola500 milioni (Sh783 bilioni). Ni kampuni kubwa inayoajiri zaidi ya watu 2,000 ikijishughulisha zaidi katika kusaga nafaka, kusindika matunda, usafiri wa meli na biashara ya mafuta. Pia kwa kutengeneza pipi na ice cream. Bakhresa aliacha shule akiwa na umri wa miaka 14 na kuanza biashara ya kuuza viazi mbatata. Baada ya hapo alifungua mgahawa na baadaye kuingia katika biashara ya kusaga nafaka.


4) Mo
Mafanikio yake yamechangiwa zaidi baada ya kuendeleza mali ya wazazi wake. Anafanya biashara ya nyumba, kuuza mazao na viwanda vya mafuta. Mo alirejea Tanzania baada ya kumaliza masomo yake katika Chuo Kikuu cha Georgetown, Marekani na kuendeleza biashara ya maduka ambayo yalianzishwa na baba yake. Alinufaika baada ya kununua viwanda vilivyobinafsishwa na Serikali. Alivifanya viwanda hivyo kutengeneza faida na kuinyanyua Kampuni ya Mohamed Enterprises (MeTL) kuwa miongoni mwa kampuni zenye mafanikio makubwa Tanzania. Mo pia anajihusisha na biashara ya usambazaji bidhaa, viwanda vya nguo na kilimo.


Jarida hilo lilipiga hesabu za utajiri wa wafanyabiashara hao kwa kuangalia thamani ya bidhaa zinazouzwa na kampuni zao, mikataba yao na hasa wale walio kwenye sekta ya mafuta na ukubwa wa kampuni zao.


 
Ndugu zangu maTAIRI wana Stori ndefu sana! Hakuna anaeweza kusema ukweli namna alivyotajirika! Km ni mbatata cdhani km aliuza Peke yake kipindi hicho Nawengine hadi leo naamini bado wanauza mbona hwajafanikiwa! Mimi namheshimu2 mtu aliefanikiwa 7bu najua amepambana sana! lkn siamini atakachonambia kwamba ndo 7bu ya Utajiri wake! Ukweli ni kdg sana!
 

Well said,Tajiri anajua jinsi alivyotajirika hayo anayosema mengi ni porojo tu! Hv wale wachina waliokamatwa mikocheni na pembe za ndovu zenye thamani ya 5.4b mtaani kwao si wanawajua kwamba ni wafanyabiashara wa vitunguu na ndimu? Sasa watu wa design hii wakitajirika simply anasema nilianza kuuza ndimu na vitunguu,matajiri wengi wanazuga na biashara za kuonekana kuficha ufisadi wao wanaofanya!! Nawakubali wote kwa utajiri wao ila jinsi walivyofanikiwa wanavyotuongopea sikubaliani nao pasee!!
 

Real Talk,
Utajiri una siri sana. Watu hawatoki hivi hivi. There is always an X factor behind / somewhere which made them rise, after that the rest of the story becomes legit.
 
MwenyeEnzi Mungu anamruzuku amtakae na anamyima amtakae !! " Na Mkimshukuru kwa machache atawaongezea zaidi "
Hazina yake haina mwisho...!! Jipange ina a RIGHT place and RIGHT time. God blessings.
 

Mkuu salama, Ni kweli matajiri wana hadithi ndefu kama ilivyo kwa mwananchi yeyote yule wa kawaida.

Na si kweli kuwa hakuna anayeweza kusema jinsi alivyotajirika, wapo wenye utajiri ambao unathibitika wameupata vipi. Tuwe makini kwenye michango yetu siyo tu kutoa general statement kama hizi zenye mapungufu makubwa ya fikra.

Pia ni makosa kawafananisha wauza mbatata wote wako sawa kwa sababu tu wote wanafanya biashara sawa. Kuna vitu vingi vinavyokuwa ama ndani ya biashara au kwa mfanyabiashara. Biashara ina fikra, malengo, dhamira, shauku na pia nidhamu. Zaidi inahitaji maono ya mfanyabiashara,Je anataka biashara yake imkifikishe wapiau afike wapi?

Ni kweli kabisa wanastahili heshima sababu wamepambana mpaka kufika hapo walipo. Biashara si kitu cha mzawa kama huna roho ngumu, shauku na ujasiri uwezi dumu.

Kuamini au kutokuamini hiyo ni wewe na jinsi ulivyojiwekea kwenye nafsi yako. Kama ujiamini wewe mwenyewe ni vigumu sana kumuamini mtu mwingine. Isipokuwa kama utaweza leta au unao ushahidi uliotofauti na maelezo yake. Basi nitakuwa sina budi kuamini alichokieleza sababu kinawezekana, kuna nini unachokiona alichoeleza Bakhresa kina miujiza.

Jiamini ndugu yangu achana na hizi fikra nyepesi nyepesi.
Inasikitisha sana unapoweka comments kama hizi bila kubeba fikra ni hatari sana.
 
Mkuu wangu EWGM's. Niko salama kabisa! Stori km hz za watu kuanza kuuza Mbatata hadi kuwa maTAJIRI ni Stori zakuwaTIA MOYO watu ambao wanaanza kupambana ktk kutafutafuta lkn kwa mtu anaejua kutafuta PESA! haingii AKILINI huo ndo ukweli Matajiri wengi hawawezi kukwambia ukweli anajua naww ukipita humo utakuwa km yy! Matokeo yake ndo km hivyo anakwambia aliuza mbatata peke yake! KWELI?
 
Mmmmhhh jamani mi ninapita tu kutafuta ujuzi wa wengine hasa walio feli na waliofanikiwa katika maisha, ndo kwanza nimemaliza masomo flanflan mda si mrefu, ndo nataka nianze ili siku zijazo nifike huko waliko na zaidi!!!! sasa hapa kwenye wachangiaji ndipo penye changamoto!!!:shocked: :shocked: :shocked: :shocked:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…