Bakita lataka matumizi ya neno kisimbuzi badala ya king'amuzi na "dijiti" badala ya dijitali..

Bakita lataka matumizi ya neno kisimbuzi badala ya king'amuzi na "dijiti" badala ya dijitali..

sosoliso

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2009
Posts
8,540
Reaction score
9,473
Baraza la Kiswahili la Taifa limezitaka mamlaka zote zinashughulika na kucimamia teknolojia ya habari (Tehama) pamoja na vyombo vya habari (ikiwa ni pamoja na JF) kusitisha matumizi ya maneno "king'amuzi" na "dijitali" kwa kuwa hayasadifu maana halici kwa lugha ya kiswahili..

Istilahi sahihi ni "
kisimbuzi" na "dijiti"..

Kwa hiyo wana JF mnaombwa sana kuzingatia matumizi sahihi ya istilahi hizo..
 
kwahiyo king'amuzi ninini? nielewesheni mimi na wengine wenye uhitaji wa maarifa haya
 
Hivi lugha imeshakoma kuwa sauti za "nasibu"?
 
BAKITA watakuwa na homa za manjano, lugha ni sauti za nasibu na kamwe neno huwa halikataliwa ispokuwa kama litakuwa chukizo au litakuwa lisilo faaa mbele ya jamii, kwaiyo waliiache tu king'amuzi litawale maana tangu linachukua kasi wwalikuwa wapi? na wakati kila mwezi wanatakiwa wawe wanatoa jarida la maendeleo ya kiswahili lakini wamelala tu, kwaiyo hapo lugha itakuwa iekuwa na kuongezeka msamiati, maneno king'amuzi na dijitali yaendelee na pia kisimbuzi na dijiti yaendelee tuu.
 
kisimbuzi ni neno lililokaa kianalogia mno.digitali ndio mpango mzima.
 
Hivi lugha imeshakoma kuwa sauti za "nasibu"?
Dah! Mkuu sijui watu kama wanaelewa hii.
Nikiwa darasa la tatu katika somo la Kiswahili nilifundishwa hivi:
"Lugha ni sauti nasibu zenye umaana". Maana yake ni kwamba hapakuwa na kikao kilichokaa kusema hii tuiite kalamu, hii tuiite nyumba, n.k. Kila kitu kilitokea kwa bahati nasibu.
Siku hizi watu wanakaa mkutano kabisa na posho wanalipwa ili kuilazimisha jamii kukiita kitu fulani jina wanalolitaka wao.
Hii sio tafsiri ya lugha.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Back
Top Bottom