Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,211
- 3,611
Ukiongea au kuandika maneno yenye kufanana na hayo huku akili imezingirwa na mawazo hasi utapata tabu sana kuimudu lugha."Kuna haja kubwa..."
Hicho Kirai (phrase) hakifai kwenye mawasiliano rasmi na ya staha.
Ebu ona hii:-
"Kuna haja kubwa"
Tafsiri zake mchanganyiko:-
1. Kuna uhitaji mkubwa.
2. Kuna choo (stool) kikubwa.
Kwa mgeni katika nchi anayejifunza lugha ya Kiswahili atapata shida ya Kirai (phrase) hicho na vingine vyenye muelekeo kama huo.
Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
Ushauri wa Baba wa taifa Mwl. Nyerere Gwiji wa lugha za Kiswahili, Kiingereza cha Oxford na Kilatini aliwahi kuitahadharisha BAKITA kuhusu matumizi ya msamiati "Imepelekea" kwamba unatumika isivyokusudiwa ktk Isimu.Ukiongea au kuandika maneno yenye kufanana na hayo huku akili imezingirwa na mawazo hasi utapata tabu sana kuimudu lugha.
NB:Sijakushauri upuyange lugha.Ongea kwa kuamini unalenga mawazo mazuri na utafanikiwa.
Mfano wako hauna mfanano.Na ndipo hapo unapatwa na mzingiro.Ushauri wa Baba wa taifa Mwl. Nyerere Gwiji wa lugha za Kiswahili, Kiingereza cha Oxford na Kilatini aliwahi kuitahadharisha BAKITA kuhusu matumizi ya msamiati "Imepelekea" kwamba unatumika isivyokusudiwa ktk Isimu.
Mfano:-
Hali hiyo imepelekea kuwepo na changamoto hizi.
Badala ya:
Changamoto hizi zimekuwepo kufuatia hali hiyo.
Akafafanua kuwa "imepelekea" ni tangible verb (tendo la kuonekana kwa macho) kwamba ni makosa kulitumia kama intangible verb.
NB:
Sijajua akili ya Mwl ilikuwa imezingirwa na mawazo gani?
Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app