Watu wa Baraza la Kiswahili la Taifa nakuombeni muweke neno "Ufisadi" kama mbadala ya neno Uhujumu uchumi. Hii inatokana na kutumika kwa kasi kubwa na kuzoeleka midomoni mwa watu wengi hasa waandishi wa habari, watangazaji na wanasiasa kwa ujumla. Ninapendekeza kwamba neno ufisadi liwe na maana mbili ya kwanza uhujumu uchumi, ya pili ni uharibifu wa ndoa za watu kwa uzinzi. Liwekwe kwenye kamsi rasmi pamoja na msamiati mpya wa kujivua gamba, kama mlivyoweka neno kung'atuka.