Nyundo_tz
JF-Expert Member
- Jul 14, 2009
- 640
- 20
Kartika Sari Dewi Shukarno Tuesday, September 29, 2009 5:09 AM
Mrembo wa vivazi wa Malaysia ambaye alikamatwa akinywa pombe hadharani atachapwa bakora sita kama kawaida pamoja na shinikizo la mataifa ya magharibi kupinga adhabu hiyo. Mahakama ya kidini ya Malaysia imeamuru mrembo wa vivazi wa Malaysia aliyekamatwa akinywa pombe hadharani, achapwe bakora sita kama adhabu yake ilivyotolewa pamoja na kwamba kesi hiyo iliamsha mgogoro mkubwa wa kimataifa.
Kartika Sari Dewi Shukarno, 32, alihukumiwa na mahakama ya kidini miezi sita iliyopita kuchapwa bakora sita baada ya kukamatwa akinywa pombe hadharani kwenye klabu ya starehe.
Kartika atakuwa mwanamke wa kwanza nchini Malaysia kukumbana na adhabu ya kuchapwa bakora. Wanaume wengi washachapwa bakora nchini humo kwa kuvunja sheria mbali mbali za kiislamu.
Awali Kartika alinusurika adhabu hiyo baada ya serikali kuingilia kati na kudai adhabu hiyo ni kali sana na itaharibu sifa ya Malaysia kimataifa.
Lakini baada ya mahakama ya sheria za kiislamu katika mji wa Kuantan ambao Kartika alikamatwa akinywa pombe, kukata rufaa kupinga Kartika kuachiwa huru, kesi hiyo ilipitiwa tena na mahakama iliamuru Kartika achapwe bakora sita kama sheria zinavyosema.
Tarehe ya Kartika kuchapwa bakora hizo bado haijapangwa.
Malaysia ina mifumo miwili ya sheria. Mfumo mmoja ni wa kawaida na mfumo mwingine unafuata sheria za kiislamu kwaajili ya waislamu wanaokiuka misingi ya kiislamu.
Raia wa Malaysia wenye asili ya China na India ambao wengi wao si waislamu wao wako huru kunywa pombe muda wowote bila kubughudhiwa.
Hali ni tofauti kwa raia wa Malaysia ambao ni waislamu kwani matendo yao yoyote yanayokiuka misingi ya kiislamu huamriwa na mahakama za sharia za kiislamu.
Source: AFP